Wazima humu!!!!
Jana nilipita maeneo ya soko kuu la Mwanza mjini nikashuhudia wamama wawili wauza ndizi za kupika wakijiponza wenyewe hadi kutiwa nguvuni.
Akina mama hao wauza ndizi za kupika (matoke) huwa wanakawaida kama walivyo wachuuzi wengine wakiona mteja kila mmoja anajitahidi kumshawishi mteja huyo anunue bidhaa zake. Miongozi mwa wateja alipita askari polisi wa kike (WP) alikuwa amevaa kiraia. Basi akapokelewa na mama aliyekuwa amekaa mwanzoni (huwa wanajipanga kama mstari hivi). Mama mwingine ambaye alikuwa mbele kidogo akaanza kumtolea lugha chafu yule mwenzio aliyempokea mteja/polisi, "Mama Robhi acha ujinga, huyo dada ni mteja wangu wa siku zote kwa nini umemdaka huko? Unatabia mbaya sana ya kupenda kudaka daka wateja ambao sio wa kwako..." na matusi mengine mengi. Yule mteja/polisi akamjibu yule mtoa matusi kuwa mimi na nunua popote pale na nyie wote mnauza ndizi yawezekana siku nyingine nitanunua kwako. Mama mtoa matusi hakuridhika akaendelea kumtukana mwenzio, mwishoe ikifikia "tena wewe naweza kukupiga mimi" akanyanyuka akamfuta yule mwenzie aliyekuwa anamhudumia mteja/polisi akampiga kofi, yule naye hakukubali kupigwa, akamrudishia basi ikawa zogo.
Saaaalaaaaleee! bila kutegemea mteja/polisi akabadilika!!! "MIMI NI ASKARI POLISI, (akatoa kitambulisho) SASA TWENDENI HAPO KITUO CHA POLISI CHA PAMBA MTOE MAELEZO KWA KOSA LA KUPIGANA HADHARANI NA KUTOA LUGHA YA MATUSI"
Wamejiponza bila kutegemea wadada wale!!!