Faida ya Mtanzania kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya kitongoji, mtaa, na kijiji ni pamoja na:
1. Kuchagua viongozi bora: Inatoa nafasi ya kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kushughulikia maslahi ya jamii.
2. Kuhakikisha uwakilishi wa wananchi: Kupitia kura, wananchi wanapata viongozi wanaowawakilisha kwenye maamuzi yanayogusa maisha yao moja kwa moja.
3. Kuimarisha demokrasia: Kushiriki kwenye uchaguzi ni sehemu ya kutekeleza haki yako ya kikatiba na kuimarisha demokrasia nchini.
Ndugu zangu, wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni huu. Hii ni nafasi yetu ya kuhakikisha tunapata viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya jamii zetu. Fanya uamuzi sahihi, jiandikishe leo ili ushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao
Mnasubiri nini???
Hizo faida unazozitaja zinafia njiani kama yai linapogeuka viza. Tungeziheshimu hizi sauti za watu ndo utapata zao tarajiwa unalolinena.
Nchi masikini kwa mujibu wa vyombo vya fedha:
1: Tume/taratibu mbilimbili za chaguzi ndani ya nchi moja. Tunahitaji hili kweli kama tunajitambua na kuijali nchi na watu wake? Tunashindwa kupata utaratibu wa kitaifa kupata viongozi kwa mfumo wa gharama halisi na kupeleka pesa kwenye shughuli nyingine za maendeleo ya jamii?
Kipi kina gharama kati ya kubadili sheria ili tume moja isimamie uchaguzi(ambayo ipo na inatumia fedha) dhidi ya tasisi nyingine ku-recruit watu wapya na kwa muda mfupi kufanya kitu kilekile kwa uzoefu na uimara nisioweza kuulinganisha na wa tume?
2: Una kitambulisho cha mpiga kura, umetumia fedha, mali nyinginezo na muda wa watu kujiandikisha. Hukitumii ipasavyo.
3: Una kitambulisho cha utaifa, umetumia fedha, mali nyinginezo na muda wa watu kujiandikisha. Hukitumii ipasavyo.
4: Unashindwa kutengeneza mfumo wa ku-capter wale tu waliofikia umri wa kupiga kura ili uwaongeze kwenye mfumo husika na kuutumia huo mfumo?
5: Kila uchaguzi unatumia muda wa watu kujiandikisha nchi nzima, kupanga foleni kwenye kujiandikisha na kupiga kura bado tunasema kuna watu tumewasomesha kuhusu teknolojia na tunaitumia kupunguza gharama za maisha. Pia tuna think tank ya Taifa?
6: Hii ilitakiwa kuwa ni long lasting data base, unaingiza wapya tu na unapiga kura kwa finger print. Ungerahisisha mchakato kwa gharama zisizojirudia. Kuna mambo mengi yanarudiwa rudiwa kwa msingi huo tusiseme hatuna hela. Ila tuwe tayari kwa matokeo yake kama tukiweka mfumo sawa kwani na uhalisia huongezeka.
7: Kama kusipokuwa na intermediate/vituo vya kati hapo kuchakachua, kila mtu angepata picha kulingana na alivyonawa uso au kulingana na poda aliyoweka usoni.
8: Tuachane na mambo ya ujima, tunaandikisha hata hakuna mfumo wa kuunganisha ku-verify unaemwandikisha kuwa mhusika mfumo wa NIDA unamtambua kama raia? Hata bank tu zinaweza kufanya kitu hiki, NHIF, NSSF nk. Je serikali kwenye jambo hili kama ni la muhimu inashindwa nini??