Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Wanachama wengi wa CDM wameibuka kuanzia 2005 upto 2015 idadi kubwa ya hawa ni vijana au age profile yao ni 20 upto 40+yrs hawa siyo wahamiaji kutoka ccm wengi walikuwa undecided members kutoka kwenye jamii au waliokuwa vyama vya upinzani vingine.Kumbuka wanachama wengi sana CDM wametoka CCM. Waliozaliwa CDM ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CDM sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.
Wanachama wengi wa ccm wanaohama ccm kwenda upinzani wengi ni watafuta vyeo na madaraka na siyo waumini wa itikadi ya CHADEMA bali ni watafuta vyeo tu.
Hivyo basi hoja yako ya kuwa wanachama wengi wa CHADEMA walikuwa wanaccm ni hoja potofu na haijajengwa katika msingi sahihi wa kihoja.
Turudi kwenye mada hata kama wanachama wa CHADEMA wengi ni wahamiaji kutoka ccm (which is questionable) haimaanishi kwamba kila uchaguzi CHADEMA inapaswa kuokoteza mgombea kutoka ccm hii haikubaliki hata kidogo chama kina wanachama wengi sana wenye uwezo wa kuongoza nchi kuliko hata rais Magufuli ambaye ana record za ufisadi kwenye nyumba za serikali.