Nilichojifumza kuhusu German cars hapa South Africa ni hiki,,usimiliki BMW, Benz au Audi ambayo imeisha warranty itakutesa sana. Rafiki yangu anamiliki corolla 2015 nilimsindikiza kwenye Kia dealership mwezi uliopita kufika pale tukakuta Benz, Bima Na Audi kibao mpaka tukauliza vpi? Mnauza na gari za kijerumani? Sales person akajibu hapana.
Watu wana nunua hizi gari mpya ambapo mara nyingi zinakuja na 60000 km 4-years warranty,hapo ina maanisha shida yoyote ya gari inakua chini ya manufacturers isipokua kama umepata ajali au umefanya matengenezo mwenyewe basi warranty inakua void. Warranty ikiisha tu watu wanaenda kufanya trade in na Toyota, Kia, Hyundai nk. Mtu anaithaminisha gari take kisha anapewa mpya, Ile aliyoiacha inakua kama sehemu ya malipo.
Kisha hao dealers wanaziuza kwa mtindo wa malipo ya installment Ila ulinunua service zote na matengenezo juu yako. Sasa bongo mtu unaagiza BMW , Benz au Audi una 15 yrs ujue kabisa huo ni msiba. Hizi gari zimeundwa ili ziwe zinaharibika kirahisi zikitumika sana,ziko complex kutengeneza,spare parts ghali nk. Buy them at your own risk.