Wana CCM Tuwe na desturi ya kupitia post (Nyuzi) humu JamiiForums na kuzijibu kwa hoja

Wana CCM Tuwe na desturi ya kupitia post (Nyuzi) humu JamiiForums na kuzijibu kwa hoja

Mtajibu kwa matusi, dharau na kejeli? Au mtajibu hoja kwa hoja?
Je, hayo majibu mtapewa na nani ikiwa viongozi wenu tu hawana??
Hatuta jibu kwa matusi Wala kejeli tutajibu kwa kuwaambia watu ukweli kwasabu mambo ambayo Chama Cha Mapinduzi imeshafanya yanaonekana Ni swala la kuwambia tu wananch. kwa mfano ujenz wa daraja la busisi si hata ww unaona, ujenz wa reli ya kisasa si hata ww unaona watu wamepata ajira..etc
 
Hiki chama bado kinaishi katka ujima utazani wapo dunia Yao neno maendeleo wao Ni kuleta maji na kujenga zahanati

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Hahahaha Magufuli wa kuwapitisha bila kupingwa hayupo tena enyi wana CCM. Demokrasia ndio hofu yenu kubwa sasa naona shindano imeanza kupenya vizuri. Na bado!
Hapana wananchi ndo wanaotupa Kura hatupiti kwa mgongo wa mtu, WANANCHI hufanya tathimin na kuona ccm ndicho chama Cha kuwapa maendeleo...daima tutachagua kazi
 
Tutajie mtu mmoja aliye pewa adhabu kali usemayo kwa sababu ya wizi wa pesa

Muongo mkubwa wewe
Danganya wajinga wajinga huko
Wale wajumbe wa bodi ya reli na bado bunge litaanza kujadili
 
Sisi ni wageni nchi hii? Posho inaendaje kujenga zahanati? Kwa bajeti gani?
Hiyo posho lazima itakuwa na miongozo kuwa yupi atastahili posho na yupi hata stahili posho kwa kazi ipi na kazi ipi haitahitaji posho..kwa mfano upimaji wa ardhi na uwekaji wa bicon etc
 
Upinzani upi?
Husika na kichwa Cha habari hapo juu....sisi makada wa Chama Cha Mapinduzi, uzarendo wetu kwenye chama chetu Ni kujibu hoja za wapinzani na kuujuza Umma wa Watanzania juu ya Mambo ambayo yamefanywa/Yanafanywa na chama chetu Cha CCM. Tujivunie uwazi uliopo ndani ya chama chetu Cha CCM na mafanikio tuliyoyafikia, Kuna vyama toka 1992 mpaka Leo vimekuwa vikipokea fedha kutoka kwa wafadhri, Ruzuku na kuchangisha watu michango lakini bado Kuna giza nene juu ya matumizi ya fedha hzo wengine hata ofs hawana, kwahyo sisi Kama makada na walinzi wa Chama Cha Mapinduzi lazima tuwatahadharishe wananchi wasiingie mkenge tunashukru kuona umma unajua tayari, hz barabara, disp. Hosp za rufaa kila mkoa, CT scan kila mkoa, madaraja, Elimu bure, mikopo vyuo vikuu, vivuko, nk. Ni sera ya Chama Cha Mapinduzi.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Hiki chama bado kinaishi katka ujima utazani wapo dunia Yao neno maendeleo wao Ni kuleta maji na kujenga zahanati

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Bora hata hayo maendeleo tunayaona na yamesaidia Sana kuongeza life expectancy ya Watu...mkuu Kuna vyama vinamiliki magari tu hakuna chamaana chochote wanachomiliki hawana legacy yyte Ile. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Gusia chama chetu kilivyo shughulikia report ya CAG
Kila mtu atashugulikiwa kwa nafasi yake na haki itatendeka bila kumuonea mtu hyo ndo Raha ya chama chenye haki na usawa...mpaka wa confirm makosa ya mtu naye aone ni kweli ndipo Sheria inachukua mkondo wake
 
Husika na kichwa Cha habari hapo juu....sisi makada wa Chama Cha Mapinduzi, uzarendo wetu kwenye chama chetu Ni kujibu hoja za wapinzani na kuujuza Umma wa Watanzania juu ya Mambo ambayo yamefanywa/Yanafanywa na chama chetu Cha CCM. Tujivunie uwazi uliopo ndani ya chama chetu Cha CCM na mafanikio tuliyoyafikia, Kuna vyama toka 1992 mpaka Leo vimekuwa vikipokea fedha kutoka kwa wafadhri, Ruzuku na kuchangisha watu michango lakini bado Kuna giza nene juu ya matumizi ya fedha hzo wengine hata ofs hawana, kwahyo sisi Kama makada na walinzi wa Chama Cha Mapinduzi lazima tuwatahadharishe wananchi wasiingie mkenge tunashukru kuona umma unajua tayari, hz barabara, disp. Hosp za rufaa kila mkoa, CT scan kila mkoa, madaraja, Elimu bure, mikopo vyuo vikuu, vivuko, nk. Ni sera ya Chama Cha Mapinduzi.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Nilipoona umeandika "uzarendo" badala ya uzalendo nimeku identify mara moja wewe ni nani!
Ni walewale tuu!
Haya mjibu hoja welcome to the show!
 
Nilipoona umeandika "uzarendo" badala ya uzalendo nimeku identify mara moja wewe ni nani!
Ni walewale tuu!
Haya mjibu hoja welcome to the show!
Hiyo ni writing error tu mkuu. Ok thank you
 
Ila hii kesi ukimsikiliza mdee Kuna kitu pale na viongozi wake wa chama anyway ngoja tuwe na subra
Ndio maana hiyo kesi imechukua muda mrefu kisa kuna kitu na viongozi wake? Kwahiyo unataka uje na wanaccm wenzako humu kisha utetezi wako ndio huu wa kiwango cha chini hivi?!
 
Ndio maana hiyo kesi imechukua muda mrefu kisa kuna kitu na viongozi wake? Kwahiyo unataka uje na wanaccm wenzako humu kisha utetezi wako ndio huu wa kiwango cha chini hivi?!
Hapana hapo nimegusia kidogo tu tuiachie mahakama
 
Hapana hapo nimegusia kidogo tu tuiachie mahakama
Muda ni jambo la muhimu, kama ya urais hapo Kenya imeisha, nini kinaendelea kwenye hizi mahakama zenye uwezo duni hapa kwetu? Si bure wawekezaji wanatumia mahakama za nje maana wanajua upuuzi ulioko hapa. Halafu ww ndio unasema uchaguzi ukiharibiwa wapinzani waende mahakamani!
 
Hiyo ni writing error tu mkuu. Ok thank you
Ilipo R na L ni mbali sana. Usijali lakini, twende kazi.
Ila kukuondolea aibu ya kutoa majibu irrelevant katika hoja utakazo jibu nikukumbushe kupitia vidokezo vyako kuwa ruzuku uliyotaja na kujenga maofisi sidhani kama unajua malengo ya hizo ruzuku zitolewazo kwa vyama vya siasa.
Na mengi tuu uko wrong
 
Back
Top Bottom