Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

Mwaka 2007 nilikwenda Korogwe, kulikua na send-off . Baada ya sherehe mishale ya saa sita jamaa yangu akani drop mbele ya Magoma guest house. Wakafungua na kunipa room. Aisee!! Shuka hazijafuliwa, Ile naendelea kuchunguza nikakutana na kunguni wenye njaa, mvunguni mende wametawala. Ilibidi nivue nguo zote ili nisije kubeba mbegu ya chawa wa CCM na kunguni.
Nikilala usingizi wa mang'ang'am haswa.
Kifupi Ni kwamba wasambaa hospitality industry waachieni wakinga.
Hunilazi kitanda chenye mdudu yoyote yule nikapata usingizi hata lepe.
NJE YA MADA.
Mimi baada ya kuoa rasmi na kuanza kuishi na mke na watoto nyumba moja sijui nini kilitokea ila nili develop hisia sensitive za hali ya juu sana. Yan hata nilale usingizi fofofo akinigusa tu kunguni au sisimizi au mbu, yan ghafla tu paap!! Usingingiz unakata instantly naamka.Hata niwe usingizin kias gani mtu akigusa kitasa cha mlango wa chumbani kwa nje ghafla usingiz unapaa!!. Ilinitesa sana hii situation mpaka baada ya miaka kama miwil hiv ndio nimeweza kui controll.
TURUD KWENYE MADA.
Mwaka 2018 nilikutana na kadhia hii hii mkoa wa morogoro kulikua na maadhimisho ya siku kuu ya nane nane kitaifa kama sikosei..Sehem za kulala nyingi zile nzuri zilijaa sana nikapata shida sana kupata mahala pa kulala nikaangukia guest bubu.
Nikakagua kitanda nikaona kunguni, nikajionsa isiwe tabu, nikawasha laptop nikakesha mezani mpaka asubuh
 
Halafu kwa wamiliki wa lodges na hotel jitahidi kufunga kamera za usalama kwenye jengo lako hua zinasaidia sana wakati mwingine hasa nje, mapokezi, kwenye korido za kuingia vyumbani, na kila mgeni aandike jina lake halisi either aoneshe kitambulisho au kwa raia wa kigeni lazima akuoneshe hati yake ya kusafiria ili unakili namba zake kwa ufasaha,
Guest ya hivyo wateja wakijua huwapati ng'oo. Katika vitu vinawapa hela wamiliki wa lodge ni wateja wanao ingia kupigana mti na utakuta ni mume au mke wa mtu wanafunzi nk sasa hayo mambo ya camera tena na watu ambavyo mafriji hayagandishi hakuna maana ya faragha hapo hukawii kukuta clip yako ikiwa hewan mzee mzina inaingiza room katoto.
 
nilikua nafanya dhambi mara kadhaa pale lunchtime hotel nikiwa mabibo hostel, asee nimerud after 5yrs hakuna kitu kizima kuanzia ac, koki za chooni/bafuni, kiti/meza mpk kitasa cha mlango ni tia maji tia maji, uzuri tu bei imeshika kidogo[emoji3]
 
Siwezi sahau enzi za ujana wangu, nimeenda Morogoro nikachukua lodge moja nzuri sana kwa mwonekano, sasa nikawa na ka pisi “ka albino”, shida ikaja wakati wa kuoga...nimeingia bafuni fungua maji ni ya chumvi yaani bora hata ya baharini. Kuoga mimi macho yakaanza kuwasha shauri ya chumvi. Ka albino kangu hakawezi kuoga maji ya chumvi na ngozi na macho yake, aise niliteseka. Ilinibidi ninunue maji yale ya kwenye kichupa kikubwa kwa ajili ya kuoga yeye.
 
Back
Top Bottom