Vita hiyo waliingiza ushabiki wa dini na siasa, pia tatizo lilianzia October 7 baada ya watu wengi kupongeza mauaji ya jamaa ya kushambulia wananchi, wale wananchi walikuwa na makosa gani? Kama hamas wangekamata wanajeshi wa IDF au wanasiasa wa Israel, lakini wadada na watoto na mabibi! Israel hana cha kupoteza anajua anavyochukiwa na maadui zake hasa nchi za kiarabu, aneshatishiwa kufutwa kwenye ramani ya dunia, anaona akiwachekea hamas yatakuja mengine zaidi ya hayo. USA hana uwezo wa kuzuia Israel ili isishambulie Gaza, kitakachoweza kuzuia na kumaliza vita ni hamas kuachia mateka na kukaa meza moja na viongozi wa Israel ili waangalie namna ya kuishi kwa amani na kwa kuheshimiana. Ujanja wa hamas na shinikizo toka nje haviwezi kumaliza tatizo, madai ya hamas na nchi za kiarabu kuitambua Palestinians na kutojitambua Israel haviwezi kuleta amani hata siku moja, na haiwezi kuirudisha Israel nyuma.