Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Spika ameongea kitu cha maana sana. watu kama Tito Magoti, Maria Sarungi, Ole Ngurumo na type zake zooote hizo, wanaichafua sana nchi na wanatamani hata Masai mmoja tu afe ili wapate cha kuongea. Wadhibitiwe mapema, sio afya kwa taifa.
Afya kwa taifa ni kufukia uchafu?
 
Hata Magu nae alikua na majibu hayo leo ni chakula cha mchwa na sisimizi 🤧
 
kuna wakati najiuliza hivi kuna watu wamehakikishiwa wataishi milele? au wanavyotudhurumu wataenda navyo? binafsi sielewi! naamini sana katika kutafuta kwa jasho na njia halali nasikitika sana watu wanaotakiwa kutusaidia na kutufusha ndio wanaotuuza!

Kibaya zaidi sisi tunaohitaji huo msaada tumekubali kudhalilika na kuwakumbatia huku tukipewa makombo kidogo na kulidhika yaani toweze kumudu leo tu! kama mikopo ya bodaboda, mama lishe, na vimiradi vidogovidogo ambavyo hatuwezi kutoboa mhn!

Ukitaka kuingia uchungu jaribu kuvaa uhusika wa Mbwa wako unayemtupia chakula baada ya wewe kula (achana na mbwa wao wanaokula vizuri kuzidi sisi) akiwa kwenye banda huku akiwa na mnyororo!
ndivyo tunavyofanywa pia.

MWENYEZI MUNGU atuhurumie kwa kuwa wavumilivu tusiovumilika na kila siku tutaishia malalamiko!
shame upon us! Hata wanamziki na wasanii ambao wangeweza kutuhamasisha kwa nyimbo za kujikomboa kiuchumi na fikra sasa wanatuimbia nyimbo za maombolezo kabla ya kwenda kaburini kwa kuwa wote wanahubiri ngono hakuna tena anayezungumzia ukimwi unaua na badala yake wengine wamekuwa wahamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja na jamii iko kimya ikiwaangalia.

Viongozi wetu wa dini wameondoka kwenye misingi yao ya kujenga mioyo ya tumaini kwa waumini na wememezwa na sadaka na ibada za mazingaobwe!

Walio kwenye haki hawawezi kutoa tena haki na wakati mwingine si kwamatakwa yao bali mazingira yanawalazimisha!
Mkuu hii comment ni uzi tosha!! Ifungulie uzi wake
 
Hata mimi nasimama na Wamasai, sio kwa ufisadi ule wa kuuziana vitalu, sijajua mkubwa gani ana 'interest' hapo?!, anyway sijajua kwa undani hili saga limeanzaje...
Ukitaka kujua walioko nyuma anza kutrack vitalu vya huko vilianza kumegwa wakati wa awamu ya nani kiutawala utapata majibu yote
 
Leo Bungeni baada ya Waziri mkuu kuongelea video inayosambaa kwamba kuna mapigano yameanza Ngorongoro, Spika Tulia Ackson ametoa maoni yake na kutaka mhusika ashughulikiwe na taasisi zilizosajiliwa nchini zifate.

======

Spika: Tupo kwenye vita ya kiuchumi na nchi zingine, tukiwaacha hawa wakaendelea kutumika, wale waliopo hapa nchini sheria zetu zichukue mkondo wake.

Kama mtu anafanya upotoshaji kama huyo ambae amechukua hiyo clip na inajulikana ameichukulia wapi, tunaweza kuanza na huyo halafu wengine watafata ikiwa ni pamoja na hizi taasisi ambazo zimesajiliwa hapa nchini kwetu tukifikiri kwamba zina lengo jema na sisi hapa nchini lakini kama zinafanya jambo tofauti pia sheria zichukue mkondo wake.

Huyu Spika ni mjinga kweli? Ishu picha ni halali au siyo halali? Wamasai wanauawa au hawauawi? Jinga kweli, lina mawazo ya Ndugai na Magufuli kwa sababu ni zao la hao majangili
 
Viongozi wetu na "vita ya uchumi" wanatuona sisi mafala sana.
 
Back
Top Bottom