Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

Sio kila mtu anaweza kufanya biashara
Kwa hiyo unapenda kazi ya u referee kama kwenye mpira referree kujifanya anaujua mpira sana wakati hajawahi Chezea hata timu ya uchochoroni

Maisha sio u refferee kama wa mpiran wa miguu Ingia ucheze .Kafungue lodge yako tuone.

Huwezi jua nini kinawakwamisha hao unawaita wana.lodge mbovu washindwe kuboresha hizo lodge ziwe kiwango chako unachokiota
 
Kuna lodge nililala Kakola Shinyanga eeeh bwana chumbani aliingia yule mdudu mweusi kama mpanzi.

Huyo mdudu Kelele zake zinatakiwa azipigie nje kwenye uwazi sio chumbani aisee triiiiiiiiiiiiiiiìiiiiiiiiìiiiiii triiiiiiiiiiiiiiiiiiìi sauti yake nilikuwa naisikia kwenye ngoma ya sikio.

Niliamka kichwa kinaniuma Asubuhi, mawazo yangu nilijua mdudu yuko nje ya dirisha. Wakati navaa viatu nikamwona aisee nilimkanyaga kwa hasira.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nikienda lodge huwa nakagua kila kitu ninachohitaji kabla sijaandikishwa, maana ilishawahi nikuta nililipia chumba kabla sijakagua nikakutana na mambo ya ajabu aheri hata kuomba hifadhi kwa mtu ili upumzike.
 
33.Usiku wanakuja madada poa halafu kibabe..
34.wanazuia kuvuta ndumu ndani..(huwa wananikera sana.) ndio maana huwa nawaambia waiteni police wanikamate au mtaniua humu..
35. Kale kadude ka kupasha maji yawe moto kapo ila hakafanyi kazi (heater)

36. Bomba mvua / shower haina koki yaani haifunguki hivyo ukitaka kuoga unakinga maji kwenye ndoo kwa kabomba ka chini
 
Kuna lodge nililala Kakola Shinyanga eeeh bwana chumbani aliingia yule mdudu mweusi kama mpanzi.

Huyo mdudu Kelele zake zinatakiwa azipigie nje kwenye uwazi sio chumbani aisee triiiiiiiiiiiiiiiìiiiiiiiiìiiiiii triiiiiiiiiiiiiiiiiiìi sauti yake nilikuwa naisikia kwenye ngoma ya sikio.

Niliamka kichwa kinaniuma Asubuhi, mawazo yangu nilijua mdudu yuko nje ya dirisha. Wakati navaa viatu nikamwona aisee nilimkanyaga kwa hasira.

Hahahah
 
Kuna tule tusabuni tudogo kama kiberiti, sijui wanavinunua Tsh100.. unapewa wakati umelipa 50k+ wanashindwa kutoa sabuni zinazoeleweka, sijawahi kuvitumia kuoga!
Mbaya unamkuta mwamba anaweka kwenye bag, sometime hata wateja tuwe serious!
Wanawake tukienda hoteli kama vile tunahama.
Mimi nikisafiri kitu ambacho sibebi ni maji tu sijui sabuni, dodoki, towels, mswaki ,dawa, etc vyote tunabebaga vya kwetu. Nyie wanaume ndo mnateswa na haya mambo.

Mfano sabuni ni kitu kidogo sana wakati unasafiri beba yako. Utatumiaje ilotumika kama aliyetoka jana aliitawazia? Hapana tubebe vitu vyetu.

Maana hata hotel kubwa wanaweka tule tu eva sasa tunavyo nuka vibaya mnatuogeaje?

Kama umeoa mkeo wakati anakuandalia kila kitu akuwekee kwenye begi lako.
 
Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
12. Blankets hazibadilishwi zinanuka

13. Mhudumu anakujibu lolote analojisikia, ili akujibu vyema mpaka umpe pesa kama tip

14. Hakuna uwiano wa maji ya moto na ya baridi kwenye Bomba la kuongea

15. Kutoa receipt ni mtihani

16. Lodge ni sehemu ya madada poa ya usiku kuleta wateja wao.

Yaani yako mengi na Wana KERO sana, nadhani wamiliki wengi wa hizi nyumba huduma ni mbovu kwa sababu wanatumia mapato ya hiyo lodge kufanya maendeleo mengine na lodge inajikuta haiwezi kujiendesha vyema, wanalazimika pia kuchukua wahudumu wa hivyo hovyo tu mitaani ambao hawajui hiyo kazi kama nayo ni taaluma za watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna lodge ilikuwa mpya kabisa ndo imetoka kuzinduliwa tu nikaenda kulala pale. Sasa nimeamka ile asubuhi kabla sijaingia kitaa nikasema ngoja nitest kama huwa wanafua yale mashuka. nikaweka kialama kdogo sana kwenye zile shuka nijue kama wamebadilisha shuka ama la. Nikarudi jioni nakagua zile alama zangu nakuta mashuka ni yaleyale hayajabadilishwa! Nikamvaa mdada wa mapokezi akajitoa ufaham eti alibadilisha nikakomaa akayatoa mashuka yote na kuweka mengine. niligundua muda wote yule dada alikuwa anachezea simu yake tu pale mapokezi anangoja maokoto mwisho wa mwez
 
Nimekuja kugundua lodge za dar es salaam za bei ya 50000 au 100000 zinalingana hadhi au zimezidiwa na lodge za mkoani za Tsh.25,000 au 30,000 mfano mzuri nenda singida uchukue lodge kama Tilito au mitaa ya mwenge ukiwa unakuja stend mpya, au mitaa ya Sky Way ujionee.
 
Kuna lodge ilikuwa mpya kabisa ndo imetoka kuzinduliwa tu nikaenda kulala pale. Sasa nimeamka ile asubuhi kabla sijaingia kitaa nikasema ngoja nitest kama huwa wanafua yale mashuka. nikaweka kialama kdogo sana kwenye zile shuka nijue kama wamebadilisha shuka ama la. Nikarudi jioni nakagua zile alama zangu nakuta mashuka ni yaleyale hayajabadilishwa! Nikamvaa mdada wa mapokezi akajitoa ufaham eti alibadilisha nikakomaa akayatoa mashuka yote na kuweka mengine. niligundua muda wote yule dada alikuwa anachezea simu yake tu pale mapokezi anangoja maokoto mwisho wa mwez
Huwaga ni walaini hawa watoto hawajui kukataa.
 
Back
Top Bottom