Ramesses II
JF-Expert Member
- Sep 29, 2013
- 3,710
- 5,054
Ni kweli neno Ngorongoro ni la asili ya Kimaasai (Korongoro). Lakini jina siyo uthibitisho wa historia kwamba fulani ndo mkazi wa asili wa eneo husika. Hata Misri mkazi wa asili siyo Muarabu. Hujui enzi za zama za kale na zama za kati Tanganyika ikiitwa AZANIA?Asili Tu ya neno ngorongoro ni hao hao wamasai, hivyo hadithi yako ni ya urongo.
Ngorongoro is believed to be an onomatopoeic word termed by the Maasai people of the region to describe the sound of the bell that hangs around the neck of the lead cow in a herd. The bell makes an echoing “ngor ngor” sound, which made the local pastoralists name the area Ngorongoro.
Lakini ukweli unabaki Watu wa kwanza wahamiaji kuingia eneo la Ngorongoro ya Leo ni Wairaqw, wakifuatiwa na Wabarbaig. wabarbaig hawakukaa muda mrefu kutokana na vita baina yao na wairaqw. Then, wakafuta Wamaasai na kufanikiwa kuwatimua Wairaqw.
Lakini katika ulimwengu wa leo aliye katika eneo husika ndo mwenye eneo maana Tanzania hii karibu kila kabila ni wahamiaji kama ambavyo leo huwezi kuwaambia wangoni Songea siyo kwao ingawa dunia inajua kabisa Wangoni ni Wahamiaji ten awa miaka tu ya karibuni katika karne ya 17 na 18.