Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
Ungetupa uhalisia unazungumzuia Lodge zipi...za elfu 5,10,15,20,25,30,au 50!
 
Mwaka jana miezi kama hii (msimu wa baridi) nilisafiri kwenda Mafinga, sasa katika kutafuta lodge nikaangukia lodge moja hivi ambayo kampuni hiyo ya lodge wana hoteli jina kubwa tu Mikumi pia...

Sasa nishalipia, nimepewa chumba na nahitaji kuoga ndipo nilipoanza kuona mapicha picha...

Maji ya moto hayatoki sijui kuni zimelowa maji hivyo wanahangaika kuzikausha, kumbe maeneo ya huko wana teknolojia yao ya kuchemsha maji kwa kuni, reservoir ya maji ni kitanki kimejengewa kwenye kitu kama tanuri hivi...

Pili, hata hayo maji ya moto yakiwepo basi yanatoka kwa ratiba na ni muda ule mtu wa kuchochea kuni atapokuwepo...

Nilikaa usiku mmoja tu, kesho yake nikatafuta mahali pengine
 
Duh [emoji849][emoji849] wew utakuw umeend kukagua lodge


Mimi hizo lodge tatzo langu kubwa ni wao kukodsha chin ya masaa24

Natak lodge mtu akiigia saa 2 usiku hadi kesho saa usiku
Mkuu imekuwa ni mitandao ya simu ,kwamba ukiiunga leo saa nne mpaka kesho tena saa nne
 
Ubungo stendi zipo hoteli za bei hiyo na haya malalamiko yapo Tele..tiles za bafuni chafu....TV Haina channels...
Mabomba yameharibika n.k
Acha uongo itaje jina hotel hata moja ya 60k hapo ubungo yenye upuuzi huo

Ww umezoea kulala gest bubu za 15k unataka kuhalalisha upuuzi huo na kwenye hotel
 
Kuna lodge ilikuwa mpya kabisa ndo imetoka kuzinduliwa tu nikaenda kulala pale. Sasa nimeamka ile asubuhi kabla sijaingia kitaa nikasema ngoja nitest kama huwa wanafua yale mashuka. nikaweka kialama kdogo sana kwenye zile shuka nijue kama wamebadilisha shuka ama la. Nikarudi jioni nakagua zile alama zangu nakuta mashuka ni yaleyale hayajabadilishwa! Nikamvaa mdada wa mapokezi akajitoa ufaham eti alibadilisha nikakomaa akayatoa mashuka yote na kuweka mengine. niligundua muda wote yule dada alikuwa anachezea simu yake tu pale mapokezi anangoja maokoto mwisho wa mwez
Mie uzuri wangu shuka likilaliwa tu huwa najua,nikilinusa.
 
Fursa hiyo jitose kwenye biashara ya Lodge nzuri.Jenga zako nzuri upige pesa
Badala ya kukaa unalaumu humu watu wenye lodge mbovu
Atajenga lodge nchi nzima? Watoa huduma ni lazima waelezwe ili waboreshe huduma zao. Lasivyo tukilalamikia bank mtu akwambie jenga bank yako, ukilalamikia hospitali hivyo hivyo kweli?
 
Atajenga lodge nchi nzima? Watoa huduma ni lazima waelezwe ili waboreshe huduma zao. Lasivyo tukilalamikia bank mtu akwambie jenga bank yako, ukilalamikia hospitali hivyo hivyo kweli?
Tatizo kubwa umaskini wa hela

Tafuta pesa Lodge huendana na mfuko wa mtu.

Mbona ziko kibao tu ni pesa yako tu tofauti na benki zinazohudumia watu wote wenye pesa.nyingi na malofa kwenye jengo moja
 
Ubungo stendi zipo hoteli za bei hiyo na haya malalamiko yapo Tele..tiles za bafuni chafu....TV Haina channels...
Mabomba yameharibika n.k

Do inspection before you check in, shida nu kwamba unafikiri unasafiri wenyewe.
 
Atajenga lodge nchi nzima? Watoa huduma ni lazima waelezwe ili waboreshe huduma zao. Lasivyo tukilalamikia bank mtu akwambie jenga bank yako, ukilalamikia hospitali hivyo hivyo kweli?
Na ukikuta restaurants kigoma huduma mbovu..ujenge restaurants kigoma na nchi nzima??
 
Back
Top Bottom