Mashujaa...Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha “Televisheni ya mtandaoni” bila kuwa na leseni.
Waliokamatwa ni;
Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani haraka kadri itakavyowezekana.
- Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga;
- Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV;
- Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na;
- Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatiwa mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.
Wakuu nina swali. Hivi nikitaka kuwaambia watu kitu ni lazima nipate kibali sirikalini?Wakuu,
Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.
Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!
Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.
======
TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.
Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.
Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.
Waulize ukianzisha YouTube channel unajisajiri wapi Tanzania? Na je kwa nini TRA wanachukua 5% ya mapato yao kama hawatambuliki Tanzania?Yaani YouTube channel imegeuka TV tena. Nahisi hilo neno Channel linawachanganya.
Hakuna uhakika wa maandamano lakini ni vizuri yakitokea.
Hawajauawa? Au ni zile maiti zilizopatilana juziWakuu,
Watu wanne waliokuwa wanamiliki akaunti za mtandao wa Youtube za Wispoti TV, T.Media Two na Costa Tv wamekamatwa kwa madai ya kuendesha akaunti hizo bila ya kuwa na leseni. Akaunti hizo ni kati ya zile zilikokuwa zikirusha press za Polepole kila alipokuwa akizitoa.
Kumbuka Polepole alishawahi kusema kuwa media zimelipwa huku nyingine zikitishwa kutorusha maudhui yake. Hili limethibitika sasa, maana waliokuwa wakiendelea kurusha maudhui hayo ndio kama hawa ambao kama walishindwa kuwashughulikia kipindi kile wanadili nao sasa ili kuzidi kuzima kelele zinazohimiza kupatikana kwa Polepole!
Media sasa zimekuwa za serikali na CCM, kila kitu wanachoposti kama sio cha kusifia CCM basi ni kuponda upinzani, na kuweka vitisho kwa wananchi ili waendelee kuwa watii kwao! Sheria za ovyo zinatumika kama fimbo ya kuwachapia wale wote wanaoonekana kuwa tofauti na serikali pamoja na CCM.
======
TAARIFA KWA UMMA
WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA KWA KUENDESHATELEVISHENI YA MTANDAONI BILA LESENI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, tarehe 03 hadi 10 Oktoba, 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha "Televisheni ya mtandaoni" bila kuwa na leseni. Waliokamatwa ni; 1. Japhet Alex Thobias, Mkazi wa Sabasaba Ukonga; 2. Joseph Augustino Mabwe, Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV; 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha, Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na; 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.
Upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili wafikishwe mahakamani haraka kadri watuhumiwa wote itakavyowezekana.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni watu wote wanaotuhumiwa kutenda makosa.
Imetolewa na;
Kamanda wa PolisiKanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam.
Hawa jamaa kwenye hii habari wamekamatwa kwa kuwa na channel youtube zisizokuwa na leseni. Yani mtandao wa kijamii unatakiwa uukatie leseni ya kuutumia. Na bado muda huo huo, AdSense hawakulipi pesa mpaka uweke TIN Number yako hili ukatwe kodi. Na sasa hivi kila YouTube anakatwa kodi ya lazima huko YouTube kupitia Google AdSense. As long as unalipwa na Google kupitia Google AdSense kwa wale bloggers wenye website au wenye YouTube basi wote wanalipia kodi TRA, pesa inakatwa juu kwa juu, utaambiwa tu uwezi kutoa pesa mpaka uweke TIN Number ya nchi ya Tanzania na Google wanakuambia ni sheria za nchi ya Tanzania.
Sasa swali langu, mtu wa YouTube anatakiwa awe na leseni ya kuwa na channel YouTube na ailipie hiyo leseni na wakati huo huo juu kwa juu TRA wanakata chao huko Google. Sasa kwa nini awe na leseni wakati TRA tayari wao wanakata chao juu na hawakuulizi huko kwenye google. Huu mfumo wa kodi ya TRA kumiliki YouTube bado haujakaa sawa, YouTube ni mtandao tu wa kijamii... Kodi ikatwe hatukatai, ila leseni ya YouTube ina kazi gani Sasa, ukiweka leseni ya YouTube weka na leseni ya Instagram na Facebook na Twitter, na TikTok kwa sababu zote zina maudhui yale yale na watu wanaingiza pesa kote.
View: https://www.instagram.com/p/DP1FmVDjNZ-/?igsh=MXBlbG00YzBsdGMxNQ==