Wamachinga: Tuko tayari kuandamana 2025 Rais aendelee kubaki madarakani

Wamachinga: Tuko tayari kuandamana 2025 Rais aendelee kubaki madarakani

Dkt Magufuli alishasema hatoongeza muda, hivi wanaosema aongeze muda wanafikiri wanamfurahisha nani? Nadhani misingi aliyoijenga Dkt. Magufuli ni muhimu tujiandae namna ya kuilinda na kuiendeleza.
 
Mimi kama mmachinga napinga hilo. Hicho kikao cha kukubaliana mlikaa na nani?
 
Dkt Magufuli alishasema hatoongeza muda hivi wanaosema aongeze muda wanafikiri wanamfurahisha nani? Nadhani misingi aliyoijenga Dkt Magufuli ni muhimu tujiandae namna ya kuilinda na kuiendeleza
Yeye mwenyewe Rais ndio anaesuka mipango ya kukaa muda mrefu madarakani.
 
Wamachinga wa Dar wamesema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali na kutengeneza mazingira bora ya kufanya kazi.

Wamesema hakuna Rais aliyefanyia wema kama Rais Magufuli hivyo wako tayari kuandamana ili Rais Magufuli abaki madarakani.

Aidha wamachinga wamesema uongozi waliokuwa nao kwa takribani miaka saba ni uongozi wa kiuanaharakati hivyo wanataka kuchagua viongozi kwa kukubaliana.

Matatizo mengine waliyoyataja ni pamoja na kuwa na namna rasmi ya kukopeshana ili kuweza kuongeza mitaji ya biashara.


Kweli kabisa.
Lazima wamwongezee muda.
Walikuwa wanalala nje lakini ndani ya uongozi wa JPM wamefanikiwa kujenga karibu wote.
Walikuwa wanapita madirishani kugombea daladala lakini sasa wanakwenda Kariakoo kufuata mali kwa vigari vyao binafsi.
Sasa bidhaa hususani vyakula bei ni kitonga.
Mafuta, mchele, sukari bei cheee
 
Hata Museven kuna machinga wapo tayari kufa kwaajili yake.
Hata Idi Amini Dada alikuwa na wapambe wengi tu.
Mwamuzi wa haki huwa ni democrasia ya kweli.
Lakini tukisema wapambe waamue future yetu nchi itaendelea kunung'unika daima.
Trump asingetoka pale kama USA isingekuwa na misingi imara ya democracy.

Wapambe huwa mnajali matumbo yenu tu na hamnaga aibu.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hilo picha tunachezewa, hao sio Wamachinga, watu wanatest kupima reaction,

Ila kubwa zaidi, Jamaa bado yupo yupo hata baada ya 2025.
 
Mkuu urais ni taasisi nyeti,kuna few chosen vessels like JPM ndo wanafaaa,kwangu Mimi kazi Yangu inanitosha,urais tumwachieni JPM.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Basi mkuu iko hivi, kama wewe huwezi kuwa rais kuna wengine wanaweza. Watanzania tupo zaidi ya milioni 60 hivyo tupo tunaoweza kuwa marais. JPM hawezi akawa mtu pekee kati ya watu 60,000,000 mwenye akili ya kuwa rais.
 
sioni ajabu kwa wao kuliunga hili mkono maana makontena yote ya mali to ulaya na china hukabidhiwa wao kwa siri na importer ili wauze kwa mtindo wa kimachinga,hivyo serekali kukosa matrilion kutoka kwa wafanya biashara hao dukani panauzwa frige na machinga anauza frige dukani lazima uwe na mashine ya risiti kwa mmachinga risiti sio lazima kuwa na mashine ya risiti duka lina mali ya milioni 20 na mmachinga ametandaza mali za milioni 20
 
Machinga na wafanyabiashara wote lazima mjifunze kuishi bila kukariri aina moja ya maisha, akifa je mtaandamana kwenda nae ndani ya kaburii!!?
BOUBLE STANDARD YA HALI YA JUU SUALA HILI KIUNDANI LINALAZIMISHA HATA MFANYA BIASHARA MKUBWA AWE MACHINGA ILI AEPUKANE NA RABSHA MBALI MBALI KUNA UBAYA GANI HAPO KARUME KUKAJENGWA MJENGO UTAKAOKUWA NA FREMU 500 ILI KUWARASMISHA RASMI KIMPANGILIO
 
Wamachinga wa Dar wamesema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali na kutengeneza mazingira bora ya kufanya kazi.

Wamesema hakuna Rais aliyefanyia wema kama Rais Magufuli hivyo wako tayari kuandamana ili Rais Magufuli abaki madarakani.

Aidha wamachinga wamesema uongozi waliokuwa nao kwa takribani miaka saba ni uongozi wa kiuanaharakati hivyo wanataka kuchagua viongozi kwa kukubaliana.

Matatizo mengine waliyoyataja ni pamoja na kuwa na namna rasmi ya kukopeshana ili kuweza kuongeza mitaji ya biashara.


Ohooo!! Imeanza kwa Trump, Donald!! King of the World!
 
Putin yeye ameisha maliza kazi, mpaka kuleeeee! 2034. "Kuna mwenye swali?"
"Hakuna Mkuu"
"Haya kaeni chini"
"Asante Mkuu"
 
JPM akiamua kuchukua njia hiyo itakua Tanzania haina tofauti tena na Burundi, Uganda, Rwanda, Sudan, Congo hatutakua na lingine la kujivunia, atakua ameturudisha nyuma miaka 50, pamoja na umasikini wetu na elimu mbovu ya CCM na uminyaji wa haki za binadamu bado tulikua na la kujivunia kwamba Rais anakaa miaka 10 tu.
Huwezi kumlinganisha mtoto aliyekulia Manzese, Buguruni na yule aliyekulia Oyster bay.
Watanzania ni watu waliokulia Oyster bay. Usiombee vurugu kama hizo, huna uzoefu nazo!
Angalia upepo wa Ulimwengu unavyokwenda my friend!
Amerika, Urusi, the big Nations!
Tamasha la Ulimwengu limebadilika!
Unaweza usiwe na nia kabisa, lakini watu waka- force uwe na nia, - upende usipende!
 
Daah kumbe kumi ni Michache sasa wanazungumzia kutanua goli tuu muda wote na hilo linawezekana kwa jinsi ya avyotengenezwa mazingira kuanzia bungeni kila mahara...
 
Wabongo bana ajabu sana!
Mara ooh muda si mrefu Covid itamuondoa, Mara ooh anataka kuongeza 10, sasa which is which banaa!?
Mbona mnatuchanganya?
 
Back
Top Bottom