Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Lakini pia hao watu wanasifika kwa kupenda kamserereko mpaka kujihusisha na mambo yanayotweza utu wao mfano huyo dimpozi pozi kwa pozi
Kuna jambo huwa ni mila, utamaduni na desturi ya kabila fulani. Na kuna jambo huwa ni tabia na mwenendo wa mtu fulani. Kwahiyo kama kuna jambo ambalo amefanya dimpoz basi amelifanya kutokana na tabia na mwenendo wake, ila sio kwa mila, utamaduni na desturi ya kabila lake. Nafikiri umenielewa bruh.
 
Pamoja na mbwembwe zote hizi lakini ndio kabila pekee ambalo halina lugha yake ya asili yani kilugha chake kama ilivyo wasambaa-kisambaa,wagogo-kigogo etc
 
Suala la ujasiri ni sifa ya Wakurya (kanda maalum) na mahasimu wetu wamasai pekee. Nyie wengine mnaongopa kujipa sifa ya ujasiri!
 
Wabwali, wakusu, wamasanze na wabembe hao wote ni jamii ya wamanyema bruh. Kama wewe ndo haujui uulize.
Hujui kitu wamanyema wanatokea Kasongo DRC wakati wabwari wanatokea Burundi
 
Pamoja na mbwembwe zote hizi lakini ndio kabila pekee ambalo halina lugha yake ya asili yani kilugha chake kama ilivyo wasambaa-kisambaa,wagogo-kigogo etc
Lugha ya asili ipo, hakuna kabila la kiafrika ambalo halina lugha ya asili, isipokuwa kiswahili ndio kimeimeza lugha yao. Leo hii hata vijana wa kizaramo wengi ukiwauliza hata salam ya kizaramo hawajui sababu, na wao babu zao waliendeleza sana kiswahili na kukifanya ndio lugha yao ya nyumbani.
 
bebi bebi bebi ndagushima chane ommy dimpo kaimba kiha hapo na sio kizaire aka kicongo
 
Yah..kn mzee mmj yuko tmk
Sahv anauza spare za machine(jina kapuni)utajiri wake ulitokea kwenye uwizi kwenye treni na pembe za ndovu

Ova
 
Tanzania ukitoa wahzabe na wagogo, makabila yaliobakia yote yalitoka sehemu mbali mbali za afrika. So kama wewe sio mmoja wa makabila hayo niliyoyataja hapa, basi hoja yako haina mashiko mkuu.
wahadzabe wana asili ya nchi za kusini,hata lugha zinafanana ,wanafanana hata na makhirikhiri
 
wahadzabe wana asili ya nchi za kusini,hata lugha zinafanana ,wanafanana hata na makhirikhiri
Afrika imeanzia juu (kaskazini + magharibi) kushuka chini (mashariki + kusini) kwahiyo hao wa kusini walianzia tanganyika (wahadzabe) wakateremka hadi kusini. Kumbuka historia inasema mifupa na hata nyayo za binadam wa kale kabisa zilipatikana ("Tanga", Tanganyika) Kwahiyo usishangae pengine hao wa kusini na sehem zingine za afrika wanaweza kuwa ni wahadzabe ambao walitoka Tanganyika zaman sana na kusambaa sehem zingine za Afrika ikiwepo hiyo kusini kutafuta chakula nk. Ndio maana hayati Magufuli kwa kutambua uchakachuaji wa historia yetu, alitakaa wataalam wake tena chini na kuiandika upya. Haiwezekani Tanzania tu ndio iwe nchi pekee ambayo kila kabila eti limetoka nchi nyingine.
 
Mhhhh. Wabwari wanatokea Burundi
Katiba ya burundi inatambua makabila matatu tu, yani watusi, wahutu na watwa. Hao wengine unawatambua wewe tu, lakini warundi wenyewe hawawatambui. Na hii sio kwa Burundi tu hata nje ya Burundi kwa mfano uki google kuhusu makabila ya Burundi, google itakuonesha makabila matatu tu niliyoyataja mimi hapo juu. Hao wabwari, wabembe nk ni migrants tu walioingia Burundi kipindi cha utumwa na ukoloni. Ila hawana asili na wala hawana uhusiano wowote na warundi. Wewe unaongea kwa hisia zako, mimi naongea kupitia fact za warundi wenyewe kwenye google, na pia wabeleji wenyewe ambao walitawala nchi zote mbili za Burundi na Congo. Hapo chini imeandikwa kwa kifaransa na wazungu wenyewe waliotawala nchi zote mbili, kwahiyo ukiachilia mbali warundi hawawatambui wabwari kama unavyosema ww lkn pia na wakoloni wanatambua kuwa ubwari walipotokea wabwari ipo Congo.
 

Attachments

  • Screenshot_20220610-112130.jpg
    47.8 KB · Views: 26
  • Screenshot_20220610-113223.jpg
    44.9 KB · Views: 21
Yah..kn mzee mmj yuko tmk
Sahv anauza spare za machine(jina kapuni)utajiri wake ulitokea kwenye uwizi kwenye treni na pembe za ndovu

Ova
Dah.. kwahiyo mkuu makabila mengine hayana wezi?
 
Haya unayoongea ni ya miaka hii, ila kuanzia 2000 kushuka chini maeneo mengi ya nchi, hakuna watu waliokuwa wanafahamu kabila linaloitwa waha.
Kwa taarifa yako utambulisho wa kabila ni lugha. Wamanyema wanaongea lugha gani?
 
Pamoja na mbwembwe zote hizi lakini ndio kabila pekee ambalo halina lugha yake ya asili yani kilugha chake kama ilivyo wasambaa-kisambaa,wagogo-kigogo etc
Ndo maana hawana sifa ya kuwa kabila.
 
Kama msikiti wa manyema ulijengwa kabla ya wakoloni na wakoloni( Waarabu ) ndio wenye dini yao sasa hao wamanyema uislam waliujulia wap???
 
Pamoja na mbwembwe zote hizi lakini ndio kabila pekee ambalo halina lugha yake ya asili yani kilugha chake kama ilivyo wasambaa-kisambaa,wagogo-kigogo etc
Kama unamaanisha lugha moja ni kweli Wamanyema hatuna lugha moja ya asili kama ilivyo kwa Wachaga ila tofauti na Wachaga sisi tunayo lugha unganishi "lingua franca" Kiswahili cha lahaja ya kiungwana, pia kwa mfanano na Wachaga tunazo lugha zaidi ya moja kufuatana na kabila dogo la ndani la kimanyema, mf. Mimi ni Mgoma na huzungumza Lugha ya Kigoma ambayo pia kiisimu hutambuliwa kama lahaja ya Lugha ya Kizyoba kama ilivyo Kibwari(Kabwari) na Kimasanze(Kisanze).
 
Hujui kitu wamanyema wanatokea Kasongo DRC wakati wabwari wanatokea Burundi
Hata wewe pia hujui kitu, siyo tu Kasongo bali Congo nzima hakuna kabila la Wamanyema, bali kuna jimbo linaitwa Maniema, Utambulisho wa jamii ya Wamanyema ni Tanzania pekee, na zaidi zaidi Ujiji tumezoeleka kama Waswahili, majina ya jamii nyingi hutolewa kwa dhana tofauti tofauti ila Wanaanthropolojia huhesabu watu fulani kuwa jamii tengefu kwa utangamano na mfanano wao mf. Wamanyema tuna utambulisho mmoja mkuu ambao ni utamaduni wetu wa kiungwana "Tanganyika-arabian" na kutokeza kama jamii moja, kuhusu utofauti wa asili za baadhi ya makabila hilo lipo kwa jamii karibu zote, mf. Waluguru wana koo km. wabena, wamwenda, wahafigwa na wachuma na zote zina asili tofauti zikakutana uluguru na kutengeneza utambulisho mmoja. Hivyo tofautisha Umanyema wa kikabila na Umanyema wa nasibu anaoweza itwa mtu wa Kasongo kwa vile ni jimboni Maniema, pia fahamu kabla hilo jimbo halijagawiwa mpaka Kivu(walikotokea Wabwari) ilikuwa ni moja na iliitwa yote Kivu-Manyema na jina Manyema ndo la asili siyo Kivu maana makabila karibu yote ya Wamanyema yana chimbuko la eneo lenyewe la Manyema hata kabla ya kusogea Kivu na hatimae Kigoma
 
Mhhhh. Wabwari wanatokea Burundi
Wabwari wenyeji wa Burundi wapo ila kiasili wanatokea Zoni ya Fizi katika Himaya ya kijadi ya nusu kisiwa ya Ubwari, ili jibu lako liwe sahihi inategemea unajibu kwa mtazamo gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…