Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

hadi nitokwa na machozi nyakati tunaziacha gafla zinakuwa kama historia
 
Fredrick Bundala alihamia KAHAMA fm, ila baadae alirudi tena RFA miaka ya 2016. Kwasasa sijui yuko wapi huyo jamaa. Alivyorudi mara mojamoja alikuwa anashika kipindi cha Mambomambo.
 
Kuna jamaa alikuwa anapiga ngeli hapo kiss fm utafikiri akina Wayne Rooney, alikuwa anatangaza usiku saa nne aliitwa Bory the Pilot.
mwanzoni nlijua kiss fm sio redio ya tanzania. sasa kuna mmoja anaitwa seba aliondoka capital radio akaja kuanzisha hii ya kuhani musa mwanzoni akaikuza nikajua musa karudi huku na radio ni mpya kabla sijamsikia tena nasikia mambo ya kiroho ung'enge ulikuwa mwingi sana
 
mwanzoni nlijua sio redio ya tanzania. sasa kuna mmoja anaitwa seba aliondoka capital radio akaja kuanzisha hii ya kuhani musa mwanzoni akaikuza nikajua musa karudi huku na radio ni mpya kabla sijamsikia tena nasikia mambo ya kiroho
Zile vibe za Kiss Fm zilikuwa hazijakaa kibongo kabisa.
 
Sahara media ya Diallo ndio kuishiney
Rfa kifo ,star tv kifo , kiss FM kifo
Huyu mzee kafeli vibaya sana
Ukiangalia hizo media zilikuwa moja kati ya vyombo vya habari bomba kabisa
Wajifunze kwa Azam, Rostam, Dewj, Manji. Hawa jamaa wanazingatia sana muendelezo. Ukiwa mfanyabiashara mkubwa, unatakiwa ufanye trial za kukaa pembeni uachie watu wengine waendeshe kampuni yako ili ujue kama kampuni inaweza kuendelea bila ushiriki wako wa moja kea moja. Na ni vema kuchanganya family members na non family members.
 
Miaka hiyo kwa radio za diallo niliipenda sana kiss fm, ilikuwa na watangazaji wakali nawakumbuka akina The Bush Baby, Steve kabuye aka kafire, Dj Maliz, Tobi the splash na wengineo wengi
 
Kiss FM nlikua nafuatilia AT40 (american top 40) kila jpili nadhani kuanzia sa 10 au 11. Miaka inakimbia
 
Huu mwandiko[emoji1787]
 
Fredrick Bundala alihamia KAHAMA fm, ila baadae alirudi tena RFA miaka ya 2016. Kwasasa sijui yuko wapi huyo jamaa. Alivyorudi mara mojamoja alikuwa anashika kipindi cha Mambomambo.
Hilo group la akina Bundala walivyohama RFA walianzisha online radio iliitwa tone radio lakini haikudumu nadhani watz kusikiliza online bado. Baadaye kidbwoy akaenda Clouds, Sky Walker akaanzisha Dizzim tv na baadaye akauza sijui ndio akaanzisha SNS ipo mpaka leo na Irene akaenda East Africa Radio.
 
Zile vibe za Kiss Fm zilikuwa hazijakaa kibongo kabisa.
Ilikuwa na nguvu kiasi kwamba hadi iliwalazimu baadhi ya makampuni kutengeneza matangazo ya english maalum kwa kiss fm hata voda hawa wakiwemo. Leo ukiwasikiliza unakuta waganga wa kienyeji wanapewa airtime kinoma yaani kiss imekuwa kama radio ya wilaya huko.
 
Wengi wanashangaa kufa kibudu kwa radio hizi ili hali wanasema mwisho wa kusikiliza radio ni 2012 kurudi nyuma, hii inamaanisha kizazi cha redio kinapotea na sasa kimengia kizazi cha youtube,netflix, nyimbo za Flash na Tiktok.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…