Wana CCM Tuendelee kuungana na kuwa kitu kimoja na Tuendelee kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Mama Samia, Wapinzani Wameishiwa pumzi

Wana CCM Tuendelee kuungana na kuwa kitu kimoja na Tuendelee kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Mama Samia, Wapinzani Wameishiwa pumzi

Mbolea imepungua nusu ya Bei ya mwaka Jana ambapo ilikuwa inauzwa shillingi laki na 40 lakini mwaka huu mbolea Kama DAP inapatikana kwa 70 Tu
Hiyo Bajeti inaweza kuwa ni sawa maana wengine hapa tulishaachana na mambo ya bajeti, lakini kwenye mbolea bado ipo 100k+ kutoka kwenye around 50k.
 
Ndugu zangu Wana CCM lazima Tufahamu kuwa Nguvu ya CCM na Wanaccm imekuwa Ni katika umoja wetu, Ushirikiano Wetu,mshikamano wetu ,upendo miongoni mwetu, UZALENDO wetu kwa chama na serikali yetu, misimamo yetu, kutanguliza mbele maslahi ya chama na serikali yetu, Sera na ajenda zetu pamoja na kuwa na Dira na muelekeo unaoeleweka na kuwa vutia watanzania katika kutuunga mkono na kutuchagua kila ufikapo uchaguzi wa aina yoyote Ile unapoitishwa na kufanyika

Nguzo hizi hatupaswi kuziacha, Wala kuzisahau,Wala kuzitupa,Wala kuhisi zimepitwa na wakati, Ni nguzo zilizotufikisha hapa Tulipo, Ni nguzo zilizokishikiria chama chetu, Ni nguzo zilizotufanya kuaminika kwa watanzania, kupigiwa kura kila uchaguzi, kupigania chama katika uchaguzi na kukilinda chama chetu kwa Hali na Mali, Ni nguzo zilizofanya maadui wa ndani na nje ya chama kukosa upenyo wa kukivuruga na kukisambalatisha chama chetu, Ni nguzo Zinazofanya chama hiki kionekane bado ni kijana kila siku, Ni nguzo zinazoongeza wanachama wapya kila siku,

Ni nguzo Zinazofanya kadi za CCM zitafutwe Kama Dhahabu katika ofisi zake na Ni nguzo ambazo zimekifanya CCM kuwa Tumaini la watanzania wa matabaka na Rika zote hapa nchini na zaidi Ni kuwa Ni nguzo Zinazofanya mwanachama akihama Leo CCM lazima kesho Arudi ndani ya CCM na kujutia uamuzi wake wa kukihama chama, mwisho ni kuwa hizi Ni nguzo Zinazofanya chama hiki kuwa kikubwa kuliko mtu binafsi na maslahi yake, Hakuna mkubwa ndani ya CCM, Kama huamini Hama leo CCM uone Kama kitayumba au kuyumbishwa

Hivyo lazima Tuendelee kuwa wamoja na kushikamana, Tusichonganishwe na mtu wa aina yoyote yule kwa misingi ya udini, ukabila, ukanda,jinsia Wala Hadhi, Tuseme na Tufahamu kuwa wote Ni sawa na tuna haki sawa ndani ya CCM, wote Tukipiganie na Tukilinde chama chetu kwa nguvu zetu zote, Hakuna mpinzani atakaye tulindia chama chetu Wala kutujengea chama chetu, Hakuna mpinzani anayependa kuona tukiwa wamoja, wapinzani wanatamani tusambalatike hata leo tu, Tusiwape upenyo huo

Tusiwape Siri zetu, Tusiwape mipango Wala mikakati yetu, Tusiwaonyeshe njia zetu.

Tumpe ushirikiano wakutosha Mwenyekiti wetu Mama Samia, Tumtetee kwa nguvu zetu zote popote tulipo, Tuwajibu wapinzani wetu kwa hoja nzito nzito, Tumbebe Samia wetu katika mikono yetu, na migongo yetu, Tusikubali ashambuliwe na wapinzani wetu,

Tufahamu akishambuliwa yeye Ni sawa na kwamba tumevamiwa sote, siasa Ni hoja na Ni sayansi, lazima Tuwe watu wa hoja muda wote zidi ya wapinzani wetu,CCM Ni moja, Wana CCM Ni wamoja na chama ni kimoja Tu CHAMA CHA MAPINDUZI, Tusiumizane, tusipaniane.

Tusiwekeane mitego wenyewe kwa wenyewe Wala Tusichukiane wenyewe kwa wenyewe, Wala Tusiangushane wenyewe kwa wenyewe kwa kumnufaisha mpinzani wetu

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

LUCAS Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Nyie na propaganda zenu uchwara ndiyo mnawaletea watu matatizo ....!!

Magufuli mlimdanganya hivyo mpaka alipoona moto wa kampeni za CDM ndipo akaishiwa nguvu. Kama ni kweli alikufa kwa matatizo ya moyo ..... basi uchaguzi utakuwa ulichangia kwa asilimia kubwa.
 
Acha kutumia nguvu ming iyo nguvu iamishie uchanguza wa 2030 huu wa sasa ushaisha na mshindi anajulikana

Labda yale mabunge ya jiwe yalopata ubunge wa kupema ndo yanahari ngumu na ayo ndo yatatoka yote bungeni
 
Unaiwinda nafasi ya Jerry Muro siyo Kwa debe hili! Ccm Mna uzalendo Gani zaidi ya kuifisidi nchi na kuwaibia wananchi Kwa njia ya tozo na kuhamasisha uvunjivu wa amani?
Muache mh Jerry Mulo achape kazi ya kulitumikia Taifa letu
 
CCM hii hii inayoiba kura na kulindwa na polisi ili ishinde uchaguzi?
images (3).jpeg
 
Ndugu zangu Wana CCM lazima Tufahamu kuwa Nguvu ya CCM na Wanaccm imekuwa Ni katika umoja wetu, Ushirikiano Wetu,mshikamano wetu ,upendo miongoni mwetu, UZALENDO wetu kwa chama na serikali yetu, misimamo yetu, kutanguliza mbele maslahi ya chama na serikali yetu, Sera na ajenda zetu pamoja na kuwa na Dira na muelekeo unaoeleweka na kuwa vutia watanzania katika kutuunga mkono na kutuchagua kila ufikapo uchaguzi wa aina yoyote Ile unapoitishwa na kufanyika

Nguzo hizi hatupaswi kuziacha, Wala kuzisahau,Wala kuzitupa,Wala kuhisi zimepitwa na wakati, Ni nguzo zilizotufikisha hapa Tulipo, Ni nguzo zilizokishikiria chama chetu, Ni nguzo zilizotufanya kuaminika kwa watanzania, kupigiwa kura kila uchaguzi, kupigania chama katika uchaguzi na kukilinda chama chetu kwa Hali na Mali, Ni nguzo zilizofanya maadui wa ndani na nje ya chama kukosa upenyo wa kukivuruga na kukisambalatisha chama chetu, Ni nguzo Zinazofanya chama hiki kionekane bado ni kijana kila siku, Ni nguzo zinazoongeza wanachama wapya kila siku,

Ni nguzo Zinazofanya kadi za CCM zitafutwe Kama Dhahabu katika ofisi zake na Ni nguzo ambazo zimekifanya CCM kuwa Tumaini la watanzania wa matabaka na Rika zote hapa nchini na zaidi Ni kuwa Ni nguzo Zinazofanya mwanachama akihama Leo CCM lazima kesho Arudi ndani ya CCM na kujutia uamuzi wake wa kukihama chama, mwisho ni kuwa hizi Ni nguzo Zinazofanya chama hiki kuwa kikubwa kuliko mtu binafsi na maslahi yake, Hakuna mkubwa ndani ya CCM, Kama huamini Hama leo CCM uone Kama kitayumba au kuyumbishwa

Hivyo lazima Tuendelee kuwa wamoja na kushikamana, Tusichonganishwe na mtu wa aina yoyote yule kwa misingi ya udini, ukabila, ukanda,jinsia Wala Hadhi, Tuseme na Tufahamu kuwa wote Ni sawa na tuna haki sawa ndani ya CCM, wote Tukipiganie na Tukilinde chama chetu kwa nguvu zetu zote, Hakuna mpinzani atakaye tulindia chama chetu Wala kutujengea chama chetu, Hakuna mpinzani anayependa kuona tukiwa wamoja, wapinzani wanatamani tusambalatike hata leo tu, Tusiwape upenyo huo

Tusiwape Siri zetu, Tusiwape mipango Wala mikakati yetu, Tusiwaonyeshe njia zetu.

Tumpe ushirikiano wakutosha Mwenyekiti wetu Mama Samia, Tumtetee kwa nguvu zetu zote popote tulipo, Tuwajibu wapinzani wetu kwa hoja nzito nzito, Tumbebe Samia wetu katika mikono yetu, na migongo yetu, Tusikubali ashambuliwe na wapinzani wetu,

Tufahamu akishambuliwa yeye Ni sawa na kwamba tumevamiwa sote, siasa Ni hoja na Ni sayansi, lazima Tuwe watu wa hoja muda wote zidi ya wapinzani wetu,CCM Ni moja, Wana CCM Ni wamoja na chama ni kimoja Tu CHAMA CHA MAPINDUZI, Tusiumizane, tusipaniane.

Tusiwekeane mitego wenyewe kwa wenyewe Wala Tusichukiane wenyewe kwa wenyewe, Wala Tusiangushane wenyewe kwa wenyewe kwa kumnufaisha mpinzani wetu

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

LUCAS Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Unakuta huyu wa hovyo anapenya kuwa mkuu wa mkoa ndo kina makonda hawa
 
Kwani wewe huoni juhudi za mh Rais katika kuijenga nchi hii na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja
Wewe utakuwa unaishi kwa shemeji ambako ukiamka unakuta kila kitu mezani. Hujui bei ya vyakula, gharama za nishati nk.
Maisha kwa sasa ni magumu zaidi ya wakati mwingine wowote labda 1974 wakati wa baa la ukame na 1980/82 baada ya vita ya Kagera.
Ushauri, kabla ya kuandika haya uwe unamuuliza anaye kuhudumia hali ikoje?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kwani umezuiliwa na Nani kwenda shambani? Acha nasi wakulima tufaidike na jasho letu maana miaka yote tulikuwa tunapata hasara huku nyinyi mkilakimvulini kwa kutupangia Bei mtakayo bila kujuwa gharama kubwa tuliyokuwa tunatumia katika kilimo
 
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

Credit: Malcom Lumumba
 
Kwa hiyo unataka CCM kisiwe na umoja mshikamano na upendo? Au unatakaje?
Wewe nakujua sio mwana ccm kabisa.ni vijana mnaomdharau mama samia kwa kumtangaza mkikaa na rafiki zako pale b bar sinza kuwa ukimsifia sana au ukiongelea vibaya wapinzani anatoa vyeo. Mnashindwa kujiajiri mnaanza kungangania kugombanisha viongozi wa ccm na wapinzani mpendelewe
 
Yaliyotokea October 2020 kupotea internet siku 5 huyajui au ulikua hujaja kwenye sehemu yenye access ya internet?
Hoja haipo kwenye suala la internet bali katika makaratasi hayo aliyoyashika mwanachama wenu Halima mdee
 
K
Wewe nakujua sio mwana ccm kabisa.ni vijana mnaomdharau mama samia kwa kumtangaza mkikaa na rafiki zako pale b bar sinza kuwa ukimsifia sana au ukiongelea vibaya wapinzani anatoa vyeo. Mnashindwa kujiajiri mnaanza kungangania kugombanisha viongozi wa ccm na wapinzani mpendelewe
Kweli wewe una matatizo makubwa, Mimi na bar wapi na wapi? Unajuwa niliko? Unajuwa mkoa niliopo? Unajuwa wilaya niliyopo? Unanifahamu Mimi? Umewahi niona wapi? Unazani wote Ni walevi wa kushinda bar Kama wewe? Acha kuongea ongea vitu kwa kubahatisha bahatisha tu mradi uonekane umeandika na wewe
 
Hoja haipo kwenye suala la internet bali katika makaratasi hayo aliyoyashika mwanachama wenu Halima mdee

Ngoja nikuwekee na video kabisa chawa wa Samia ndio maana nasema pengine issue ya internet ilika kikwazo kwako au ulikua hujafika mjini kabla ya uchafuzi mkuu wa 2020.

Video hiyo hapo ni kura zilizokutwa kwenye mabegi ya watu walioingia kituo cha kupigia kura wakiyapitisha kimagendo kwenda ndani sababu mawakala wa CHADEMA walikua washatimuliwa kwenye chumba cha kura muda mrefu sana na kutiwa kizuizini kwa maagizo toka kws dikteta uchwara.

Zama hizi sio kama miaka ya nyuma licha ya internet kuzimwa siku 5 watanzania walisimama upande wa haki na wachache waliendelea kutuhabarisha hata tuliokuwapo uhamishoni dunia nzima iliona ushindi batili wa mtutu wa dikteta uchawara ulivyotokea na serikali iliyokosa uhalali ilivyokuwa inaelekea kuitumbukiza nchi katika machafuko .

Nashukuru nilisimama katika haki nashangaa waliodhulumiwa walipokubali kujiunga na muovu mkuu ambaye japo hayupo ila kukosekana kwa uhalali wa serikali bado tunaona matokeo yake hata kwa zama hizi.
 
K

Kweli wewe una matatizo makubwa, Mimi na bar wapi na wapi? Unajuwa niliko? Unajuwa mkoa niliopo? Unajuwa wilaya niliyopo? Unanifahamu Mimi? Umewahi niona wapi? Unazani wote Ni walevi wa kushinda bar Kama wewe? Acha kuongea ongea vitu kwa kubahatisha bahatisha tu mradi uonekane umeandika na wewe
Uchawa wa kugombanisha mama na wapinzani Achaa,hizo zilikuwa zama zenu na magu nendeni mkalime hatuwateui ngooo kwa kusifusifu .
Mama hataki kusifiwa anataka umpe ushauri chanya kupeleka nchi ,shaur kuhusu vyanzo bora vya mapato,shauri miradi yenye tija ,leta masuruhisho ,ukishaona kijana mara ajiite mzalendo sijui kada ni wale dizaini ya sabaya na makonda .
 
Back
Top Bottom