ryan riz
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 423
- 683
Ikiwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya soko jipya la machinga linaendelea, ila limegubikwa na sintofahamu tokana na zoezi hili
Kipindi cha awali wamachinga wanaofanya biashara soko la jioni Nyerere square waliandikishwa kwa usimamizi madhubuti wa aliyekuwa mkuu wa mkoa Antony mtaka kuhakikisha hakuna upendeleo kwa wote wanaofanya biashara maeneo hayo.
Kipindi yupo majina yalitoka na watu waliona majina yao.waliitwa kwenye kikao cha ugawaji wa maeneo na kupewa namba ya vibanda vyao.
Kikao hicho alikuwepo waziri wa fedha MWIGULU NCHEMBA alikuwepo kushuhudia zoezi hilo na pia alitoa AHADI kuwa mama SAMIA ametoa bilioni 2 kumalizia soko lote likamilike.
Sasa kizungumkuti kimetokea baada tu ya mkuu wa mkoa kuondoka,majina ya wale waliopewa vibanda awali yameandikwa VERIFIED lakini hawajapiga picha ya vitambulisho vya soko lile na kuambiwa waondoke watapigiwa simu. Huku wale waliondikwa kwenye majina yao ACTIVE wakipiga picha na kupatiwa vitambulisho vya soko hilo wakati wote wanafanya biashara eneo hilo miaka na miaka toka zamani.
Sintofahamu hiyo inakuja kwanini huyu wa active apewa na huyu wa verified asipewe na wote awali walipewa maeneo kabla hata ya soko halijakamilika vizuri ila baada ya kukamilika wanatemwa?