Wamiliki wa mabasi fursa mmetengenezewa hiyo hapo chukueni hela

Wamiliki wa mabasi fursa mmetengenezewa hiyo hapo chukueni hela

Mfano unaongea na wenye basi unaweka mtu ofisini kwao kila mkoa so ndiye anayekuwa anafanya hii kazi Kama wao wanaogopa kufilisiwa.
Eti Kuna mkijani mmoja anadai eti lipa tozo afu uone matokeo yake Mana hazipendi mifukoni mwao hao jamaa waliozileta.
Na ilala mmekosa nini mpaka mkatuletea huyo mzalendo ambaye hata Mia yake haikatwi.
Yaani wao wangeanza wao kwanza wakatwe tuone Kama ni wazalendo.
Afu eti kajamaa kalikorudia pr anadai ni tozo ya uzalendo mbona wao hawakatwi ama wao uzalendo hauwahusu kweli.
Tuwe wazalendo wote kwa mifano jamani na sio wachache wanajazwa kichwa eti uzalendo Mara wanyonge kumbe ni gia ya kuwakamua
Wao wakatwe million 2 kwenye mishahara yao ili tuwaone ni wazalendo kuanzia mawaziri mpaka wabunge
 
Naona ni wakati wa E-wallet huduma zake zianze kuwa applied hapa bongo, kwasababu makato Yanataka Kuwa makubwa kwenye hizi local transfer zetu
Wataziletea kodi tu yani kuitumia lazma waweke mfumo wa kukwamishana
 
Eeh ni kutengeneza Metropolitan Network tu na mawakala wengine ambao mnaaminiana!

Kwa Tabata unakuwa na mtu kila kituo kuanzia stand ya Kimanga pale to Bima to Segerea na kila muamala unachaji buku tu wala sio hela nyingi! Kupitia network hio nyie kama mawakala mtapiga hela hadi mchoke sababu hela zenu zinakuwa zinazunguka na commission ni cash money! Kadri mtandao wako wa trusted patners unavyoongezeka ndivyo ambavyo mnazidi kupiga hela!

Kikubwa unaji market tu kama wakala wa zone ya Tabata kwahio watu wote wenye shida za kutuma hela maeneo hayo wakutumie wewe tu network yako ya patners inakuwa wazi na ukomo wako wa huduma mwisho labda saa 10 jioni kwa sababu za kiusalama zaidi! Mnakutana mlimani City mnapeana kila mtu kibunda chake kulingana na records game over!

Hela mnakuwa hampitishi kwa hawa wanyonyaji wa mitandao na mwigulu! Wasifikiri ile system yao ni kitu cha ajabu sana mbinu zipo bado!
Idea nzuri sana....
kadiri serekali inavyoleta magumu watu wanajiongeza....
 
Wao wakatwe million 2 kwenye mishahara yao ili tuwaone ni wazalendo kuanzia mawaziri mpaka wabunge
Yaani wakubali kula 5M Kama hawataki waachie hizo nafasi Kuna graduates kibao mtaani watagombea hela inayobakia hapo itumike Kama uzalendo kusaidia ujenzi wa madarasa pia kuajiri waalimu wa sayansi,shule nyingi za kata hazina walimu wa physics or maths.
Gari apewe double cabin Toyota inatosha kwani atazikwa nalo.
Yaani tunahitaji viongozi wao ndio wao mfano mzuri wa uzalendo.
Na sio wanatumia Kodi zetu kuileta Brazil kucheza na Taifa stars kwa gharama ya 3bn kisa mkuu wa nchi ajifurahishe jamani wakati Kuna wamama wanajifungulia njiani ama wagonjwa wanafia njiani maana ambulance hazipo.
Ila kweli Hawa viongozi kweli ni mafisadi.
Mag bado hajaoza tutamkumbuka
 
Ni wazo zuri sana lakini hii Serikali haramu inaweza kabisa kupiga marufuku ili tu ihakikishe inatukamua Watanzania kisawa sawa.

Habari zenu wanajukwaa!
Tupeane namna ya kukwepa kutuma hela kwa simu Mana jamaa wanadai wazalendo Ila hata Mia Yao mbovu haikatwi pia hatunziwi hela wake kupewa wakizeeka Ila wewe ndiye wa kutunziwa pia ndiye wa kulipa Kodi ya kizalendo.
Jamaa wamelewa Kodi zetu,kumbuka yeye hajui kuwa Kuna shida afrika yaani yeye anaishi life hata mzungu wa uk hampati.

Nisiwapotezee muda ishu Iko Ivi Kama mwenye umiliki wa mabasi ama mtu anaweza akaingia nao ubia wakafanya biashara hii.
Niko dar natoa hela kwa kampuni labda ni 50k afu wewe uko mbeya uko kwa iyo ofisi ya hapo mbeya wao wanahakiki aliyeko dar akatoa hela afu wa mbeya anapewa hapo baadaye wanajumlisha fresh Mambo yanaenda.
Mie Niko zangu Singida unayemtumia uko bukoba nenda ofisi Fulani wasiliana nao yaani ukiwapa tu wa bukoba namie Niko singida nachukua.

Pia kuweka hela benki Mana mawakala wamejaa kila Kona afu nenda atm chukua hela makato ni 1200 kila unapochukua hela kuanzia 5k mpaka 400k.
Na kwa atm waweza chukua mpaka 2M so makato jumla ni 1200*5=6k.
Aisee hii njia ya mabasi wakitokea wakiwa na akili itakuwa poa sana.
Yanai ofisi ya mabasi ya kisire iko mza kahama na Tarime ni mwendo tu Niko kahama nawapa hela afu wao wanampatia hela wa mwanza Mana wanahakiki kuwa huyu jamaa mwenye namba hii mpe 50k.
Ngoja niachie hapa nadhani nimeeleweka. Makato wanaweka nusu ya yaliyopo kutumaa na kutokea.

Yaani wameweka kutuma na kutoa pote pote jamani kweli.
Yaani Hawa jamaa sijui wanalewa sana.
 
Yaani wakubali kula 5M Kama hawataki waachie hizo nafasi Kuna graduates kibao mtaani watagombea hela inayobakia hapo itumike Kama uzalendo kusaidia ujenzi wa madarasa pia kuajiri waalimu wa sayansi,shule nyingi za kata hazina walimu wa physics or maths.
Gari apewe double cabin Toyota inatosha kwani atazikwa nalo.
Yaani tunahitaji viongozi wao ndio wao mfano mzuri wa uzalendo.
Na sio wanatumia Kodi zetu kuileta Brazil kucheza na Taifa stars kwa gharama ya 3bn kisa mkuu wa nchi ajifurahishe jamani wakati Kuna wamama wanajifungulia njiani ama wagonjwa wanafia njiani maana ambulance hazipo.
Ila kweli Hawa viongozi kweli ni mafisadi.
Mag bado hajaoza tutamkumbuka
Alisema mtanikumbuka sana na sasa yanaenda kutimia aisee! Watu wamerudi kazini kwa kasi ya 5G ni mwendo wa kujichotea mipesa tu maana njia haziko tight nahakika ripoti ijayo ya CAG itaibua madudu ya ajabu sana!
 
Baada ya miaka 5 wanakunja mamilion yao , wanyonge tunazidi kuwa wanyonge kipeuo cha pili! Eee mwenyezi MUNGU twangalie watoto wako,hawa watu najua wewe wayaona machozi yetu yanavyotirirka katika mashavu yetu, kila tukitaka kunyanyuka tunakandamizwa fanya njia pasipo na njia, bahari ya Shamu watoto wako walivuka, hata sisi tunaweza kuvuka ukitaka, ni katika jina lako YESU lipitalo majina yote AMEN AMEN KUBWA.
 
Haiwezekani kwa sasa maana watu washazoeshwa urahisi wa mobilemoney
 
Haiwezekani kwa sasa maana watu washazoeshwa urahisi wa mobilemoney
Kama mimi siwezi kuacha maanake kubeba cash ni kipaji, nitakachofanya kila anaenilipa kwa njia ya simu lazima alipe na ya kutolea. Mwanzo nilikuwa napotezea ila hizi 16,400/- siwezi kuziacha zile kwangu.
 
Hii kitu walifanyaga Scandnavia Express enzi hizo naona sasa tunarudishwa zama hizo kijanja!
Wakifanya watakamatwa. Sidhani kama leseni yao inaruhusu kufanya kitu kama hicho.

Labda wachukue leseni ya kufanya hivyo.

Unaweza kufanya kimya kimya ila ukikamatwa, huo ni UHUJUMU UCHUMI.
 
Wakifanya watakamatwa. Sidhani kama leseni yao inaruhusu kufanya kitu kama hicho.

Labda wachukue leseni ya kufanya hivyo.

Unaweza kufanya kimya kimya ila ukikamatwa, huo ni UHUJUMU UCHUMI.
Hahahahah ni noma ila kwa wenye vibanda vya mpesa ukifanya haina madhara
 
Back
Top Bottom