Wana CCM wapewe nafasi ya kuwania kiti cha Urais kisha Kura zipigwe. Kile kilichofanyika ni dhulma

Wana CCM wapewe nafasi ya kuwania kiti cha Urais kisha Kura zipigwe. Kile kilichofanyika ni dhulma

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo Salama!

Wapo watu walitaka na wanatamani kuwa sehemu ya watakaotumia Haki Yao ya kikatiba kuwania Tiketi ya Urais kwa Njia ya CCM. Hata kama Wana CCM hao ni wawili au Mmoja. Wanahaki ya kufanya hivyo.

Watu wote waungwana, watu wote wenye AKILI, watu wote wenye kupenda haki, watu wote wenye kuzingatia utu na heshima ya Uongozi tunajua kuwa kiongozi Bora na sahihi lazima apatikane kwa kuruhusu Demokrasia ya kweli. Kisha Yule atakayechaguliwa na wengi kwa Haki na Wala sio kwa vitisho, Rushwa na kuhongwa. Huyo ndiye kiongozi Bora.

Kiongozi hata angekuwa Malaika na alete maendeleo ya ajabu katika jamii yake. Kama hatokani kwa HAKI na KWELI kiongozi huyo hawezi kuwa kiongozi wa maana au kiongozi Bora.

Ubora WA mtu au kitu upo katika Uhuru wa Mtu kukichagua kitu hicho.

Kwenye Uundaji wa familia,
Mwanaume hata awe na sifa zipi za maana Sana lakini hawezi kuwa Mume Bora kwa Mwanamke ambaye hakumchagua. Hii ni kusema uchaguzi na Uhuru wa watu kujiamulia mambo Yao ni Moja ya nyenzo kuu katika maisha ya Mtu.

CCM kama chama kikuu cha siasa kinapaswa kiwe Mwalimu mzuri kwa vyama vidogo ili kujenga siasa Bora katika taifa letu.

Upatikanaji wa viongozi wa juu ambao baadaye huwa viongozi wa kiserikali ili uwe na Tija na manufaa katika nchi lazima upitie Haki katika kulinda maamuzi ya wengi kwenye chama.

Moja ya Mbinu za Kupata viongozi waliochaguliwa na wengi ni kupitia uchaguzi Huru na wahaki.
Kutoa Fursa Sawa kwa watu wote wanaotaka kuwania nafasi za uongozi.

Kura ziwe za karatasi na ziwe kwa Siri.

CCM inawakosea baadhi ya wanachama.
CCM haijali Haki za baadhi ya wanachama wanaotaka kuwania nafasi hizo.
Haijali maumivu Yao. Jambo ambalo sio sahihi Kabisa.

Nafikiri uchaguzi wa CHADEMA utatoa fundisho kwa vyama vingine kukubali mambo hata kama ni magumu.
Kukubali hukubalikina kuwaachia wanaokubalika.
Kukubali sauti ya wengi ni heshima kubwa ndani ya nchi.

Mueleko mpya 2025 -2030
 
Back
Top Bottom