Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
Upo sahihi mkuu,umesahau na mikoa yenye baridi blanket zinanuka
 
TATIZO WEWE ULILALA GUEST HAUKULALA LODGE KAMA ULIVYOANDIKA.
KUNA TOFAUTI YA HIVYO VITU, GUEST NDIO PANA UJINGA UJINGA HUO MAANA NI BEI RAHISI ILA LODGE BEI YAKE IMECHANGAMKA KIDOGO LAKINI VYUMBA NI VIZURI.
Sawa mtaalamu hizi mambo nimekubali, lakini gesti zipo kweli now days? sijaziona kitambo sana
 
Kuna wapumbavu wengine blankets wanazifutiaga shahawa halafu wanazikunja vizuri Kama hwajalitumia muhudumu akija analikunja vizuri zaidi.

Sasa ukijifnya mwamba ukaingia kwenye blanket utakutana na uvundo wa ajabu mno[emoji16]
 
Siku moja Moshi mjini mitaa ya Majengo nilichukua room kwenye lodge moja, 20k. Nilipoingia tu nikafunga mlango wa room kwa funguo, nikavua nguo direct kuoga bafuni. Huko bafuni nililazimika kurudishia mlango maana bafu ni dogo sana. Ile nafunga mlango nikasikia kitu kinaanguka upande wa pili wa mlango (upande wa chumbani). Sikujali nikaendelea kuoga.

Nimemaliza kuoga nafungua mlango haufunguki. Kumbe handle ya kitasa upande wa nje na kile kijichuma kinaunganisha handles na kitasa ndio vinedondoka.

Niliita wahudumu kwa nguvu sana ila wasisikie mpaka koo likauma na matusi yote hapo nimeshamaliza, na hakuna hata mteja mwingine room jirani anisikie awaambie. Wamekuja baada ya nusu saa hivi ila hawawezi kuingia chumbani kwangu kwani nimefunga. Funguo za akiba hawana anazo boss mwenye guest house. Boss amepigiwa yupo mbali, shambani. Alikuja baada ya kama 3hrs hivi. Muda wote huo nipo chooni tu.

Walipofungua nikatoka. Jicho nililowakata wakaelewa namaanisha nini. Wakanirudishia hela yangu bila kusema chochote nikaondoka kutafuta lodge nyingine.
[emoji16] kupenda vya buku jero tu
 
Kuna lodge nililala Kakola Shinyanga eeeh bwana chumbani aliingia yule mdudu mweusi kama mpanzi.

Huyo mdudu Kelele zake zinatakiwa azipigie nje kwenye uwazi sio chumbani aisee triiiiiiiiiiiiiiiìiiiiiiiiìiiiiii triiiiiiiiiiiiiiiiiiìi usiku kucha sauti yake nilikuwa naisikia kwenye ngoma ya sikio.

Niliamka kichwa kinaniuma Asubuhi, mawazo yangu nilijua mdudu yuko nje ya dirisha. Wakati navaa viatu nikamwona aisee nilimkanyaga kwa hasira.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mwaka jana miezi kama hii (msimu wa baridi) nilisafiri kwenda Mafinga, sasa katika kutafuta lodge nikaangukia lodge moja hivi ambayo kampuni hiyo ya lodge wana hoteli jina kubwa tu Mikumi pia...

Sasa nishalipia, nimepewa chumba na nahitaji kuoga ndipo nilipoanza kuona mapicha picha...

Maji ya moto hayatoki sijui kuni zimelowa maji hivyo wanahangaika kuzikausha, kumbe maeneo ya huko wana teknolojia yao ya kuchemsha maji kwa kuni, reservoir ya maji ni kitanki kimejengewa kwenye kitu kama tanuri hivi...

Pili, hata hayo maji ya moto yakiwepo basi yanatoka kwa ratiba na ni muda ule mtu wa kuchochea kuni atapokuwepo...

Nilikaa usiku mmoja tu, kesho yake nikatafuta mahali pengine
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom