Wamasai wa Ngorongoro wanaopelekwa Handeni hawataweza ku-survive pale

Wamasai wa Ngorongoro wanaopelekwa Handeni hawataweza ku-survive pale

NI AJABU sana kama watz bado tunawaza kwa ufinyu kiasi hicho basi kama ndivyo vijana hamuwezi kufika popote.bado karne hii mtu unawaza kubebwa na mabeberu na hifadhi.handeni maji siyo shida na serikali siyo wajinga kuwapeleka watu sehemu ambazo hazina huduma.shida yetu watz siku zote tunafikiria negativity but we don't think positively.kwamba halimi na walikuwa wanapewa missada,sasa watafundishwa kulima pia kujitegemea.taifa la watu ombaomba siyo taifa imara.watu wajifunze kufanya kazi kwa bidii after all binadamu anaweza kuishi katika mazingira yote kwa kadiri Mungu alivyotuumba kwamba tutaishi kwa jasho pia kuyatawala mazingira yanayotuzunguka.

Ndo maana wanadeka kisa walikuwa wanapewa chakula,wamewadekeza sana hao watu
 
Iyo mifugo wanamfugia nani had wasiweze kujitegemea chakula huko walikopelekwa? Au izo ng'ombe zao ni mapambo haziwezi kuwafanya wajitegemee?

Wafugaji wote nchi hii wanalishwa na serikali?
 
Hao ni wazaliwa wa hapo na wapo hapo Handeni kwa ridhaa yao hawakufukuzwa popote, hata wewe sasa hivi ukoo wako wote mkihamishiwa (kwa nguvu) Mkoa mwingine msioujua watu msiowajua muanze moja, utaona ni sawa ? Ni haki hiyo ? Hata Samia mwenyewe hawezi kufurahia ukoo wake wote ukihamishwa kwa nguvu ktk labda Makunduchi na kupelekwa Hai au Marangu, Singida au unafikiri watakubali ?
Wanapinga tu lkn changamoto sana ,mtumishi tu ambae anatoka eneo moja kwenda lingine tena kwa kaz ile ile lkn kunakua na changamoto ya mazngira au maisha na inamchukua muda mpaka kuzoea ,kuliko hawa ambao ndio chimbuko lao
 
Ni uonevu na unyama wa hali ya juu, fikiria mtu aje akuamishe wewe na familia yako na ukoo wako wote kukupeleka sehemu ambayo hauijui wala haujawahi kufika na utamaduni na maisha ya watu hauyajui achilia mbali livelihood yako.

Lakini mtu anatembea na Kamera Misikitini na kuhiji kuomba Allah, sijui hata wanaomba nini?
Wakenya na mabwanyenye wenu haliowapenyeza nchini kwetu hamna chenu tena kule Ngorongoro. Cha kufanya ni ku deal na serikali yenu iwape sehem salama za kulishia mifugo yenu. Tulio wengi tunapinga Tanzania kuendelea kufanywa shamba la bibi. Tanzania ni moja, popote watapopelekwa ndani ya Tanzania hii ni kwao. Wakimbizi wangapi wameacha majumba yao, ardhi zao, mazao yao na wengine familia zao, wamevuka boda kutoka katika nchi zao kuja Tanzania kutafuta hifadhi makambini na wanaishi vizuri tu. Ije kuwa tatizo kwa mtanzania anaetolewa sehem moja ya Tanzania, na kupelekwa sehem nyingine ya Tanzania! Hapa hapa Tanzania ni watanzania wangapi wamevunjiwa nyumba zao katika mikoa mbali mbali, sana sana Dar es salaam ili kupisha miradi ya serikali kama vile barabara nk. Je mliandika chochote kuwatetea? Serikali iendelee na oparation zake na ikitokea kusita sita kokote wananchi tuliochoka nchi yetu kufanywa shamba la bibi tutaandamana ili oparation hiyo iendelee.
 
Huu ni upuuzi mtupu, unapigia debe waendelee kulishwa bure?
Waacheni nao wapambane kama wanyaturu wengine.
Walichokuwa wanalishwa nacho ni pesa za serikali ambazo zingefanya kazi zingine.
Sio kulishwa bure, kule Ngorongoro wanategemea mifugo, Handeni hakuna maeneo ya kuchunga, pia wanauza Shanga
 
Tembelea handeni, handeni fursa ni nyingi sana,fanya utembelee Handeni.Handeni kuna watu wenye asili za nchi za mbali wengi sana,na wenyeji ni wengi sana,kabila la wazigua,ni kabila ambalo huwezi kuwakuta ni wahangaikaji,kwenda wilaya tofauti na yao,kwenda mikoa tofauti na mkoa wao.Jiulize kwa nini kabila la wilaya hiyo,huwezi kuwakuta mikoa mingine,ni kutokana na fursa nyingi zilizopo kwenye wilaya yao,na ni wilaya kubwa sana kati ya wilaya za Tanga,ni wilaya yenye madini tofauti tofauti.
Hahaaa zipi hizo?
 
Kwenye Hifadhi za Taifa, ukiachana na Zoo, huwa kuna vibao vimeandikwa Dont feed birds or animal. Kwamba usiwalishe ndege na wanyama wengine na ni kosa kubwa sana ndani ya hifadhi kuwatupia hata nyani ndizi.

Hii ni suala la kisayansi zaidi na sio suala la kiusalama kwamba unaweza kuwalisha sumu hapana.

Utakapo walisha ndege na wanyama kule Hifadhini watafikia sehemu watakuwa hatawaweza kujitafutia chakula chao na watakuwa wakitegemea kulishwa.

Sasa basi kule Ngorongoro kwa kipindi kirefu sana Wananchi hasa wa tarafa ya Ngorongoro walikuwa wakiletewa chakula na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hii ni kwa sababu hakuna kulima hivyo Mamlaka ilibeba jukumu la kuwalisha. Ukiachana na Chakula walikuwa wanasambaziwa maji na Gari za Mamlaka, wale wamasai walikuwa wanapewa misaada chungu nzima na Wazungu hasa watalii.

Kwa kifupi wale Wamasai walikuwa wanaishi kwa misaada ya Mamlaka na Wazungu na pia watalii nao waliwapa sana sapoti.

Kuwapeleka Handeni waanze kujitegemea na either waanze kulima ni kuwaumiza hawa watu, hawataweza survive kule kamqwe, Kuna wajinga wanaona zile nyumba za tofali kama ndo msaada mkubwa sana kwao

Wamasai hawana shida na nyumba za kisasa na shida kubwa ni mazingira.

Kule Handeni hawataweza ku move free kama Ngorongoro, kule Handeni itabidi sana walime badala ya kufuga make eneo halitatosha kufuga. Kule Handeni hakutakuwa tena na free service kama za maji na Chakula na pia biashara yao ya kuuza shanga kwa watalii haitakuwepo kule.

Wamasai ni wafugaji na sio wakulima, Handeni imejaaa hakuna maeneo ya kufuga sasa hawa wana forciwa wabadilike kutoka kufuga na kuwa wakulima jambo ambalo ni gumu sana kwao. Wamasai wa Monduli au Simanjiro wanaweza Survive vyema Handeni ila sio hawa wa Ngorongoro.
ugomvi woote ule ni kwamba, wale masai wengi ni wakenya, na kingine wameishi kwa kuuza shanga na vinyago vyao kwa pesa nyingi kwa wazungu. kule wanapelekwa hakuna mbuga, hawataona mzungu hata mmoja. na masai huwezi kumtenganish an amzungu kwasababu fahari yake huwa anapenda mzungu amuone ili amshangae. hapo anajisikia rahaaa.
 
Pumba tupu umeandika. Wamasai wa Ngorongoro wamedekezwa mno. Na hao wanaharakati wanaowatetea ni kwamba wanaumia harakati zao kufikia tamati kwasababu walikuwa wanaingiza pesa nyingi toka kwa mabeberu kwa kujifanya watetezi wa masai. Kinachonikera ni masai kutaka wawe na maamuzi pale NCAA. Yaani jitu halina elimu yoyote na lenyewe liwe sehemu ya vikao na maamuzi muhimu ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
 
Kwa uzoefu mdogo sana nlionao kuhusu NCAA kunauwezekano mkubwa uhamisho huu ukaathiri idadi ya visitors. Wamaasai ni mojawapo ya kivutio ngorongoro
NB: hawakuwa wanapewa huduma bila sababu waliinufaisha gvnt.
 
Huu ni upuuzi mtupu, unapigia
debe waendelee kulishwa bure? Waacheni nao wapambane kama wanyaturu wengine.
Walichokuwa wanalishwa
nacho ni pesa za serikali
ambazo zingefanya kazi
zingine.
Tuache roho mbaya au ubaguzi, wastaafu wanapewa zawadi za magari na kujengewa nyumba za kifahari kwani hizo pesa hazina sehemu zengine zenye uhitaji?
 
Kwa uzoefu mdogo sana nlionao kuhusu NCAA kunauwezekano mkubwa uhamisho huu ukaathiri idadi ya visitors. Wamaasai ni mojawapo ya kivutio ngorongoro
NB: hawakuwa wanapewa huduma bila sababu waliinufaisha gvnt.

Nilikuwa nangojea mtu aliseme hili - Wamasai wa Ngorongoro pia ni kivutio kwa watalii.
Naweka stress: Wamasai wa Ngorongoro.
 
NI AJABU sana kama watz bado
tunawaza kwa ufinyu kiasi hicho basi kama ndivyo vijana
hamuwezi kufika popote.bado
karne hii mtu unawaza
kubebwa na mabeberu na
hifadhi.handeni maji siyo shida
na serikali siyo wajinga
kuwapeleka watu sehemu
ambazo hazina huduma.shida
yetu watz siku zote tunafikiria
negativity but we don't think
positively.kwamba halimi na
walikuwa wanapewa
missada,sasa watafundishwa
kulima pia kujitegemea.taifa la
watu ombaomba siyo taifa
imara.watu wajifunze kufanya
kazi kwa bidii after all
binadamu anaweza kuishi
katika mazingira yote kwa
kadiri Mungu alivyotuumba
kwamba tutaishi kwa jasho pia
kuyatawala mazingira
yanayotuzunguka.
Hao wanasiasa tu ambao ndio viongozi wetu hawawezi kuishi nje ya system kujiajiri hawawezi.
 
Wa masai ni pastoralists na ufugaji wao ni kupitia uchungaji. Hapa ndio wadau wanatakiwa kua makini sana vinginevyo majanga yatatuhusu. Sidhani kama eka 3 zinatosha. Na viongozi wengi wa nadhani wanalielewa hili lakini ukweli ni tofauti. Itabidi kuwe na monitoring ya karibu sana.
 
Mnatetea Watu kuendelea kulishwa na kuveshwa!
Wakapambane na Maisha huko Handeni,

Kazi Iendelee hakuna kulala.
 
Nilikuwa nangojea mtu aliseme hili - Wamasai wa Ngorongoro pia ni kivutio kwa watalii.
Naweka stress: Wamasai wa Ngorongoro.
Baniani mbaya kiatu chake dawa. Wanahamishwa lakini wanahitajika pia; nahisi ndiomaana wakafanya kuwa hiari.
 
Back
Top Bottom