Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Mnajua jinsi awamu ya 5 "ilivyofanikiwa" kwa kutumia propaganda pekee. Leo hii Magufuli angekataliwa kugombea CCM sio ajabu angejiunga CHADEMA na kutimiza ndoto yake. Siasa ndivyo zilivyo, tuwe tayari kwa lolote hata kama ni "kubadilisha gia angani" kama inatusaidia sawa. Magufuli ametumia kila njia kuua Upinzani kama mnavyojua, sisi tukijifanya ooh kwanini Nyalandu, kwanini Membe, Mbowe, etc tutaishia kugawanyika na kuwa dhaifu.

Tuwe na lengo MOJA, kushinda uchaguzi kwa njia yoyote ile inayokubalika na inayofanya kazi. Wana CHADEMA jueni kwamba CCM wanafuatilia mienendo yote na wanaogopa sana maamuzi ya CHADEMA. Itakuwa vibaya sana kama tutaruhusu kugawanyika kutokana na maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA. Tusimamie malengo yetu makubwa ambayo ni kuitoa CCM madarakani. Magufuli amekuwa na madhaifu mengi sana kuliko rais mwingine yeyote Tanzania ila CCM wameamua kumbeba kuliko kuanza kuzungumzia madhaifu yake, CHADEMA tunapaswa kuwa hivyo wakati huu muhimu.
 
Hatuwezi kuendelea kupokea kizazi cha shetani na kukipa nafasi ya kutuongoza.

Chadema tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu kwanini turuhusu kizazi cha shetani ccm kuwa sehemu ya harakati zetu zinazoongozwa na Mungu?

Tuache njia za mkato
Kumbuka wanachama wengi sana CHADEMA wametoka CCM. Waliozaliwa CHADEMA ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CHADEMA sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.
 
Chadema kama chama kikuu cha upinzani kimeshakomaa, huu ni wakati wao kuwa na mgombea wao, wapime uungwaji mkono watakaoupata toka kwa wananchi, waijue nguvu yao.

Hili suala la kuchukua watu toka CCM waje kupewa nafasi ya kugombea Chadema linatakiwa kufa, likiendekezwa litajenga tabia, halafu litashusha hadhi ya chama.
 
Kumbuka wanachama wengi sana CDM wametoka CCM. Waliozaliwa CDM ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CDM sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.
Sawa, lakini Chadema pia ina watu wake nao wanastahili hizo nafasi, hao wanaokimbia CCM wanatakiwa kuwa wavumilivu huko walipo wasubiri zamu yao, kama ni kuja Chadema waje, lakini wasipewe nafasi za juu, hilo lifahamike mapema.
 
fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako.

Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka CCM, bora tusimamishe jiwe.

Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
 
Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa ccm ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
Mnajua kuwa jiwe hafai kuwa rais laikin wana ccm hawaangalii hilo la sivyo wasingemsimamisha. Kuweni werevu.
 
Kumbuka wanachama wengi sana CDM wametoka CCM. Waliozaliwa CDM ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CDM sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.

Tunashukuru kwa haya maelezo mazuri, lakini mgombea urais wa upinzani toka ccm kwa sasa hapana. Tuko tayari kuongozwa na ccm bila ridhaa yetu, lakini sio kuokoteza watu wa ccm ndio waje watuongoze. Huyo mzee yuko huko porini anaagiza eti wapinzani waungane yeye ndiye aje agombee urais. Yaani kabaki anaagiza kama yuko hotelini, wali kuku, wali ng'ombe, ugali mchicha, maanina zake.
 
Mnajua kuwa jiwe hafai kuwa rais laikin wana ccm hawaangalii hilo la sivyo wasingemsimamisha. Kuweni werevu.

Suala la kuwa jiwe hafai kukaa madarakani hilo halina mjadala. Lakini hatuko tayari tena kutumia hizo takataka toka ccm kuitoa ccm. Wazee kama mmekula hela ya hilo jizee mrudishieni.

Huyo mzee muacheni abaki na hela zake akazitumie kupambana na kisukari, na sio kujifanya anaweza kuongoza wapinzani kuitoa CCM. Kama hao CCM wameweza kumkata kwenye kikao cha watu watano, na hamna alilofanya, atawezaje kuja kuwatoa sehemu walipo na backup ya tume ya uchaguzi na vyombo vya dola?
 
Tunashukuru kwa haya maelezo mazuri, lakini mgombea urais wa upinzani toka ccm kwa sasa hapana. Tuko tayari kuongozwa na ccm bila ridhaa yetu, lakini sio kuokoteza watu wa ccm ndio waje watuongoze. Huyo mzee yuko huko porini anaagiza eti wapinzani waungane yeye ndiye aje agombee urais. Yaani kabaki anaagiza kama yuko hotelini, wali kuku, wali ng'ombe, ugali mchicha, maanina zake.
Hiyo kauli yake ilikua imejaa kinyaa sana
 
CHADEMA kitakuja kuchukua URAIS mwaka 2045 kwa Kura za waliozaliwa kuanzia Early 2000's ambao watakuwa wanaula msoto wa Uchumi wa Kati.
 
Suala la kuwa jiwe hafai kukaa madarakani hilo halina mjadala. Lakini hatuko tayari tena kutumia hizo takataka toka ccm kuitoa ccm. Wazee kama mmekula hela ya hilo jizee mrudishieni. Huyo mzee muacheni abaki na hela zake akazitumie kupambana na kisukari, na sio kujifanya anaweza kuongoza wapinzani kuitoa ccm. Kama hao ccm wameweza kumkata kwenye kikao cha watu watano, na hamna alilofanya, atawezaje kuja kuwatoa sehemu walipo na backup ya tume ya uchaguzi na vyombo vya dola?
Mimi nafikiri kama takataka inaweza kutusaidia tuwaondoe ccm madarakani basi tutumie takataka hizo. Unajua vyema takataka waliyonayo ccm na jinsi inavyowasaidia. Unajua jinsi jeshi la polisi na vyombo vingine vinavyosaidia ccm kuwa madarakani. Ccm wanatumia kila njia tusisubiri eti watumie njia safi. In fact wanatumia njia mbovu kuua upinzani ndizo zinazofanya kazi kwao. Siasa ndivyo zilivyo. Tuwe werevu.
 
Nasema hivi, kama Membe kakatwa na watu watano hapo Dodoma, na hamna lolote kafanya, ndio atawaweza ccm wakiwa na mbeleko ya vyombo vya dola? Huyo Membe akawaunganishe wapinzani kama akina APPT MAENDELEO, TADEA, jahazi Asilia, UDP nk ili agombee urais kuwatoa ccm fullstop.
 
Wewe ninekushtukia sio mpinzani na hujawahi kuwa upinzani. Kwa wakati huu Membe anatosha kabisa kupeperusha bendera ya chadema na tutashinda
#makamanda twendeni na jasusi membe 2020#
fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
 
Huyo jamaa sio mpinzani na hayupo chadema, mtu mwenye akili timamu huwezi kukataa kumtumia mtu kama Membe jasusi mbobezi kutuvusha

Back
Top Bottom