Kaka kaka nakushauri huyo aliyezaa achana naye kabisa ndugu yangu utafulia. Kulea mtoto wa mtu mwingine ni usumbufu mkubwa. Siku nyingine huyo baba yake atakuja kwako eti anakuja kumwona mwanae. Na mtoto akikua akikujua kwa babake haishi kiguu na njia kwenda huko kusimulia yako. Ukimrudi kakukosea, atasema kwa kuwa si babake. Likimtokea lolote baya atasema ningekuwa naishi na babangu isingekuwa hivi, shauri ya baba wa kambo. Na hata ukimfanyia mema vipi akafanikiwa, bado atarudi kumuenzi baba mzazi wakati wewe ndiye uliyelea.
Na ikiwa mtoto huyo kabaki kwa babake nawe ukachukua mke, hiyo ni balaa zaidi. Mke ni kila mara kiguu na njia kwa mzazi mwenzie kumwona mwanae. Na nakwambia watazaliwa wengine hapo home kwako na huyo bwana!
Kwa nini ujiingize kwenye usumbufu wote huo na wakati wasichana fresh kabisa wapo hawajazaa, wamejitunza kwa adabu na heshima wanasubiri mume? Huoni kuoa hiyo nung'aembe ni kama promotion kuwa hata wao wanafaa kuolewa kumbe hawafai?
Labda kama na wewe una mtoto bila ndoa, basi oa huyo mtaendana, na kila mtu atamvumilia mtoto wa mwenzie. Lakini kama na wewe hujazaa, usijiharibie heshima yako, achana na hilo nung'aembe.