Wana habari wengi wa media za Bongo ni mashabiki wa Simba wamejaa fitina

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Mafanikio ya Yanga Mwaka huu hasa katika mashindano ya kimataifa yamedhihirisha jinsi wana habari wengi walivyo mashabiki wa Simba hadi wanashindwa kuficha hisia zao, chuki na wivu kwa mafanikio ya Yanga.

Wamekuwa wakijificha kwa kile wanachokiita uchambuzi lakini ukifuatilia chambuzi zao unagundua zimejaa wivu na chuki tu. Bahati nzuri Mungu amekuwa akiwaumbua sana. Kuna chambuzi nyingine unaona zimebeba matamanio yao. Yaani wanafanya media propaganda zenye lengo la kuwakatisha tamaa wachezaji wa Yanga na Mashabiki wake, unakuta muandishi anaonyesha kuwa hakuna uwezekano wa Yanga kuifunga Rivers utd, Marumo au USM Alger. Halafu ikitokea Yanga kuifunga Rivers utd au Marumo wanarudi na kusema Yanga imekutana na timu dhaifu sana msimu huu.

Leo nimepitia uchambuzi wa jamaa wa Clouds anaitwa EDGAR KIBWANA kuwa Yanga hawezi kuifunga USM Alger, yaani ukisoma uchambuzi wake unagundua una lengo la kuwakatisha tamaa Yanga na pia uchambuzi umebeba matamanio yake.

Wachambuzi aina ya Kibwana, Edo kumwembe na Jemedari ikitokea nchi kuingia vitani wanatakiwa kufichwa maana ni propagandist wanamnufaisha adui. Nadhani mliozaliwa zamani mtakumbuka miaka ile ya 70s issue ya mtangazaji wetu mmoja alijisahau sana hadi ikabidi apishe....
 
Wachambuzi uchwara waliotamani Yanga isisonge:

1. Wilson Oruma
2. Geof Leah - EFM/TVE
3. Jemedari Said - EFM
4........Tindwa-clouds
5 Edo Kumwembe
6. Edgar Kibwana- Clouds.

Walioumia zaidi Yanga kufika Fainali
1. Karia
2. Ahmed Ali

Walioaibika zaidi yanga kufika Fainali
1. Fei Toto

Vipaji vya ukweli fani ya habari
1 . Ally Kamwe
2. Haji Manara- nje ya uwanja but
Never give up

Wazalendo wa Kweli
1. Mama yetu Samia
2. PM - Majaliwa
3. MO - Dewji
4. Salim Kikeke

Kiongozi wa Mfano
1. Eng. Haris

Wa kupewa Maua
1. Mama yetu
2. Nasrin Nabi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…