LETA HATA HIYO REPORT UNAYOITA YA VIKAO HALALI
Kumbuka kwa mujibu wa Katiba ya ACT mkutano mkuu kumpitisha Membe ulifanyika na utakutana Baada ya miezi 60
Leta hayo maazimio yenu
5.3 Ndugu Msajili, maamuzi ya ushirikiano na vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na kuunganisha Chama kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ni moja ya maamuzi muhimu ambao lazima ufanywe na Mkutano Mkuu wa Taifa na chombo hicho hakiwezi kukasimisha madaraka hayo kwa chombo kingine bila kufuata utaratibu uliwekwa na Katiba yetu.
5.4 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa Ibara ya 18(i) ya Katiba ya ACT Wazalendo Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimu baadhi ya madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe wa kikao. Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu baadhi ya madaraka yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo. Lazima kuwe na Azimio Maalum.