Wamiliki wa mabasi fursa mmetengenezewa hiyo hapo chukueni hela

Hivyo zamani tulikuwa tunafanya
Unatuma hela mpaka kongo na.malawi zambia etc

Ova
 
Hili wazo nimelipata Jana usiku, nikawaza niweke sh m3 cash kijijini kibosho, mimi nipo kariakoo Watu kibao wanatuma hela pale kijijini, wananipa hapa town kisha mtu anaenda kuichukua hapo kijijini dukani.
Zikifika Labda M2 huku kwangu namuwekea kwenye akaunti ya bank akachukue dirishani Moshi.
Makato /gharama Natumia Yale ya mpesa /tigopesa ya zamani.

Asante Mwigulu Kwa kutuongezea fursa
 
Hii njia inausumbufu mwingi na gharama kubwa zaidi.
Tulishatuma pesa sana scandnavia enzi hizo kabla ya sim pesa.
Kwenye kila sh10,000 walikuwa wanachukua sh1000. Ukijumlisha na huo usumbufu wa kufuata huduma kwenye kituo Cha basi husika.
Nazani kwakuwa tuligoma kuitwa wanyonge acha tulipe tu hakuna namna.
 
Namie nafanyia wazo lako biashara mangi. Namie kijijini kwetu Keisangora naweka mtu kwa dizaini iyo.
Big up Sana. Ni lazima Sasa watu wafanye hizi biashara Mana hazina stress.
Kama hao wasomali waliokuwa uk unatumiwa hela tokea huko so unapeleka kwa ndugu zao wa majuu afu wewe unaichukua hapa fasta.
So jamaa walikuwa wanakula ya transfer na exchange rate wanapiga twice.
Mana watakuambia akatuma Dola 400 exchange rate ni hii so zidisha uone.
Wanakupiga sh 5-10 kwa Dola wanafanya biashara.
Mana Western Union nao Wana makato Yao.
Pia wire transfer inachukua karibia siku 3-5 Tena siku za kazi
 
Ni njia ilianzishwa na watu,wakati wahusika wa huduma za fedha walikuwa wamelala hakuwa na hawajawahi kuja na idea hiyo, hata hivyo ilisaidia sana

Ova
 
Sema idea nzuri sana hii nimeielewa! Naweza nikaifanyia kazi hata mimi!
Imekaa vzur kama Bank fulani ila ikishika kasi lazma kuna kodi itaandaliwa juu yako na taratbu kibao zitatengenezwa ili imrad tu wakukatishe tamaa....

By the way watasema mabus ni kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo tu sio pesa.
 
Imekaa vzur kama Bank fulani ila ikishika kasi lazma kuna kodi itaandaliwa juu yako na taratbu kibao zitatengenezwa ili imrad tu wakukatishe tamaa....

By the way watasema mabus ni kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo tu sio pesa.
Kwenye ma bus lazma ije kupigwa ban tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na fine kubwa ili kuwajambisha
 
Kwenye ma bus lazma ije kupigwa ban tu [emoji23][emoji23][emoji23] na fine kubwa ili kuwajambisha
Kabisaa yaan utapigwa jamba jamba mpka utaacha

Kuna Jokes moja inasema sio kila baya lina ubaya ile babe tuma na ya kutolea sa hv unasema njoo uifate Milion yako geto 20,000 ya kutolea chukua boda chap uje kama yuko Moro unamwambia chukua Abood hapo uje

NB. Kama kuna watu wamefurahia hii ni Bank kwa maana watu watarud sana kwenye ATM
 
Umeleta wazo zuri mkuu ila hili naona linahitaji kuanzisha system mpya ..kitu ambacho kitachukua muda kuanza kutoa huduma ya uhakika maskini tutakuwa tushaumizwa sana na haya makato..

WAZO LANGU: bado kuna mwanya kwa mawakala kuokoa hii system kandamizi. Nijuavyo mimi wakala kutuma pesa kwa wakala mwenzie hakuna makato hivyo basi anaetuma pesa aende kwa wakala na anaepokea pesa nae aende kwa wakala aliepo karibu nae kisha hawa mawakala watumiane pesa wao kwa wao .
Kisha wakala alietumiwa anatoa cash kwa yule aliekuwa anatumiwa hizo pesa na kwakua hakuna makato yoyote basi hawa mawakala watachaji makato yao kwa cash pale pale. Kwa kufanya hivi wakala atakuwa ameokoa biashara yake na wateja wataokoa pesa zao zinazokwenda na haya makato mapya.
 
Hahahaha eeh yani ukimbie 1,200 Atm ukimbilie kukatwa 4,750 kwenye simu
 
Wakiona traffic ya hivyo wataweka zuio πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kwa limits maybe hamna kurushiana zaidi ya kiwango flani kwa siku ama mwisho mara 3 kuhamishiana mpaka baada ya masaa 24!
 
Hii kitu walifanyaga Scandnavia Express enzi hizo naona sasa tunarudishwa zama hizo kijanja!

Mkuu wala usijali..waswahili sisi ni wasahaulifu sana! Hata wanasiasa wanajua namna ya kuishi na sisi. Hili litaongelewa siku mbili tatu...litaishia hewani na watu watazoea tuu....itunze hii post kwa reference!
 
Iko vizuri sana hii.
 
Iko vizuri sana hii.
Ni kama wale mawaka wa 1xbet wanavyofanya kazi kwa uaminifu mkubwa!

Everybody gets a fair share as well kwa kila transaction anaetuma analipa buku na atakaepokea ataacha buku! Mawasiliano yanafanyika live kwa whatsapp call.

Hamna hela ya mtu inayopotea cha msingi! Ila operation hii itainvolve zaidi kutuma hela sio kuweka kwenye personal account!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…