Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

Ubarikiwe sana kwa ushauri mzuri
Kumbuka wanachama wengi sana CDM wametoka CCM. Waliozaliwa CDM ni wachache na ndivyo siasa zilivyo. Uingereza wanabadilisha vyama kila miaka 4 au 8 unafikiri kuna wanachama wapya au ni wale wale wa upande mmoja wanaamua kusapoti upande mwingine? Tuwe flexible itatusaidia CDM sio dhehebu ni uwanja wa demokrasia.
 
Nakuunga mkono hao mapandikizi hawatakiwi ndani ya chama
Chadema kama chama kikuu cha upinzani kimeshakomaa, huu ni wakati wao kuwa na mgombea wao, wapime uungwaji mkono watakaoupata toka kwa wananchi, waijue nguvu yao.

Hili suala la kuchukua watu toka CCM waje kupewa nafasi ya kugombea Chadema linatakiwa kufa, likiendekezwa litajenga tabia, halafu litashusha hadhi ya chama.
 
Cdm this time hakuna mtu wa kuwapa red carpet hao wahamiaji. Wasubiri tuwaamini kwanza
fazili,

Weka ujumbe wako vizuri ni nini unataka kusema. Lakini kama unataka Membe au Nyalandu, ndio wawe wagombea wa urais wa upinzani, wala usipoteze muda wako. Hao viongozi wa chama tuliwaamini 2015 wakatuletea tapeli, saa hii naona wanaanza kuwa chenga chenga kurudia yale ya 2015. Kama hakuna wagombea wa urais nje ya hizo taka ngumu toka ccm, bora tusimamishe jiwe. Kama mmechukua hela kutetea hao wahuni wa CCM ili wagombee kupitia upinzani, tunawasihi mzirudishe.
 
Hakuna kuitafuta kibra? [emoji23][emoji23][emoji23]
Yeyote atakayepewa shoka ni sawa; kazi ni moja tu kuliondoa shingo la CCM na safari hii tumekubaliana hakuna kuligeuza, huko huko lilikotazamia!!
 
Lengo la chadema ni kuchukua nchi kutoka kwenye makucha ya ccm, hivyo kwa njia yoyote iwezayo kutumika kuiondoa ccm ni muhimu ili mradi iwe inakubalika kwa jamii ya wastaarabu wa kisiasa.
Lakini hatutaki tena kutumia kizazi cha shetani kuingia madarakani
 
Mnajua jinsi awamu ya 5 "ilivyofanikiwa" kwa kutumia propaganda pekee. Leo hii Magufuli angekataliwa kugombea CCM sio ajabu angejiunga CHADEMA na kutimiza ndoto yake. Siasa ndivyo zilivyo, tuwe tayari kwa lolote hata kama ni "kubadilisha gia angani" kama inatusaidia sawa. Magufuli ametumia kila njia kuua Upinzani kama mnavyojua, sisi tukijifanya ooh kwanini Nyalandu, kwanini Membe, Mbowe, etc tutaishia kugawanyika na kuwa dhaifu.

Tuwe na lengo MOJA, kushinda uchaguzi kwa njia yoyote ile inayokubalika na inayofanya kazi. Wana CHADEMA jueni kwamba CCM wanafuatilia mienendo yote na wanaogopa sana maamuzi ya CHADEMA. Itakuwa vibaya sana kama tutaruhusu kugawanyika kutokana na maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA. Tusimamie malengo yetu makubwa ambayo ni kuitoa CCM madarakani. Magufuli amekuwa na madhaifu mengi sana kuliko rais mwingine yeyote Tanzania ila CCM wameamua kumbeba kuliko kuanza kuzungumzia madhaifu yake, CHADEMA tunapaswa kuwa hivyo wakati huu muhimu.
Silaha yeyote hapo itakayotumika kumbutua CCM sie tunaunga Mkono ,GIA ya ANgani ndio Nzuri kama ile ya ENL iliyomchakaza JIWE 2015 mpaka leo JIWE hataki kusikia UKAWA na wala KUMSIKIA MEMBE maana ni THREAT kwake.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)kinafanyaga vikao vyake popote pale,iwe jf,fb,insta sawa tu.maana mitaani chama hakipo kimebaki kwenye mitandano tu.
 
Back
Top Bottom