Wana CCM kataeni UHUNI uliofanyika Dodoma

Wana CCM kataeni UHUNI uliofanyika Dodoma

Siasa za CHADEMA na minyukano hujaimaliza umehamia mambo ya CCM wakati Mbowe na Lisu na kambi zao kutwa kucha kuchambana. Hebu tuhangaike na ya kwetu
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Utakuja kufika wakati hili suala litapigiwa kelele sana. Ni nani alitegemea kusikia yote yanayosemwa na CDM juu ya Mbowe hii leo?

Ni kiasi cha muda tu, litakuja kuibuliwa na kila mmoja atakiri namna alivyolipokea.
Hayo yatasemwa baada ya raisi kutoka madarakani, sio sasa. Hapo ndio naposhangaa unafki wa wabongo. Hili nina uhakika wanaccm watalisema huko mbeleni na pengine kumtukana huyu aliyepo sasa kuwa waliburuzwa
 
Kama wewe siyo mwana CCM, NINI KINAKUUMA? Nilitarajia haya yasemwe na kuamuliwa na wana CCM wenyewe
Tumewasikia wanaccm wengi wakitoa maoni yao kwenye sakata la wagombea uenyekiti wa CHADEMA wenye akili wamekaa kimya hawahoji
 
Kwenu wana CCM mnaojitambua, wenye mapenzi mema na chama na mustakbali mwema wa nchi hii.

Hicho mlichofanyiwa Dodoma ni uhuni mtupu, hakipo ndani ya kanuni, taratibu wala culture ya chama.

Inakuwaje mnakubali genge dogo la watu wachache wanakaa chemba ili waje wawastukize kwa jambo nyeti kama hilo la kupata mgombea wa nafasi za Urais wa JMT na ZNZ?.

Kwa nini mgeuke rubber stamp tu ya maamuzi ya genge dogo lililokwepa taratibu za chama zilizozoeka?

Hebu jiulizeni, huyo anayekwepa mchakato wa kawaida wa kugombea anaogopa nini, kawakosea nini wana CCM hadi aruke vikao vya maamuzi vya chama kama mwanga arukavyo kwenye ungo?.

Ndugu wana CCM, mkikubaliana na uhuni huu maanq yake mnatengeneza precedence ya UHUNI mkubwa zaidi kufanyika ndani ya chama.

Aliyewahi kuwa katibu mkuu mwenezi wa CCM bwana Polepole amewahi kusema kuwa ndani ya CCM kuna WAHUNI na bila shaka mmethibitisha wenye hili jambo kwa UHUNI usio na chembe ya haya wala aibu, kwa kuletewa mgombea kwa mlango wa nyuma bila ngazi tofauti za chama na taratibu zake kufuatwa.

Najua bado mna hyesteria ya mkutano, wengine posho zimewatia upofu, Pengine mastarehe ya muda mfupi yaendayo na mkutano bado mna hangover nayo. Lakini Jiulizeni hiki kilichofanyika ni sawasawa.

Hebu simameni sasa muanze kukataa uhuni huu wa watu wachache kupika mambo sirini halafu wanakuja kuwastukiza kama mmekamatwa ugoni vile.

Msikubali kuwa pawns au kete za kutumika tu katika hii chess ya mustakbali wa chama na nchi. Anzeni kuonyesha hisia zenu waziwazi.

Hii siyo CCM ya Nyerere, hii ni CCM ya kihuni.
CCM achana nao ni chama cha wahuni, demokrasia IPO chadema tu
 
Back
Top Bottom