Wamasai wameweza. Umoja waliouonyeshea ndîo Ushindi wenyewe

Ndio maana Nyerere kwenye baraza Lake la mawaziri alikua anajitahidi mno kubalance.

Ila sasa ni kama serikali ni ya watu wa pwani tu.
 
Kwema Wakuu!

Sitaki kujua Nani yupo Sahihi na Nani hayupo Sahihi.
Nafuatilia wanachofanya Wamasai Huko Ngorongoro.

Nimevutiwa na umoja waô, hii inamaanisha soon watakuwa na Ñguvu.

Nakumbuka Mwezi wa nne mwaka huu nilikiwa naenda kumzika Bibi yàngu mzaa Mama, ndàni ya Basi Siti ya Kulia kwetu walikuwepo Masai wakike na wakiume àmbao ni Mume na Mke wakiwa ni Watu wazima.

Nami nilikuwa na familia yàngu, yàani Mke na Mtoto.
Yule Mwanamke WA kimasai alikuwa mchangamfu kweli, tukawa tunapiga stori na Mumewe naye akawa mchangiaji.

Walisema Wanatoka Zanzibar, nikawa namtania ninyi ndîo wale mliowachapa viboko wazenj kule ufukweni ndîo mnakimbilia kwèñu. Basi tukawa tunacheka safari ikiendelea.

Baadaye wakasema waô wanaenda Nyumbani Ngorongoro,na Hapo ñdipo nikavutiwa na tàarifa hiyo.
Nikamwambia lakini Huko Ngorongoro si Watu walishaondolewa na wakahamishwa Msomera. Akaniambia waliohama NI kidôgo ila wengi wamebaki.

Nikataka kujua maonî yake kuhusu sakata la waô kuhama kuona kama anakubaliana nalo au Laa.
Tayari alikuwa na hofu, alihisi labda Mimi ni mserikali lakini Kwa uchangamfu na Stori za kuingiziaingizia aliamua kufunguka.

Wao wameona warudi nyumbani(Ngorongoro) ili kutia Ñguvu katika kuhakikisha wanabaki katika ardhi ya Ngorongoro.

Nikamwambia lakini mnaweza ishi popote ndàni ya nchi hii. Yôte NI nchi yetu. Akanijibu kuwa nchi yôte NI Moja ila Kwa Wamasai ni Ngorongoro, na maeneo mengine yanayozunguka Arusha na Manyara.

nikamuuliza vipi kama mkishindwa, akasema hawawezi kushindwa lakini yôte Mungu ndiye anajua.

Tukafika Korogwe, wakapanda Wamasai Wengine wanne wôte wakiwa Wanaume. Hawakupata Siti hivyo walikuwa wamesimama wakiwa wamekuja Karibu nasi kwani walimuona Masai wenzao tuliokuwa tumetoka nao Dsm.
Wakawa wanaongea kimasai Hapo.

Kisha tukafika Mombo, nikamuuliza Yule Masai Mwanaume mwenye Mke. Hawa nao wanaenda Ngorongoro, akawatazama Kisha nao wakanitazama, akatabasamu kirafiki, Kisha akajibu Ndio.

Sikutaka kuuliza uliza tenà. Nikashuka zangu Makanya kwetu. Wao wakaendelea na safari ya Arusha, Kwao Ngorongoro.

Nilipoona haya maandamano ndîo nikakumbuka Ile familia ya Wamasai.
Huu umoja wanaouonyesha Wamasai siô rahisi kupatikana katika jamii ya Sisi wabantu.
Yàani Mtu atoke Zanzibar kisa Kwao Ngorongoro ilhali walishapewa option ya kuhamia sehemu ñyiñgine àmbayo waô wanasema siô Ardhi Yao ya Asili.

Kingine nilichojifunza nikuwa, kwèñye nchi yetu yapo Makabila au wàpo Watu àmbao bado hawaamini katika utanzania au utanganyika ndîo maana neno Ardhi ya Asili linatumika kumaanisha nchi ya Wamasai, au nchi ya kabîlà Fulani.

Tunapaswa tuliangalie hili Kwa jicho la mwewe hasa Kwa Miaka ijayo kwani tusipokuwa Makini nchi hii inaweza kupasuka Kwa kile kiitwacho Ardhi ya Asili yàani kabîlà Fulani linaweza kusema tunajiengua Kutoka katika nchi Yenu. Ndîo maana halisi ya ardhi ya Asili.

Wanaosema Ardhi ya Asili humaanisha hii nchi yetu siô Ardhi ya Asili Kwa kîla Mtu. Kwamba Mimi Taikon àmbaye NI mtu WA Makanya, siwezi kuwa na Haki Sawa na wanarungwe nikifika Rungwe.

Siô ajabu, Yapo malalamiko Kwa Baadhi ya Watu hasa watanganyika wakifika Zanzibar kujiona wàpo nchi ñyiñgine Kabisa.
Kumaanisha nini?
Kwamba nchi yetu Ipo kimtegomtego? Au Sisi siô Taífa Moja? Ila tunajifanya tu wamoja?

Sakata la Ngorongoro ni Moja ya vielelezo vinavyothibitisha kuwa nchi yetu inanyufanyufa ndogondogo Ambazo kama hazitazibwa mapema inaweza kuleta athari Hapo baadaye.

Mfano Mwingine, ni suala la Kiongozi yeyote akiwa Rais WA hii nchi utasikia, anapendelea Kwao, lakini hiyo kwao NI sehemu ya nchi hii. Au huyu mnzanzibar anauza Mali za Tanganyika. Au Zanzibar utasikia ooh! Watanganyika wametutawala.

Kumaanisha bado zîpo nyufa za Ukabila na actually siô Ukabila isipokuwa hicho kinachoitwa Ukabila kileletwa na wazungu.
Wazungu hawakukuta Makabila walipokuja Hapa Afrika mashariki isipokuwa walikuta vitaifa vidogovidogo àmbavyo baadaye walivisimika jina la Kabîlà. Lakini ukweli ni kuwa kulikuwa na nchi ya Wasukuma, wahaya, wahehe, nyamwezi, Wapare, wachagga na nchi zingine Ambazo Leo hii huitwa Makabila.

Siô ajabu, ukisikia Mtu akisema Ardhi yake ya Asili akirejelea nchi Yao. Kama usikiavyo Kwa hao Wamasai.

Kama hiyo haitoshi, kûna utaratibu Mwingine wa Mtu akifa labda Dar es salaam anasafirishwa kwenda Ardhi Yao ya Asili Kwa gharama yoyote. Hii wanayowatani zetu Wachagga na baadhi ya jamii katika nchi yetu.

Mantiki ya Jambo Hilo Watu wengi hawaijui na taikon Leo nitawajuza.
Kikawaida Mtu hawezi kuzikwa nchi ya ugenini. Hiyo tuliiona ikifanyika tangu Zamani. Tumesoma kwèñye vitabu vya Dini tukaona hata Wayahudi wanamila za namna hiyo.

Kwamba mchagga kuzikwa Mbeya Huona yupo nchi ya ugenini na sio nchi Yao.

Wito, uundwe mpàngo mpya wa kuzifanya Akili za kizazi kipya kijue na kuelewa nchi yôte ya Tanganyika ni Ardhi ya Asili yàani popote ulipo na ûkienda kwèñye nchi hii Mtu ajue ni Kwao.

Iwekwe Sheria kuwa Pasiwe na Makaburi ya Ukoo siô kabîlà sijui kurudishwa kwèñye Ardhi ya Asili.
Mtu azikwe Mahali alipokuwa anaishi na kufanya Kazi
Mfano Mtu kama yupo Dar na ameishi Dar Kwa Muda mrefu, huyo azikwe Dar.
Hii itaondoa Ile dhana ya Ardhi ya Asili na kîla Mtu ataona nchi hii kote ni Kwao.

Lakini mambo yakiendelea hivi, kuishi Kwa kutegeana kama kwamba Watu wanaviziana au wanajua Ipo Siku mambo yataharibika na tutagawana mbao. Jambo ambalo siô Sahihi.

Mimi Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Umenikumbusha sakata la DPWORLD
 
Nyinyi Baada ya miaka 50 ikiwa ngorongoro imemezwa na Watu na wanyama kutoweka ntakuja kuilaumu serikali Kwann haijuchukua hatua mapema,Tatizo kila kitu mnakiwekea sasa,wanasiasa Akili hawana wanawaza madaraka ya Leo Yao Tu,kesho yenu hawaihitaji,Haya Masai wamerudishiwa vijiji NI IPI AJENDA YA UPINZANI SASA?manake hawana AJENDA maalum wanasubiria matukiol ndo uone tweets zako au Instagram posts,
 
Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba umma haujawahi kushindwa kitu chochote kile pale wanapoamua jambo lao kwa dhati kabisa ya mioyo yao.
Get informed.
Uko sahihi kabisa, mageuzi yote yaliyotokea kuanzia Africa Kaskazini Tunisia, Algeria,Misri na Sudan watawala walitumia majeshi kudhibiti umma lakini kadiri ummma ulivyokuwa na msimamo wanajeshi wenyewe walisalimu amri na kuwaambia watawala kuwa hawawezi wakaua wananchi ili kulinda wao kubaki madarakani. Umoja ni silaha kubwa sana, imagine umati ule wa jana wa Wamasai ni generali gani atapeleka kifaru pale. Wamasai wa Ngorongoro wametoa somo kubwa sana.
 
Nyinyi Baada ya miaka 50 ikiwa ngorongoro imemezwa na Watu na wanyama kutoweka ntakuja kuilaumu serikali Kwann haijuchukua hatua mapema,Tatizo kila kitu mnakiwekea sasa,wanasiasa Akili hawana wanawaza madaraka ya Leo Yao Tu,kesho yenu hawaihitaji,Haya Masai wamerudishiwa vijiji NI IPI AJENDA YA UPINZANI SASA?manake hawana AJENDA maalum wanasubiria matukiol ndo uone tweets zako au Instagram posts,
Eneo linalobishaniwa unalifahamu au unaaandika tu kwa dhana kuwa wapinzani walikuwa nyuma ya hili sakata? Rudisheni tu hela ya mwarabu kimya kimya.
 
Nyinyi Baada ya miaka 50 ikiwa ngorongoro imemezwa na Watu na wanyama kutoweka ntakuja kuilaumu serikali Kwann haijuchukua hatua mapema,Tatizo kila kitu mnakiwekea sasa,wanasiasa Akili hawana wanawaza madaraka ya Leo Yao Tu,kesho yenu hawaihitaji,Haya Masai wamerudishiwa vijiji NI IPI AJENDA YA UPINZANI SASA?manake hawana AJENDA maalum wanasubiria matukiol ndo uone tweets zako au Instagram posts,

Kwa hîyo uelewa wako umeishia kujua Mimi NI mpinzani?

Hongera sana Mkuu
 
Wataondoka, tena kwa hiyari yao,
Wataondoka mtake msitake

Kwa umoja waô siô rahisi hivyo hata watañzania wôte tuamue kuwaondoa hatutaweza.

Hapo labda Mbinu za Akili Sana..

Wachorewe Mipaka kuwatenganisha na mbuga. Kama hifadhi Ipo Mashariki basi Makazi Yao yaelekee magharibi,
 
Watu weñye umoja ni hatari Sana.

..watu wenye umoja ni hatari kwa nani?

..tangu lini umoja umekuwa jambo baya, na la hatari?

..tatizo la serikali ni kutowaelimisha na kutowashirikisha Wamaasai kuhusu zoezi la kuwahamisha kwenda maeneo mengine.

..pia serikali ilishapoteza imani ya Wamaasai siku nyingi kutokana na unyanyasaji ambao imeikuwa ikiwafanyia tangu miaka ya 90 Muarabu alipopewa Loliondo.

..Kwasababu Wamaasai wana uchungu, na wana muamko kuhusu ardhi yao, serikali ingewaelimisha kuhusu faida ya baadhi ya Wamaasai kuhamia maeneo mengine, isingekuwa sio jambo gumu.
 
Ngorongoro ni Ardhi ya watañzania siô Wamasai pekee.

Elimu Wapewe kuwa Hakuna Mtanzania anayemiliki Ardhi isipokuwa serikali ndîo Mmiliki wa Ardhi.
 
..sio kweli kwamba Watanzania ni LANDLESS.

..Pia sheria ya kuanzisha hifadhi ya Ngorongoro inatambua uwepo wa Wamaasai hapo. Na sheria hiyo ipo tangu wakati Tanganyika haijapata Uhuru.

..Lakini tusiende huko kwenye historia na sheria. Tuliangazie suala la Ngorongoro ktk mazingira ya sasa.

..Tayari kuna Wamaasai waliohama Ngorongoro kwa hiyari yao ikiwemo hao uliokutana nao wakitokea Zanzibar.

..Sasa kama hali iko hivyo kwanini serikali imeshindwa kufanya zoezi la kupunguza idadi ya watu Ngorongoro kuwa SHIRIKISHI?

..Mimi nadhani kuna tatizo Sugu sana na CCM na serikali kujiona wako juu ya wananchi.

..Wananchi wa Tanzania hawana thamani mbele ya viongozi wa nchi hii, ndio maana matumizi ya nguvu za vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni mengi.
 
Back
Top Bottom