Nilipanda basi moja nikiwa naenda kusini. Safari ya masaa zaidi ya kumi. baada ya masaa manne dereva akasimama porini. Akatangaza Muda wa kuchimba dawa, dakika tano wanawake kulia, wanaume kushoto. Watu wakashuka wa wakatembea kama mita kumi, naona wanawake wanachuchumaa, wanaume wanafungua zipu.
Umbali kati ya wanawake na wanaume ni kama mita tatu. Konda anawahimiza wamalize shughuli chapchap, yuko nervous anasema polisi wanaweza kutokea muda wowote. Dah nilichoka.
Hivi Simba, chui, chatu au mnyama yoyote mfano angetokea, si angeondoka na mtu.