Wamiliki wawili wa Ghorofa lililoporomoka na kuua watu 29 Kariakoo wamepelekwa Mahabusu, mmoja apata dhamana

Wamiliki wawili wa Ghorofa lililoporomoka na kuua watu 29 Kariakoo wamepelekwa Mahabusu, mmoja apata dhamana

Sasa kama mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi walipelekwa hapo kufanya nini? Kwanini hawakupelekwa kwenye mahakama yenye mamlaka badala ya kupoteza muda na rasilimali zingine
nami huwa najiulizaga sana hilo swali hz sheria zngne hazinaga mantiki kwakwel,
 
wengine wanafanyaga kazi gani? miaka 38 ana gorofa kariakoo, wengine ndo kwanza wanahangaika na madalali kimbiji
Magorofa mengi kariakoo ni ya Urithi usiogope sana!!
 
Sasa kama mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi walipelekwa hapo kufanya nini? Kwanini hawakupelekwa kwenye mahakama yenye mamlaka badala ya kupoteza muda na rasilimali zingine
Huwa inashangaza sana huu mtindo, sijawahi kuelewa.
 
Sasa Ulitaka Akiwepo Mtaani Achuchumae Na Si Kudunda?
Mahakama ina siasa zake,na kuzielewa ni kazi lubwa sana ,maana saa zingine zinaweza mpaa mtu haki bila sababu yoyote ile ambae siyo muhusika!!
 
Haya ni mambo ya kisheria na siyo kupoteza muda. Sheria inataka masaa ambayo ni lazima mtuhumiwa afikishwe mahakamani ili apte ''huduma ya kwanza'' eg dhamana. Ni kama unapoumia na unapelekwa dispensary ya karibu kupata huduma ya kwanza.
Sasa kwa nini asipelekwe kwenye mahakama iliyo na uwezo wa kusikiliza kesi yake kisheria?
 
Sasa kwa nini asipelekwe kwenye mahakama iliyo na uwezo wa kusikiliza kesi yake kisheria?
Mahakama za juu zinakuwa busy na haziko kila sehemu. Huu utaratibu ni mzuri kwa sababu unalinda haki ya mtuhumiwa kupata dhamana kwa haraka japo CCM inautumia vibaya kukomoa wapinzani wake.
 
Hao waliotajwa ni magumashi Tu hakuna mmiliki hapo hata hayo majina ni fake bado... mmiliki wa jengo anajulikana na yupo mtaani anadunda Tu
Kabisa haiwezekani hawa wakawa wamiliki wa ghorofa hilo huyo mkristo na waislamu wawili huwa mambo hayawi hivyo. Wamekosea kwenye kutunga uongo wao waanze upya.
 
Wamiliki wawili wa jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es salaam wamepelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana huku mmoja wao ambaye ni Leondela Mdete (49) akipata dhamana katika kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Waliokosa dhamana ni Zenabu Islam (61), Mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38), Mkazi wa llala ambapo kwa pamoja walipewa masharti ya kuwa na Wadhamini wawili kila mmoja wenye barua za utambulisho, kitambulisho cha Taifa na watatakiwa kusaini bondi ya shilingi milioni tano kwa kila mmoja.

Wafanyabiashara hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ambapo Wakili Mwandamizi wa Serikali Adolfu Lema akisaidiana na Neema Mwanga na Erick Kamala walidai kuwa Washitakiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 16 mwaka huu Mtaa wa Mchikichi na Kongo, jijini Dar es salaam.

Ilidaiwa kwamba, Washitakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya Watu 31 ambapo baada ya kuwasomea mashitaka hayo, Hakimu Mhini aliwaeleza Washitakiwa kwamba hawatakiwi kujibu lolote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo huku upande wa Jamhuri ukidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo ukaiomba Mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa, kesi imeahirishwa hadi December 12 mwaka huu.

Pia Soma: Wamiliki jengo lililoporomoka Kariakoo wafikishwa Mahakamani Kisutu
Kwamba wamiliki wa jengo la bil 3 wamekosa dhamana ya milioni 5. Au ni wabeba mizigo ?
 
Back
Top Bottom