Wamasai wameweza. Umoja waliouonyeshea ndîo Ushindi wenyewe

Ndio maana Nyerere kwenye baraza Lake la mawaziri alikua anajitahidi mno kubalance.

Ila sasa ni kama serikali ni ya watu wa pwani tu.
 
Umenikumbusha sakata la DPWORLD
 
Nyinyi Baada ya miaka 50 ikiwa ngorongoro imemezwa na Watu na wanyama kutoweka ntakuja kuilaumu serikali Kwann haijuchukua hatua mapema,Tatizo kila kitu mnakiwekea sasa,wanasiasa Akili hawana wanawaza madaraka ya Leo Yao Tu,kesho yenu hawaihitaji,Haya Masai wamerudishiwa vijiji NI IPI AJENDA YA UPINZANI SASA?manake hawana AJENDA maalum wanasubiria matukiol ndo uone tweets zako au Instagram posts,
 
Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba umma haujawahi kushindwa kitu chochote kile pale wanapoamua jambo lao kwa dhati kabisa ya mioyo yao.
Get informed.
Uko sahihi kabisa, mageuzi yote yaliyotokea kuanzia Africa Kaskazini Tunisia, Algeria,Misri na Sudan watawala walitumia majeshi kudhibiti umma lakini kadiri ummma ulivyokuwa na msimamo wanajeshi wenyewe walisalimu amri na kuwaambia watawala kuwa hawawezi wakaua wananchi ili kulinda wao kubaki madarakani. Umoja ni silaha kubwa sana, imagine umati ule wa jana wa Wamasai ni generali gani atapeleka kifaru pale. Wamasai wa Ngorongoro wametoa somo kubwa sana.
 
Eneo linalobishaniwa unalifahamu au unaaandika tu kwa dhana kuwa wapinzani walikuwa nyuma ya hili sakata? Rudisheni tu hela ya mwarabu kimya kimya.
 

Kwa hîyo uelewa wako umeishia kujua Mimi NI mpinzani?

Hongera sana Mkuu
 
Wataondoka, tena kwa hiyari yao,
Wataondoka mtake msitake

Kwa umoja waô siô rahisi hivyo hata watañzania wôte tuamue kuwaondoa hatutaweza.

Hapo labda Mbinu za Akili Sana..

Wachorewe Mipaka kuwatenganisha na mbuga. Kama hifadhi Ipo Mashariki basi Makazi Yao yaelekee magharibi,
 
Watu weñye umoja ni hatari Sana.

..watu wenye umoja ni hatari kwa nani?

..tangu lini umoja umekuwa jambo baya, na la hatari?

..tatizo la serikali ni kutowaelimisha na kutowashirikisha Wamaasai kuhusu zoezi la kuwahamisha kwenda maeneo mengine.

..pia serikali ilishapoteza imani ya Wamaasai siku nyingi kutokana na unyanyasaji ambao imeikuwa ikiwafanyia tangu miaka ya 90 Muarabu alipopewa Loliondo.

..Kwasababu Wamaasai wana uchungu, na wana muamko kuhusu ardhi yao, serikali ingewaelimisha kuhusu faida ya baadhi ya Wamaasai kuhamia maeneo mengine, isingekuwa sio jambo gumu.
 

Ngorongoro ni Ardhi ya watañzania siô Wamasai pekee.

Elimu Wapewe kuwa Hakuna Mtanzania anayemiliki Ardhi isipokuwa serikali ndîo Mmiliki wa Ardhi.
 
Ngorongoro ni Ardhi ya watañzania siô Wamasai pekee.

Elimu Wapewe kuwa Hakuna Mtanzania anayemiliki Ardhi isipokuwa serikali ndîo Mmiliki wa Ardhi.

..sio kweli kwamba Watanzania ni LANDLESS.

..Pia sheria ya kuanzisha hifadhi ya Ngorongoro inatambua uwepo wa Wamaasai hapo. Na sheria hiyo ipo tangu wakati Tanganyika haijapata Uhuru.

..Lakini tusiende huko kwenye historia na sheria. Tuliangazie suala la Ngorongoro ktk mazingira ya sasa.

..Tayari kuna Wamaasai waliohama Ngorongoro kwa hiyari yao ikiwemo hao uliokutana nao wakitokea Zanzibar.

..Sasa kama hali iko hivyo kwanini serikali imeshindwa kufanya zoezi la kupunguza idadi ya watu Ngorongoro kuwa SHIRIKISHI?

..Mimi nadhani kuna tatizo Sugu sana na CCM na serikali kujiona wako juu ya wananchi.

..Wananchi wa Tanzania hawana thamani mbele ya viongozi wa nchi hii, ndio maana matumizi ya nguvu za vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…