GE2025 Wamiliki wa "Online TV" zilizorusha maudhui ya Polepole wakamatwa na Polisi

GE2025 Wamiliki wa "Online TV" zilizorusha maudhui ya Polepole wakamatwa na Polisi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii nchi inahitaji mabadiliko ya lazima ya kiutawala. Na kama hayatafanyika, basi tutegemee mgawanyiko na uasi wa hali ya juu baada ya Oktoba 29.

Mkuu sio lazima watu wabebe bunduki au kuwa waasi
CCM umeshafika mwisho wake
Wanakufa kifo Cha kwenye maji kutapatapa ni kawaida
 
Wakuu,

Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.


Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!

Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.


======

TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
​

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.

Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.

Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.


Aisee.
 
Bado waandamanaji,
kesi yoyote utapewa tu.
Na hapo utapoteza muda wa kutosha ndo utajua hujui.
 
Naona wanajaribu kufungia YouTube leo. Imeanza kuzingua mida hii ya saa 8:30 usiku. Pumbavu kabisa.

Haki ya Mungu wakifungia YouTube basi na mimi naandamana. Huku ni kuingiliana maisha sasa, wakati mimi sina muda na drama zao za kitoto. Kula wale wao alafu YouTube wanifungie mimi? Pumbavu.
 
Wakuu,

Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.


Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!

Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.


======

TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
​

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.

Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.

Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.


Last kick of a dying horse . Samia must go .
 
Hawa jamaa kwenye hii habari wamekamatwa kwa kuwa na channel youtube zisizokuwa na leseni. Yani mtandao wa kijamii unatakiwa uukatie leseni ya kuutumia. Na bado muda huo huo, AdSense hawakulipi pesa mpaka uweke TIN Number yako hili ukatwe kodi. Na sasa hivi kila YouTube anakatwa kodi ya lazima huko YouTube kupitia Google AdSense. As long as unalipwa na Google kupitia Google AdSense kwa wale bloggers wenye website au wenye YouTube basi wote wanalipia kodi TRA, pesa inakatwa juu kwa juu, utaambiwa tu uwezi kutoa pesa mpaka uweke TIN Number ya nchi ya Tanzania na Google wanakuambia ni sheria za nchi ya Tanzania.

Sasa swali langu, mtu wa YouTube anatakiwa awe na leseni ya kuwa na channel YouTube na ailipie hiyo leseni na wakati huo huo juu kwa juu TRA wanakata chao huko Google. Sasa kwa nini awe na leseni wakati TRA tayari wao wanakata chao juu na hawakuulizi huko kwenye google. Huu mfumo wa kodi ya TRA kumiliki YouTube bado haujakaa sawa, YouTube ni mtandao tu wa kijamii... Kodi ikatwe hatukatai, ila leseni ya YouTube ina kazi gani Sasa, ukiweka leseni ya YouTube weka na leseni ya Instagram na Facebook na Twitter, na TikTok kwa sababu zote zina maudhui yale yale na watu wanaingiza pesa kote.


View: https://www.instagram.com/p/DP1FmVDjNZ-/?igsh=MXBlbG00YzBsdGMxNQ==

In the name of siasa kila kitu kinawezekana
 
Serikali ya dikteta idd amin Samia inatumia rasilimali na kodi za watanzania kupambana na vyanzo vya habari ambavyo ni very unpopular na kuacha kupambana na mambo ambayo yanawaumiza wanainchi kama matapeli wa mtandaoni na wanaodhalilisha watu mitandaoni kwa kusambaza picha za uchi.
 
Kwenye swala la online television hizi za YouTube binafsi naona polisi mnatumia nguvu nyingi bila sababu ya msingi.

kwanza mnatakiwa mkikuta hizo YouTube na mkawajua wahusika muwape elimu kuwa kwa hapa nchini ili umiliki online YouTube lazima uwe na leseni na utaratibu ni huu wapeni muda hata wa mwezi mmoja hadi mitatu wasajili hizo tv

Myie kwenu ni kosa ila kwa vijana ni dreams come true kwao ni namna pia ya kujiajiri na wengine wanaingia humo bila uzoefu wowote maana kufungua channel YouTube ni rahisi sana na sio complicated.

Muda mwingine tutumie hekima na elimu zaidi sio nguvu kila sehemu..
Wewe hata huelewi!

Kwani hizo chanel zimefunguliwa mwezi huu? Au leo? Miaka yooote walikua hao polisi hawajui kuna sheria?

Zipo miaka na miaka sema ukipost kitu cha kuikosoa serikali ndio hizo sheria zinaanza fanya kazi!
 
Hawa ndio policcm wenu

Mhe. Lissu: ulisema umesoma chuo cha Unique Academy?

Kaaya: Ni kweli.

Mhe. Lissu: Hiki ni chuo gani hivi?

Kaaya: sio chuo kikuu, sio chuo kinachotoa advanced diploma, hiki chuo tulipelekwa maafisa wa polisi. Huwa tunapelekwa maeneo mbalimbali ikiwemo UDOM tunaendaga.

Mhe. Lissu: ukisema sina uhakika nalo ni jibu. Ukisema sijui nalo ni jibu. Sasa nataka unijibu swali langu hiyo unique academy inatoa diploma ya chochote.

Kaaya: nafikiri inatoa.

Mhe. Lissu: je hicho chuo kinatambulika na mamlaka ya ithibati ya hivyo vyuo vya ufundi?

Kaaya: Sijui kabisa
 
Je sheria za mitandao nchi jirani zinasemaje ? Tukilinganisha na hapa nchini kwetu Tanzania

Ndani ya Sheria Ambayo Itawafanya Raia Kukabiliwa na Faini ya Ksh 20 Milioni au Miaka 10 Jela kwa Machapisho ya Mtandaoni​

by Annah Nanjala Wekesa

Oktoba 16, 2025

Changarawe ya Mahakama. Picha/ Hisani
Nyundo ya mahakama. PICHA/ Hisani

Rais William Ruto, mnamo Jumatano, Oktoba 15, aliidhinisha Mswada kukabiliana na matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandaoni (Marekebisho) wa 2024, na kuufanya kuwa sheria rasmi.

Sheria hiyo mpya inaleta adhabu kali kwa utovu wa nidhamu mtandaoni, hasa unyanyasaji mtandaoni, ambao umeenea sana kwenye mitandao ya kijamii.

Chini ya sheria, mtu atakayefanya unyanyasaji kwa kutumia mtandao ikiwa, peke yake au na wengine, wanawasiliana-moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja-na mtu mwingine kwa njia ambayo anajua, au anapaswa kujua, inaweza kusababisha madhara.

Kosa hilo linajumuisha tabia ya mtandaoni ambayo inaweza:
  • Mfanye mtu aogope usalama wake au usalama wa mali yake;
  • Kusababisha madhara ya kihisia au sifa; au
  • Kuwa mchafu au mwenye kukera sana kwa asili.

Kenya Yatoza Faini ya Ksh 20 Milioni na Jela ya Miaka 10 kwa Unyanyasaji wa Mtandao​

Yeyote atakayepatikana na hatia ya unyanyasaji mtandaoni atakabiliwa na faini ya hadi Ksh 20 milioni, kifungo cha hadi miaka 10, au adhabu zote mbili.

Sheria pia inawapa waathiriwa haki ya kutafuta ulinzi kupitia mahakama. Mtu anaweza kuomba amri ya mahakama ili kumshurutisha mhalifu kusitisha mawasiliano hayo ya kuudhi au kuwazuia wengine kuwasaidia katika kuendeleza vitendo hivyo.

Mahakama inaweza kutoa amri za muda na zinahitajika kusikiliza na kuamua maombi hayo ndani ya siku 14. Katika kesi za dharura, ombi linaweza kufanywa nje ya saa za kawaida za kazi za mahakama, na mpatanishi anaweza kutuma maombi kwa niaba ya mlalamikaji.

Zaidi ya hayo, mahakama inaweza kuelekeza watoa huduma kushiriki maelezo ya mteja ili kusaidia kutambua wakosaji nyuma ya unyanyasaji.

Yeyote atakayekaidi agizo la mahakama chini ya kifungu hiki atahatarisha kutozwa faini ya hadi Ksh 1 milioni, kifungo cha miezi sita jela au zote mbili.


Soma Pia: Serikali Yaanza Kupambana na Watumiaji Mitandao ya Kijamii Saa Saa Baada ya Ruto Kutia Saini Sheria Mpya


Sheria ya Mtandao Inaipa Serikali Nguvu ya Kuzuia Tovuti, Kuzima Akaunti za Mitandao ya Kijamii​

Zaidi ya unyanyasaji wa mtandaoni, sheria pia inaidhinisha serikali kuondoa maudhui yanayoonekana kuwa haramu, yawe yanatumwa kwenye tovuti au vifaa vya kidijitali kama vile simu za mkononi.

Shughuli haramu za mtandaoni ni pamoja na ponografia ya watoto, maudhui yanayohusiana na ugaidi na desturi za kidini au kidini zilizokithiri.

Sheria hiyo mpya inaipa serikali mamlaka zaidi ya kutuma maombi ya kufungiwa mapema kwa majukwaa ya mtandaoni ikiwa wachunguzi wanaamini kuwa yanatumiwa kuwezesha shughuli za uhalifu.

Zaidi ya hayo, sheria mpya inazipa mahakama na mashirika ya uchunguzi mamlaka ya kisheria ya kuzuia tovuti zinazopangisha maudhui haramu, kuamuru kufungwa kwao, na kuwashurutisha wakosaji kuondoa nyenzo hatari.

Mamlaka hayo mapya yanafuatia kuanzishwa kwa Kifungu cha 46A, ambacho kinaipa mahakama mamlaka mapana ya kuamuru kufutwa kwa maudhui kutoka kwa vifaa vya kidijitali au tovuti, kuzima mifumo potofu, na kuidhinisha uingiliaji kati wa haraka katika kesi zinazoshukiwa.

Chini ya kifungu hiki, wachunguzi hawatahitaji tena kusubiri madhara kutokea, kwa kuwa sasa wana mamlaka ya kuchukua hatua mahakamani kabla ya maudhui haramu kuenea au kusambazwa mtandaoni.

"Ikiwa mtu aliyeidhinishwa anaamini kwamba mfumo wa kompyuta, tovuti, au kifaa cha dijiti kinatumiwa kuendeleza shughuli haramu, ponografia ya watoto, ugaidi, au desturi za kidini na za kidini zilizokithiri, mtu aliyeidhinishwa anaweza kutuma maombi mahakamani kwa amri ya kuondolewa kwa maudhui au nyenzo kwenye mfumo wa kompyuta, tovuti au kifaa cha dijitali," inasomeka sehemu ya sheria hiyo.

"Matumizi mabaya ya kompyuta yanarejelea matumizi yasiyoidhinishwa, urekebishaji, au ufikiaji wa mfumo wa kompyuta, programu, au data; na uhalifu wa mtandaoni unarejelea kosa linalotendwa kupitia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA kulenga mitandao, mifumo, data, tovuti, au teknolojia, au kuwezesha uhalifu."


Soma pia: Makosa 10 ya Kawaida Yanayoweza Kukuweka Jela


Mswada huo uliofadhiliwa na Mbunge wa Wajir Mashariki Aden Daudi Mohamed, ulichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 9, 2024, na kusomwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba mwaka huo huo.

Kuidhinishwa kwa mswada huo kuwa sheria kulijiri baada ya wabunge kuidhinisha na marekebisho mbalimbali yaliyopendekezwa na Kamati ya Idara ya Habari, Mawasiliano na Ubunifu, inayoongozwa na Mbunge wa Dagoretti Kusini, John Kiarie.

Katika mawasilisho yake kuhusu mswada huo, Kiarie aliutetea, akisema utapanua ufafanuzi wa wizi wa utambulisho ili kujumuisha manenosiri na kuharamisha kwa uwazi uigaji wa kidijitali, uvunaji wa data na wizi wa data binafsi.

Kiarie alidai kuwa Wakenya hutumia hadi saa nne na dakika kumi na mbili mtandaoni kila siku, na kuifanya nchi kuwa katika hatari ya kupata habari ghushi, uonevu wa mtandaoni, na taarifa potofu zinazozalishwa na AI.


Tag : 2024Muswada wa Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Makosa ya Mtandao (Marekebisho).Unyanyasaji wa mtandao

MAKALA SOURCE : Thekenyatimes.com
 
Je sheria za mitandao nchi jirani zinasemaje ? Tukilinganisha na hapa nchini kwetu Tanzania

Ndani ya Sheria Ambayo Itawafanya Raia Kukabiliwa na Faini ya Ksh 20 Milioni au Miaka 10 Jela​


16 October 2025

In this episode, we break down what each of these new laws really means ,from the Privatisation Bill that allows public assets to be sold without Parliament’s approval, to the Cybercrimes Amendment that could silence online voices in the name of “national security.

View: https://m.youtube.com/watch?v=nIowtQ_KByg
 
Back
Top Bottom