GE2025 Wamiliki wa "Online TV" zilizorusha maudhui ya Polepole wakamatwa na Polisi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Wakuu,

Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.

media.jpg

media1.jpg

Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!

Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.

media2.jpg

======

TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
​

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.

Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.

Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.

WAKAMATWA KWA KUENDESHA TELEVISHENI MTANDAO BILA LESENI.webp

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha “Televisheni ya mtandaoni” bila kuwa na leseni.

Waliokamatwa ni;
  1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga;
  2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV;
  3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na;
  4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.
Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani haraka kadri itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatiwa mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.
1760531366835.png
 
Tunasema hakuna ajira watu wanajichanga kufanya kile ambacho serikali yao imeshindwa kuwajibika ila bado hata huku wanawafuata..., Yaani kuwakamua wanawakamua na bado wakienda kujitafutia majani bado wanawakataza kula
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kupitia Kamanda Jumanne Muliro, limeeleza kuwa watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kumiliki vyombo vya habari (media) bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni Japhet Alex akiwa pamoja na Joseph Mabe, Tegemeo Zacharia, na Eliah Pius.

View attachment 3489008
Kwenye swala la online television hizi za YouTube binafsi naona polisi mnatumia nguvu nyingi bila sababu ya msingi.

kwanza mnatakiwa mkikuta hizo YouTube na mkawajua wahusika muwape elimu kuwa kwa hapa nchini ili umiliki online YouTube lazima uwe na leseni na utaratibu ni huu wapeni muda hata wa mwezi mmoja hadi mitatu wasajili hizo tv

Myie kwenu ni kosa ila kwa vijana ni dreams come true kwao ni namna pia ya kujiajiri na wengine wanaingia humo bila uzoefu wowote maana kufungua channel YouTube ni rahisi sana na sio complicated.

Muda mwingine tutumie hekima na elimu zaidi sio nguvu kila sehemu..
 
Hawa jamaa kwenye hii habari wamekamatwa kwa kuwa na channel youtube zisizokuwa na leseni. Yani mtandao wa kijamii unatakiwa uukatie leseni ya kuutumia. Na bado muda huo huo, AdSense hawakulipi pesa mpaka uweke TIN Number yako hili ukatwe kodi. Na sasa hivi kila YouTube anakatwa kodi ya lazima huko YouTube kupitia Google AdSense. As long as unalipwa na Google kupitia Google AdSense kwa wale bloggers wenye website au wenye YouTube basi wote wanalipia kodi TRA, pesa inakatwa juu kwa juu, utaambiwa tu uwezi kutoa pesa mpaka uweke TIN Number ya nchi ya Tanzania na Google wanakuambia ni sheria za nchi ya Tanzania.

Sasa swali langu, mtu wa YouTube anatakiwa awe na leseni ya kuwa na channel YouTube na ailipie hiyo leseni na wakati huo huo juu kwa juu TRA wanakata chao huko Google. Sasa kwa nini awe na leseni wakati TRA tayari wao wanakata chao juu na hawakuulizi huko kwenye google. Huu mfumo wa kodi ya TRA kumiliki YouTube bado haujakaa sawa, YouTube ni mtandao tu wa kijamii... Kodi ikatwe hatukatai, ila leseni ya YouTube ina kazi gani Sasa, ukiweka leseni ya YouTube weka na leseni ya Instagram na Facebook na Twitter, na TikTok kwa sababu zote zina maudhui yale yale na watu wanaingiza pesa kote.

View: https://www.instagram.com/p/DP1FmVDjNZ-/?igsh=MXBlbG00YzBsdGMxNQ==
 
Yote hii kutaka kutishia waandishi huru, katika wengi waandishi huru ni kwa kuwa wanatupatia kwa urefu na kina feedback ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Antipas Lissu inayoendelea sasa katika mahakama kuu ya Tanzania Kivukoni Front jijini Dar es Salaam

TOKA MAKTABA:
13 Oktoba 2025
Views 121,599 🔥

View: https://m.youtube.com/watch?v=py9Juz8lD60

TOKA MAKTABA :
Views 101,505
KESI ya uhaini ya Tundu lissu Leo 10/9/2025 mahakama kuu hizi ni updates Moja kwa moja kutoka mahakamani Karibuni Sana

View: https://m.youtube.com/watch?v=dU-FDMmMFbk
 
kwanza mnatakiwa mkikuta hizo YouTube na mkawajua wahusika muwape elimu kuwa kwa hapa nchini ili umiliki online YouTube lazima uwe na leseni na utaratibu ni huu wapeni muda hata wa mwezi mmoja hadi mitatu wasajili hizo tv
Huu upuuzi inabidi usiwepo in the first place... Hii serikali imezoea kutaka kula hata ambapo haitafuti wala kusaidia kutafuta; Acha tu kutaka kuziba watu midomo / uhuru kwa mgongo wa sheria bali Kodi / Makusanyo yasiyo na Tija au Uhalisia (Leseni haitoko Bure)
 
Wakuu,

Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.

Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!

Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.

======

TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
​

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.

Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.

Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.

Huenda pole pole ndio kawataja
Huyu mtu nadhani atakua hai bado anashikiliwa
 
Kwan mimi nikiwa na account ya YouTube nikaweka link ya live ya Polepole, ina maana mimi ni mwandishi wa habari .?

Sheria inasemaje .?
 
Wakuu,

Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.

Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!

Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.

======

TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
​

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.

Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.

Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.

Wandugu ni lini taifa letu,kama sii mataifa ya Afrika au duniani yatakuwa na watu wanaojali na kujua mahitaji ya wale wanaowaongoza ama kuwatawala?Je ni kweli uelewa haupo ama ni njia tu ya kuwadunisha watu wao,jamii yao na mataifa yao kwa kiburi cha mamlaka?
 
Kwenye swala la online television hizi za YouTube binafsi naona polisi mnatumia nguvu nyingi bila sababu ya msingi.

kwanza mnatakiwa mkikuta hizo YouTube na mkawajua wahusika muwape elimu kuwa kwa hapa nchini ili umiliki online YouTube lazima uwe na leseni na utaratibu ni huu wapeni muda hata wa mwezi mmoja hadi mitatu wasajili hizo tv

Myie kwenu ni kosa ila kwa vijana ni dreams come true kwao ni namna pia ya kujiajiri na wengine wanaingia humo bila uzoefu wowote maana kufungua channel YouTube ni rahisi sana na sio complicated.

Muda mwingine tutumie hekima na elimu zaidi sio nguvu kila sehemu..
Ingekuwa hivyo hata majambazi yangekuwa yanapewa elimu kwanza kuwa ujambazi ni mbaya. Kutojua sheria haikupi nafasi ya kutoadhibiwa endapo umekosea. Waliokamatwa ni wapumbavu mno. Wanajua kabisa hawana leseni halafu wanapost ujinga wa Polepole asiye na adabu.
 
Back
Top Bottom