Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

Kumbuka wanachama wengi sana CDM wametoka CCM. Waliozaliwa CDM ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CDM sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.
Wanachama wengi wa CDM wameibuka kuanzia 2005 upto 2015 idadi kubwa ya hawa ni vijana au age profile yao ni 20 upto 40+yrs hawa siyo wahamiaji kutoka ccm wengi walikuwa undecided members kutoka kwenye jamii au waliokuwa vyama vya upinzani vingine.

Wanachama wengi wa ccm wanaohama ccm kwenda upinzani wengi ni watafuta vyeo na madaraka na siyo waumini wa itikadi ya CHADEMA bali ni watafuta vyeo tu.

Hivyo basi hoja yako ya kuwa wanachama wengi wa CHADEMA walikuwa wanaccm ni hoja potofu na haijajengwa katika msingi sahihi wa kihoja.

Turudi kwenye mada hata kama wanachama wa CHADEMA wengi ni wahamiaji kutoka ccm (which is questionable) haimaanishi kwamba kila uchaguzi CHADEMA inapaswa kuokoteza mgombea kutoka ccm hii haikubaliki hata kidogo chama kina wanachama wengi sana wenye uwezo wa kuongoza nchi kuliko hata rais Magufuli ambaye ana record za ufisadi kwenye nyumba za serikali.
 
Kila unachosema hapa ni completely opposite from the reality. CCM 2015 ilikuwa imekufa ila Magufuli kafufua chama, na kasi aliyokuwa nayo chama sasa ni imara ila wabaya wake wengi wapo ndani ya chama kwani ule ulaji, madili hamna tena! Ubinafsi
ulizika vyama vya upinzani November 2015 na hatutegemei uhai kurudi tena upinza. Upinzani sasa hauna ‘base’! Yaliyokuwa yanafanywa na Edward Moringe Sokoine na Mwl Nyerere sasa yanatekelezwa.
Ubinafsi kamwe sio sababu ya upinzani kudhoofika. Kama kuna ubinafsi uliopaswa kuoneshwa katika chama chochote basi ni ubinafsi wa Magufuli? Kila kitu kinajulikana kuanzia kuiita serikali ni ya magu, mimi..., mimi....nita...hadi wanaccm walifikiri ccm ni mali ya magu. Hakuruhusu mtu yeyote asimame nae kwenye uchaguzi huu, huu ni ubinafsi mkubwa mno. Ila unajua kwanini CCM haidhoofishwi na ubinafsi na hata udikteta wa magu?

Alichofanya magu ni kutumia udikteta kuwaadabisha watu ndani ya ccm ndio maana kila mtu ccm anamsifia kwa LAZIMA na ole wako usifanye hivyo. Kudhoofishwa kwa upinzani kumefanywa na magu kwa makusudi kabisa.
 
Wanachama wengi wa CDM wameibuka kuanzia 2005 upto 2015 idadi kubwa ya hawa ni vijana au age profile yao ni 20 upto 40+yrs hawa siyo wahamiaji kutoka ccm wengi walikuwa undecided members kutoka kwenye jamii au waliokuwa vyama vya upinzani vingine.

Wanachama wengi wa ccm wanaohama ccm kwenda upinzani wengi ni watafuta vyeo na madaraka na siyo waumini wa itikadi ya CHADEMA bali ni watafuta vyeo tu.

Hivyo basi hoja yako ya kuwa wanachama wengi wa CHADEMA walikuwa wanaccm ni hoja potofu na haijajengwa katika msingi sahihi wa kihoja.

Turudi kwenye mada hata kama wanachama wa CHADEMA wengi ni wahamiaji kutoka ccm (which is questionable) haimaanishi kwamba kila uchaguzi CHADEMA inapaswa kuokoteza mgombea kutoka ccm hii haikubaliki hata kidogo chama kina wanachama wengi sana wenye uwezo wa kuongoza nchi kuliko hata rais Magufuli ambaye ana record za ufisadi kwenye nyumba za serikali.
Nakuelewa, ila unaelewa kwanini magu pamoja na rekodi ya ufisadi anaonekana ndio anafaa sana. Unafikiri wana ccm wameangalia hilo wakati wakimchagua? Nawafundisha siasa hapa manake wengi wenu bado hamuelewi.
 
mkuu tindo najua itakuuma sana ila huna jinsi, siasa ni mchezo mchafu sana, upepo unabadilika ghafla, usione ajabu kwa Membe kugombea, watu wanaangalia namba atakazozileta, ndo maana wanageuka ghafla na kusahau kile walichokuwa wanakipigania.
fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
 
ccm record za ufisadi haziwezi kuwa kigezo cha kumuondolea sifa mgombea wao kwa sababu ufisadi ni mfumo rasmi wa maisha ya wanaccm wote hasa watawala.

Pili kuhusu suala la kufaa kwao 2015 lilikuwa na sababu nyingi ikiwemo kanda anayotoka ilikuwa na voters wengi hivyo ulikuwa mtaji pekee wa kuibakiza ccm madarakani.

Tatu kuteuliwa Kwake ilikuwa na nia ya kuvunja makundi ya chama yaliyosababishwa na mchakato wa uchaguzi.

Kufaa kwake kwa sasa kuna sababu zingine tofauti na za uchaguzi uliopita.
1 ccm haina utamaduni wa kumpinga rais aliyeko madarakani kumalizia awamu yake ya pili haijalishi anafaa au hafai kwa wananchi.
2 Magufuli kaifanya ccm ipumue kuzuia vyama vingine viisifanye siasa ibaki ccm pekee anayofanya siasa sababu kubwa ikiwa ccm wamechoka kufanya siasa zaidi ya kutegemea msaada wa vyombo vya dola hili hatuhitaji degree kulijua.

NB
Halafu unapojenga hoja na kusema kuwa wengi wetu hatuelewi, hatuelewi nini na umetumia muktadha gani kupima uelewa wetu ?

Wewe ndiye unayeelewa peke yako ?
 
Membe hawezi akaleta namba zozote upinzani zaidi ya kuja kuharibu mwelekeo wa vyama vya upinzani.
 
inawezekana wameona anaweza akaleta wabunge wengi kuliko watia nia wengine mkuu

Soma vizuri,nimesema wengi wenu, unaweza kuwepo ama la na sijasema mimi peke yangu ndio naelewa.
 
fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
Mkuu uko sahihi kabisa. Kwa maoni yangu wale wote waliotimka/watakaotimka ccm na kuja Chadema wapokelewe. Lakini waje kwa lengo la kuihujumu ccm na si kuja kuomba kuteuliwa kwenda kupambania nafasi walizozikosa huko ccm.
 
Soma vizuri,nimesema wengi wenu, unaweza kuwepo ama la na sijasema mimi peke yangu ndio naelewa.
Unatumia muktadha gani kusema wengi wao hawaelewi ?

Kama unajitoa wewe kwenye kuelewa nani sasa anaelewa tofauti na wale uliowaita "wengi wenu"??
 
Membe hawezi akaleta namba zozote upinzani zaidi ya kuja kuharibu mwelekeo wa vyama vya upinzani.
Wana CDM mnapaswa kuwa kitu kimoja na kuamua kukubaliana la sivyo mtasambaratishwa. Kinachowashikamanisha ccm ni hofu ya kukosa keki (madaraka), lakini hofu hiyo haipo kwa CDM sana. Hivyo inabidi watu wawe na upeo mkubwa sana kuwa na umoja kwa ajili ya Chama. CCM itasambaratika kama nyumba mbovu siku wakipoteza madaraka, lakini kwa sasa hofu ya kukosa keki ndio inayowapa discipline.
 
mkuu tindo najua itakuuma sana ila huna jinsi, siasa ni mchezo mchafu sana, upepo unabadilika ghafla, usione ajabu kwa Membe kugombea, watu wanaangalia namba atakazozileta, ndo maana wanageuka ghafla na kusahau kile walichokuwa wanakipigania.

Safari hii watajua sisi wafuasi ndio nguvu yao, na sio maamuzi yao.
 
Unatumia muktadha gani kusema wengi wao hawaelewi ?

Kama unajitoa wewe kwenye kuelewa nani sasa anaelewa tofauti na wale uliowaita "wengi wenu"??
Kama unaelewa jambo basi wewe usiseme tena, "watanzania wengi hatujui uchumi wa kati maana yake nini...", unasema "watanzania wengi hawajui/hamjui..." unless unataka kuwa too polite.
 
fazili,

Hatuwezi kuendelea kupokea kizazi cha shetani na kukipa nafasi ya kutuongoza.

Chadema tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu kwanini turuhusu kizazi cha shetani CCM kuwa sehemu ya harakati zetu zinazoongozwa na Mungu?

Tuache njia za mkato
MUNGU yupi? Mngekuwa na MUNGU msingekifanya chama kuwa danguro nyie ni kizazi cha nyoka hamna MUNGU

fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
Kumbe wakati mwingine unakuwaga na mawazo mazuri namna hii, unakwamaga wapi mkuu mana kuna wakitu huwa unashangaza!
 
Back
Top Bottom