LGE2024 Wana JF mmejiandikisha? hizi ni faida za kujiandikisha kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Faida ya Mtanzania kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya kitongoji, mtaa, na kijiji ni pamoja na:

1. Kuchagua viongozi bora: Inatoa nafasi ya kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kushughulikia maslahi ya jamii.

2. Kuhakikisha uwakilishi wa wananchi: Kupitia kura, wananchi wanapata viongozi wanaowawakilisha kwenye maamuzi yanayogusa maisha yao moja kwa moja.

3. Kuimarisha demokrasia: Kushiriki kwenye uchaguzi ni sehemu ya kutekeleza haki yako ya kikatiba na kuimarisha demokrasia nchini.

Ndugu zangu, wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni huu. Hii ni nafasi yetu ya kuhakikisha tunapata viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya jamii zetu. Fanya uamuzi sahihi, jiandikishe leo ili ushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao

Mnasubiri nini???
Haudhani sisi kutojiandikisha kumekuwezesha wewe kupata faida kubwa! Yaani wewe unakuwa na wema wa kutaka kiwango chako cha faida kishuke! Haiwezekani kwani wabongo si wema kiasi hicho, endeleeni tu kugawana faida.
 
Ebu angalia hii idadi ya kura zilizochagua rais;
Rais B.W.MKAPA 4,026,422
Rais J.M.Kikwete 5,276,827,
Rais J.P.Magufuri 12,516,252

Swali: Je una pata picha gani?
usisahau idadi ya Watanzania ni zaidi ya milion 55.
Na idadi ya wapiga kura ni zaidi ya milion 20.

Jibu: 1.WATU HAWANA IMANI NA SIASA ZA CHAMA.
2.HATA WAKIJIANDISHA NA KUPIGA KURA KIASI GANI, CHAMA KINAPANGA MATOKEO.
Mmmmmh! Hiyo takwimu ndivyo ilivyo kweli au naota Mimi.
 
Faida ya Mtanzania kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya kitongoji, mtaa, na kijiji ni pamoja na:

1. Kuchagua viongozi bora: Inatoa nafasi ya kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kushughulikia maslahi ya jamii.

2. Kuhakikisha uwakilishi wa wananchi: Kupitia kura, wananchi wanapata viongozi wanaowawakilisha kwenye maamuzi yanayogusa maisha yao moja kwa moja.

3. Kuimarisha demokrasia: Kushiriki kwenye uchaguzi ni sehemu ya kutekeleza haki yako ya kikatiba na kuimarisha demokrasia nchini.

Ndugu zangu, wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni huu. Hii ni nafasi yetu ya kuhakikisha tunapata viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya jamii zetu. Fanya uamuzi sahihi, jiandikishe leo ili ushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao

Mnasubiri nini???
Nyumbu wakijiandikisha inatosha sana
 
Hizo faida unazodai kupatikana kimsingi hazipo kwa sababu mshindi hapatikani kutokana na kura unayopiga bali msimamizi wa uchaguzi atatangaza mshindi kutokana na matakwa ya CCM,usifikiri watu ni wajinga ndiyo maana hawataki kwenda kujiandikisha kwa sababu hakuna uchaguzi bali uchafuzi.
Inaweza ikawa kweli au sio kweli,ila kutokujiandikisha ni ushindi mara mbili kuliko huo unaoita "kuiba kura"
 
Kwa maoni yangu binafsi kwakuwa lengo lao ni kupata huo unaoita "ushindi" basi washinde tu wawe viongozi waitwe waheshimiwa kuliko mimi kunyanyua miguu yangu na kupigwa na jua kwenye foleni ya kujiandikisha na kupiga kura halafu hiyo kura ikawa haina maana yoyote.
 
Usiseme hivyo mkuu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom