Wambulu na Wadatooga ndio wakazi wa mwanzo wa Ngororongo. Kadhia ya Ngorongoro haihitaji hisia

Wambulu na Wadatooga ndio wakazi wa mwanzo wa Ngororongo. Kadhia ya Ngorongoro haihitaji hisia

Asili Tu ya neno ngorongoro ni hao hao wamasai, hivyo hadithi yako ni ya urongo.

Ngorongoro is believed to be an onomatopoeic word termed by the Maasai people of the region to describe the sound of the bell that hangs around the neck of the lead cow in a herd. The bell makes an echoing “ngor ngor” sound, which made the local pastoralists name the area Ngorongoro.
Ni kweli neno Ngorongoro ni la asili ya Kimaasai (Korongoro). Lakini jina siyo uthibitisho wa historia kwamba fulani ndo mkazi wa asili wa eneo husika. Hata Misri mkazi wa asili siyo Muarabu. Hujui enzi za zama za kale na zama za kati Tanganyika ikiitwa AZANIA?

Lakini ukweli unabaki Watu wa kwanza wahamiaji kuingia eneo la Ngorongoro ya Leo ni Wairaqw, wakifuatiwa na Wabarbaig. wabarbaig hawakukaa muda mrefu kutokana na vita baina yao na wairaqw. Then, wakafuta Wamaasai na kufanikiwa kuwatimua Wairaqw.

Lakini katika ulimwengu wa leo aliye katika eneo husika ndo mwenye eneo maana Tanzania hii karibu kila kabila ni wahamiaji kama ambavyo leo huwezi kuwaambia wangoni Songea siyo kwao ingawa dunia inajua kabisa Wangoni ni Wahamiaji ten awa miaka tu ya karibuni katika karne ya 17 na 18.
 
Mbulu toka lini akakaa na wanyama, labda nguruwe lakini sio Simba au tembo
Kwani enzi hizo na Ngorongoro ilikuwa hifadhi? au pori tu na eneo la shughuli za Kibinadamu. Hifadhi ya Ngorongoro kupewa hadhi ya kisheria ya kuwa Hifadhi ni mwaka 1959. Kinyume na hapo ingekuwa eneo la kawaida la shughuli za Kibinadamu kama maeneo mengine. Lakini pia Wamasai waliachwa pale siyo kwa sababu bila wao hifadhi haitakuwepo, hapana. Nikweli hawa watu walishaondolewa katika eneo lao la awali ambayo ni Mbuga ya Serengeti na kuhamishiwa Ngorongoro. lakini ulipokuja tena umuhimu ya kuwa na hifadhi ya Ngorongoro kama vyanzo vya maji na masalia ya wanyama ndo ikaweklwa hiyo Sheria kwamba liwe Hifadhi Mseto. Kule Serengeti pamoja na kwamba Wamasai hawali wanyama pori lakini waliondolewa.
 
Sometimes jaribu kuficha upumbavu wako. Ni Uongo mkubwa kudai wanahamishwa kwa sababu za uhifadhi. Pale kinachofanyika ni kuwafukuza. Huyo anayejiita chura kiziwi wenu hajawahi kuwa na uchungu na uhifadhi, sio ajabu anataka madini yachimbwe huko mbugani kisa TU "wanyama hawali madini". Hapa wanataka kuwapa hao wawekezaji uchwara "waarabu". Hata Zenji ardhi ipo, waende huko wakagaiwe.
Punguza Mhemko. Limeulizwa swali la msingi kwamba Bado tunahitaji Ngorongoro iendelee kuwepo kama Hifadhi? Au iendelee kuwepo kama ardhi ya kawaida ya shughuli za Binadamu?

Kama tunataka iendelee kuwepo kama hifadhi basi hakuina jinsi kule lazima idadi ya Wamaasi wanaoishi kule ipungue kwa kuhama ama kwa hiari au kwa lazima. Binadamu wazaliana, mahitaji yao ya chakula na mengine yanaongezeka, ardhi ile haiongezeki.
 
Mihemlo mnayo ninyi mnaotaka wengine wafukuzwe ili muwakabidhi wawekezaji wenu uchwara mpige Pesa. Wajinga sana nyie.
 
Kwani enzi hizo na Ngorongoro ilikuwa hifadhi? au pori tu na eneo la shughuli za Kibinadamu. Hifadhi ya Ngorongoro kupewa hadhi ya kisheria ya kuwa Hifadhi ni mwaka 1959. Kinyume na hapo ingekuwa eneo la kawaida la shughuli za Kibinadamu kama maeneo mengine. Lakini pia Wamasai waliachwa pale siyo kwa sababu bila wao hifadhi haitakuwepo, hapana. Nikweli hawa watu walishaondolewa katika eneo lao la awali ambayo ni Mbuga ya Serengeti na kuhamishiwa Ngorongoro. lakini ulipokuja tena umuhimu ya kuwa na hifadhi ya Ngorongoro kama vyanzo vya maji na masalia ya wanyama ndo ikaweklwa hiyo Sheria kwamba liwe Hifadhi Mseto. Kule Serengeti pamoja na kwamba Wamasai hawali wanyama pori lakini waliondolewa.
[emoji7][emoji7]
 
Ni kweli neno Ngorongoro ni la asili ya Kimaasai (Korongoro). Lakini jina siyo uthibitisho wa historia kwamba fulani ndo mkazi wa asili wa eneo husika. Hata Misri mkazi wa asili siyo Muarabu. Hujui enzi za zama za kale na zama za kati Tanganyika ikiitwa AZANIA?

Lakini ukweli unabaki Watu wa kwanza wahamiaji kuingia eneo la Ngorongoro ya Leo ni Wairaqw, wakifuatiwa na Wabarbaig. wabarbaig hawakukaa muda mrefu kutokana na vita baina yao na wairaqw. Then, wakafuta Wamaasai na kufanikiwa kuwatimua Wairaqw.

Lakini katika ulimwengu wa leo aliye katika eneo husika ndo mwenye eneo maana Tanzania hii karibu kila kabila ni wahamiaji kama ambavyo leo huwezi kuwaambia wangoni Songea siyo kwao ingawa dunia inajua kabisa Wangoni ni Wahamiaji ten awa miaka tu ya karibuni katika karne ya 17 na 18.
[emoji7]
 
Rekebisha kidogo tuu, Wamasai hawakuvamia Ngorongoro bali mwaka 1959 walihamishwa kutoka Serengeti kwenda Ngorongoro na kuhifadhiwa humo, ikiwemo kula bure na huduma zote za jamii bure. Eneo hilo sio la Wambulu wala Wadatooga bali hao walikuwa wahamiaji tuu kama walivyo Wasukuma kule Ihefu au Wamasai wa Chalinze.

Wamasai walio Hampsthwaite kutoka Serengeti walikuwa ni elfu 8 tuu!, sasa wamezaliana na wengine kuvamia vya bure!, wako malaki kiasi cha kutishia ecological situation ya Ngorongoro, lazima wahamishwe kwa hiari, ikishindikana then ni kwa lazima!.
P
hoja murua kabisa. Lazima kama Nchi tuchague kimoja kati ya uhifadhi wa wanyama na uhifadhi wa Wamasai ndani ya eneo la wanyama wakati kuna ardhi kubwa nje ya hidhi pa kuwahamisha wamasai.
 
Kabla ya hiyo wilaya kuitwa Mbulu hakukuwa na neno hilo ?!!

Unafeli wapi mzee[emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Yap! katika kamusi ya wairaqw na katika lugha na asili yao hamna neno Mbulu halipo. Neno hili lililetwa na wakoloni Waingereza sijui walilitoa wapi. Eneo hili linaloitwa MBULU kwa Wairaqw wanaliita IMBORU. Inawezekana Watawala wa Kikoloni walishindwa kusikia na kutamka vizuri neno IMBORU badala yake wakalitamka na MBULU.

But jamii inayoishi eneo hili kwa uwingi ni Wairaqw. Pia zipo jamii zingine kwa uchache wakuwemo Wahadzabe na Jamii za wadatooga (Wabarbaig). WAIRAQW wanapatikana kwa uwingi katika eneo lote lilikuwa Wilaya ya Mbulu ambapo kwa sasa ina Wilaya nne na halmashauri sita (Mbulu, Karatu, Babati na Hanang') huku Mbulu na Babati zikiwa na Halmashauri mbili mbili kila moja.
 
Hakuna wahiraq wambulu acheni kujikana yaani tangu kabla ya uhuru wanajulikana wambulu mnakana jina la kabila lenu mbona wanyiramba hawajakana kuwa wao ni wairamba baadhi ya kabla hutambulikana kutokana na eneo waliko toka mfano hata wachaga wanajitambua kutokana na eneo wanakotoka hivyo zamani eneo lililotambulika mapema ni Mbulu na wanyeji ni wambulu
Hapana. katika orodha ya makabila za Tanzania hakuna kabila limeorodheshwa kama Wambulu. Ukisema Wambulu unawatenga Wakaratu, Wababati na Wahanang' na Wairaqw wengine waliotawanyika maeneo mengine. Kwa lugha ya asili ya jamii kubwa inayoishi maeneo hayo wanajiita Iraqw. Ndo maana jamii kubwa inayoishi maeneo hayo niliyoyataja linaitwa Wairaqw.

Kuwaita wambulu ni sawa lile la Wamasai wanaoishi Arusha kina koo za Mollel, Laizer nk kujiita WAARUSHA wakati wao ni wamasai. Ni sawa Wanyaturu wajiite WASINGIDA kwa sababu tu wanaishi Singida au WANYIRAMBA watiite WAKIOMBOI.
 
Back
Top Bottom