The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Baada ya kuwasikiliza wakazi na viongozi hawa wa tarafa ya Ngorongoro, nimegundua yafuatayo:
1. Kuna agenda mbaya ya siri dhidi ya Wamasai hawa wa Ngorongoro inayofanywa na serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Wanaiuza ardhi ya Ngorongoro kwa waarabu?
2. Kumbe wakazi wa Ngorongoro wala hawahami kwa hiari isipokuwa kinachofanyika ni "forced eviction". Inashangaza sana tendo hili kufanywa na serikali hii kana kwamba tunatawaliwa na serikali ya kikoloni!
3. Kati ya wakazi wa Ngorongoro 100,000+, inasemekana ni wakazi wasiozidi 7,500 pekee ndio walishahamia huko Msomera - Handeni - Tanga kwa kulazimishwa na ushawishi wa vipesa kidogo. Lakini propaganda za CCM na serikali yao wanadai wamehama wenyewe kwa hiari!
4. Hitimisho la unyama, unyanyasaji huu ni serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na CCM kuwanyima wakazi wa Ngorongoro zaidi ya 100,000 haki yao ya kupiga kura mwaka huu 2024 (serikali za mitaa) na 2025 (uchaguzi mkuu wa madiwani, Wabunge na Rais) kwa kuondoa vituo vyote vya uandikishaji wapiga kura na kupigia kura.
Wanauliza Rais Samia Suluhu Hassan, serikali na CCM wawaambie wao ni raia wa nchi gani Ili waende huko maana kuna wakati walisema Wamasai kwao ni Sudan.🤔🤔
5. Lakini cha ajabu na kwa namna serikali hii inavyojichanganya yenyewe, inadai kuwa hakuna wakazi Ngorongoro, walishahamia Msomera - Handeni - Tanga (zaidi ya 540km toka Ngorongoro).
Lakini cha ajabu ni kuwa, maafisa wa kodi na ushuru wa serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na CCM, kila siku ni kiguu na njia ktk maeneo mbalimbali ya Ngorongoro kudai Kodi na ushuru kwa Wamasai hawahawa wanaodaiwa walishahamia Tanga, Msomera Handeni!
6. Jambo jingine la kusikitisha kabisa ni kuwa, serikali inakusanya kodi kwa watu hawa lakini ime - suspend kutoa au kuboresha huduma zote za kijamii kama afya, elimu, barabara, umeme, mawasiliano nk kwa watu hawa.
Hii ni homicide inayofanywa na serikali dhidi ya raia wake. Hii ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu usiopaswa kuvumiliwa hata kidogo na dunia!
Rais Samia Suluhu Hassan na CCM, hii sio sawa hata kidogo.
Mungu hapendi na hataki matendo haya asilani. Acheni mara moja vinginevyo hukumu ya Mungu iliyo mbaya kabisa iko juu yenu.
Rais Samia Suluhu Hassan hebu atoke aseme ana ajenda gani dhidi ya Wamasai na Watanganyika kwa ujumla? Ni maendeleo gani ya kunyanyasa na kutweza utu wa watu? Kama haya ndiyo maendeleobyanayoletwa kwa njia hii ya kishetani, hatuyataki na vyema akayapeleka Zanzibar kwao!!
HII HAIKUBALIKI HATA KIDOGO!!!
Pia soma: Kuelekea 2025 - Njama: Vituo vyote vya kupigia kura Jimbo la Ngorongoro vimefutwa, ila watu bado wapo na Jimbo bado lipo