Wamama wajiponza wenyewe kwa Polisi bila kujua

Wamama wajiponza wenyewe kwa Polisi bila kujua

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Wazima humu!!!!

Jana nilipita maeneo ya soko kuu la Mwanza mjini nikashuhudia wamama wawili wauza ndizi za kupika wakijiponza wenyewe hadi kutiwa nguvuni.

Akina mama hao wauza ndizi za kupika (matoke) huwa wanakawaida kama walivyo wachuuzi wengine wakiona mteja kila mmoja anajitahidi kumshawishi mteja huyo anunue bidhaa zake. Miongozi mwa wateja alipita askari polisi wa kike (WP) alikuwa amevaa kiraia. Basi akapokelewa na mama aliyekuwa amekaa mwanzoni (huwa wanajipanga kama mstari hivi). Mama mwingine ambaye alikuwa mbele kidogo akaanza kumtolea lugha chafu yule mwenzio aliyempokea mteja/polisi, "Mama Robhi acha ujinga, huyo dada ni mteja wangu wa siku zote kwa nini umemdaka huko? Unatabia mbaya sana ya kupenda kudaka daka wateja ambao sio wa kwako..." na matusi mengine mengi. Yule mteja/polisi akamjibu yule mtoa matusi kuwa mimi na nunua popote pale na nyie wote mnauza ndizi yawezekana siku nyingine nitanunua kwako. Mama mtoa matusi hakuridhika akaendelea kumtukana mwenzio, mwishoe ikifikia "tena wewe naweza kukupiga mimi" akanyanyuka akamfuta yule mwenzie aliyekuwa anamhudumia mteja/polisi akampiga kofi, yule naye hakukubali kupigwa, akamrudishia basi ikawa zogo.

Saaaalaaaaleee! bila kutegemea mteja/polisi akabadilika!!! "MIMI NI ASKARI POLISI, (akatoa kitambulisho) SASA TWENDENI HAPO KITUO CHA POLISI CHA PAMBA MTOE MAELEZO KWA KOSA LA KUPIGANA HADHARANI NA KUTOA LUGHA YA MATUSI"

Wamejiponza bila kutegemea wadada wale!!!
 
NINGEPENDA KUJUA HADITHI/STORY HII YATUFUNZA NINI....!!!
Kuwa tusipigane,Kutukanana au Kugombea wateja???!
Sio hadithi kama unavyodhani, ni tukio la ukweli la jana. Sio hadithi ya kufikirika ujue weee Perfectz
 
Ndio mana tunaambiwa usimdharau usiyemjua
Shunie, mie nilicheka sana yule dada alivyobadilika kutoka mteja na kuvaa upolisi, hahahahahahahha. Isingekuwa nina haraka nilitamani niinde hadi karibu na kituo nione kama wataswekwa ndani au watawachukua maelezo na kuwaachia wakaendelee na kuuza ndizi zao, na hasa ikizingatiwa ilikuwa nyakati za jioni.
 
picha za wakina mama waliopigana au video maana lazima kyuma au angalau kyupi zilionekana
Sikufanikiwa kupata picha na wala siku na hilo wazo, kwanza sehemu yenyewe kuna msongamano, kiasi kwamba ugomvi wao ungedumu kwa dakika nyingi ungesababisha wachuuzi wengine kupoteza mali zao
 
Shunie, mie nilicheka sana yule dada alivyobadilika kutoka mteja na kuvaa upolisi, hahahahahahahha. Isingekuwa nina haraka nilitamani niinde hadi karibu na kituo nione kama wataswekwa ndani au watawachukua maelezo na kuwaachia wakaendelee na kuuza ndizi zao, na hasa ikizingatiwa ilikuwa nyakati za jioni.
Halo ndio ulipokosea ungeenda tu mpaka counter teh teh
 
Shunie, mie nilicheka sana yule dada alivyobadilika kutoka mteja na kuvaa upolisi, hahahahahahahha. Isingekuwa nina haraka nilitamani niinde hadi karibu na kituo nione kama wataswekwa ndani au watawachukua maelezo na kuwaachia wakaendelee na kuuza ndizi zao, na hasa ikizingatiwa ilikuwa nyakati za jioni.
Nahisi kama alikula kwanza ili wakati amewachengia wasimdai ela ya chakula
 
Back
Top Bottom