Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2016, na kuingia Ikulu 20/01/2017 baada ya kula kiapo.

Katika kipindi cha uongozi wake, alifanya mengi, yakiwemo yaliyowafurahisha na yaliyowakwaza Wamarekani.

Ingawa alionesha chuki kwa baadhi ya Mataifa, hasa ya Kiafrika, lakini alilifaa sana Taifa lake la Marekani.

Mwaka huu Wamarekani watapiga kura ya kumchagua Rais.

Bila shaka, wengi wanajua kuwa wanamuhitaji sana Trump kuliko wakati mwingine wowote.

Uthubutu wake utawezesha vita vya Urusi na Ukraine kufikia ukomo. Anaweza kusaidia kuleta amani Mashariki ya Kati, japo itakuwa ni kwa muda tu.

Atamdhibiti Rais wa Korea Kaskazini asiwe tishio kwa Marekani na maslahi ya Marekani.

Japo si nabii, lakini naamini Trump atashinda Kiti cha Urais wa Marekani mwaka huu

Hata Wamarekani waliomo humu JF, japo ni wachache, lakini wanalijua hilo.

Hawatafanya kosa. Wameamua kwenda na bilionea Donald Trump.
 
Trump ni msela muoga asiyetimiza ahadi zake sidhani kama anaweza kuaminiwa upya ilihali Yale aliyoyaaahidi katika kampeni zake hakuwahi kutekeleza alipopata madaraka.
 
Zaidi ya kung'ng'ana kujenga ukuta baina yao na Mexico sioni la maana saaana alilolifanya Donald akiwa president wa Marekani. Angewafaa wasingempa muhula mmoja
 
Sanders au mtu mwingine ataingia kama mgombea binafsi na kushinda, kwa kuwa si Biden wala Trump atakaekuwa raisi ajae, wote ni horrible, horrible, horrible!
Wamarekani wanaogopa ujamaa kama ukoma. Wakisikia Sanders wanajua anakuja kuleta mambo ya kijamaa.

Sanders hashindi hata kwa kutumia uchawi

Trump anarudi White House labda wamfunge kwenye makesi yake anayopambana nayo
 
Hata sie wamarekani pori tunamtakia ushindi trump, huyo ndiye rasi wa dunia asicheka na kinyamkera duniani
 
Back
Top Bottom