Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamiliki wa baa na hoteli jijini Mwanza wamesema wataanzisha mgomo kuanzia kesho kutokana na baraza la Taifa la mazingira NEMC kufunga baa na hoteli zao huku nyingine zikipigwa faini kubwa kwa madai kuwa wanapiga muziki kupita kiasi.
View attachment 2630066
Wamiliki hao wamekutana kwenye kikao cha pamoja na kujadiliana kuhusu sheria za NEMC walizopewa hivi karibuni ambazo wanadai zinakwamisha shughuli zao na kusema ili waweze kupata ufumbuzi wa jambo hilo ni bora wagome kufanya kazi.
Chanzo: EATV
===
Tatizo kubwa la serikali ni kupitisha sheria mbovu ambazo siyo rafiki kwa wafanyabiashara sasa mwanza wameamua kwa kauli moja ya kutifungua bar wala hotel yoyote jijini humo, mimi kwa maoni yangu mama ni vizuri aanze ufatiliaji wa watendaji wake akiendelea kuwachekea asishangae kushindwa kuiendesha serikali.
Haya yanayotokea siyo hayo tu taasisi nyingi za umma zinekuwa kero kwa jamii kwa ujumla mwenye nacho ndiye anapata huduma anayostahili kila mtendaji wa serikali anafanya atskavyo yeye mwenyewe hii ni kwasababu hakuna ufatiliaji wowote unaofanywa watu wapo maifisini kula pesa za umma huku hakuna huduma zinazitolewa kwenye jamii
Namkumbusha mama ashituke wateule wake asipowafatilia basi ajiandae chombo kinazama bila yeye kujuwa[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]mgomo kesho Mwanza.
We ni boss wa TRA bilawanamgomea nani, wameona serikali dhaifu siyo? Wanatingisha kiberiti, wakifunga watakufa njaa wao na watoto washenz hao. Hata bar unagoma? Wajaribu waone, Hata hivyo waziri mkuu alionesha udhaifu mkubwa kusikiliza yale majambazi ya K/koo, wale ni wezi wa kodi za serikali, hawataki kulipa kodi wanajaribu serikali ya mama. Naomba mama awe strong hakuna mtanzania anataka kulipa kodi mpaka walazimishwe kwa sheria. Watu pekee nchi hii hawawezi kukwepa kodi ni wafanyakazi tu. Ndio maana nchi hii ni ya wakulima na wafanyakazi, wafanyabiashara wa nchi hii ni manyan'gau tu
Kabisa 🤣Kama hawawezi kudhibiti kelele shauri yao. !! Wakifunga mabaa itakuwa ni nafuu ya pesa zetu 😅😅🙏🙏
Kwangu hakuna walokole wanaopiga makelele mkuu!Vipi kuhusu wake walokole wanapiga makelele usiku?