Wamiliki wa mabasi fursa mmetengenezewa hiyo hapo chukueni hela

Wao wakatwe million 2 kwenye mishahara yao ili tuwaone ni wazalendo kuanzia mawaziri mpaka wabunge
 
Naona ni wakati wa E-wallet huduma zake zianze kuwa applied hapa bongo, kwasababu makato Yanataka Kuwa makubwa kwenye hizi local transfer zetu
Wataziletea kodi tu yani kuitumia lazma waweke mfumo wa kukwamishana
 
Idea nzuri sana....
kadiri serekali inavyoleta magumu watu wanajiongeza....
 
Wao wakatwe million 2 kwenye mishahara yao ili tuwaone ni wazalendo kuanzia mawaziri mpaka wabunge
Yaani wakubali kula 5M Kama hawataki waachie hizo nafasi Kuna graduates kibao mtaani watagombea hela inayobakia hapo itumike Kama uzalendo kusaidia ujenzi wa madarasa pia kuajiri waalimu wa sayansi,shule nyingi za kata hazina walimu wa physics or maths.
Gari apewe double cabin Toyota inatosha kwani atazikwa nalo.
Yaani tunahitaji viongozi wao ndio wao mfano mzuri wa uzalendo.
Na sio wanatumia Kodi zetu kuileta Brazil kucheza na Taifa stars kwa gharama ya 3bn kisa mkuu wa nchi ajifurahishe jamani wakati Kuna wamama wanajifungulia njiani ama wagonjwa wanafia njiani maana ambulance hazipo.
Ila kweli Hawa viongozi kweli ni mafisadi.
Mag bado hajaoza tutamkumbuka
 
Ni wazo zuri sana lakini hii Serikali haramu inaweza kabisa kupiga marufuku ili tu ihakikishe inatukamua Watanzania kisawa sawa.

 
Alisema mtanikumbuka sana na sasa yanaenda kutimia aisee! Watu wamerudi kazini kwa kasi ya 5G ni mwendo wa kujichotea mipesa tu maana njia haziko tight nahakika ripoti ijayo ya CAG itaibua madudu ya ajabu sana!
 
Baada ya miaka 5 wanakunja mamilion yao , wanyonge tunazidi kuwa wanyonge kipeuo cha pili! Eee mwenyezi MUNGU twangalie watoto wako,hawa watu najua wewe wayaona machozi yetu yanavyotirirka katika mashavu yetu, kila tukitaka kunyanyuka tunakandamizwa fanya njia pasipo na njia, bahari ya Shamu watoto wako walivuka, hata sisi tunaweza kuvuka ukitaka, ni katika jina lako YESU lipitalo majina yote AMEN AMEN KUBWA.
 
Haiwezekani kwa sasa maana watu washazoeshwa urahisi wa mobilemoney
 
Haiwezekani kwa sasa maana watu washazoeshwa urahisi wa mobilemoney
Kama mimi siwezi kuacha maanake kubeba cash ni kipaji, nitakachofanya kila anaenilipa kwa njia ya simu lazima alipe na ya kutolea. Mwanzo nilikuwa napotezea ila hizi 16,400/- siwezi kuziacha zile kwangu.
 
Hii kitu walifanyaga Scandnavia Express enzi hizo naona sasa tunarudishwa zama hizo kijanja!
Wakifanya watakamatwa. Sidhani kama leseni yao inaruhusu kufanya kitu kama hicho.

Labda wachukue leseni ya kufanya hivyo.

Unaweza kufanya kimya kimya ila ukikamatwa, huo ni UHUJUMU UCHUMI.
 
Wakifanya watakamatwa. Sidhani kama leseni yao inaruhusu kufanya kitu kama hicho.

Labda wachukue leseni ya kufanya hivyo.

Unaweza kufanya kimya kimya ila ukikamatwa, huo ni UHUJUMU UCHUMI.
Hahahahah ni noma ila kwa wenye vibanda vya mpesa ukifanya haina madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…