LGE2024 Wana JF mmejiandikisha? hizi ni faida za kujiandikisha kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hizo faida unazodai kupatikana kimsingi hazipo kwa sababu mshindi hapatikani kutokana na kura unayopiga bali msimamizi wa uchaguzi atatangaza mshindi kutokana na matakwa ya CCM,usifikiri watu ni wajinga ndiyo maana hawataki kwenda kujiandikisha kwa sababu hakuna uchaguzi bali uchafuzi.
 
Hapana mkuu... hakuna kitu kama hicho.... kiongozi anatokana na majority decision

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hakuna faida hata moja hapo
 
Ebu angalia hii idadi ya kura zilizochagua rais;
Rais B.W.MKAPA 4,026,422
Rais J.M.Kikwete 5,276,827,
Rais J.P.Magufuri 12,516,252

Swali: Je una pata picha gani?
usisahau idadi ya Watanzania ni zaidi ya milion 55.
Na idadi ya wapiga kura ni zaidi ya milion 20.

Jibu: 1.WATU HAWANA IMANI NA SIASA ZA CHAMA.
2.HATA WAKIJIANDISHA NA KUPIGA KURA KIASI GANI, CHAMA KINAPANGA MATOKEO.
 
Tusipoheshimu na kuthamini KURA ya mtu na MAAMUZI YAKE tutaendelea kuwa na wakati mgumu kuwapata wapiga kura.

Tutaendelea kukutana na madudu mengi yanayohitaji kutetewa kwa nguvu nyingi badala ya kazi ya mikono ua utendaji kujitanabahisha wenyewe.

Mwisho ni kila mmoja kubaki anamshangaa mwenzake tumefikaje hapa.
 

Hizi namba zina ujumbe mkubwa sana, ni wachache wanaweza kupata uhalisia wake na kuchukua hatua sitahiki. Wengine watabaki kusifu na kuabudu kwani wananufaika na hali hii.
 
Nimejiandikisha kama dk 30 zilizopita hapa Kashai sokoni Bukoba. Chakushangaza nimekuta mwandikishaji tu na jamaa mmoja ndio kanikaribisha nikaingia ndani. Nikaulizwa majina nikawambia naitwa Nsangalufu Tuntufye Mwasakafyuka. nikaambiwa saini nikasaini Sijaulizwa umetoka mtaa gani, uenyeji wangu nk. Nimejiuliza maswali mengi je? kwa staili hii si wataandikishwa mamluki kibao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…