Ushauri wangu kwa mtu anayeitwa mahali popote na mtu/watu asiowajua ajitahidi kwenda na watu wengine,atoe taarifa kwa ndugu zake,marafiki au jamaa zake kwamba nimeitwa mahali fulani kuondoa dhana ya kwamba niliitwa ila nikaogopa kwa kudhani kwamba nimeitwa na watu waovu,kumbe unatenda kosa la kukaidi kuitikia wito halali wa Polisi.
Kuna siku nilikuwa ninakatiza mtaani alfajiri sana,mara nikasikia ninaitwa "Oyaaa simama mahali hapo ulipo,Wapi saa hizi?" Nikimulikwa na tochi machoni,nikasimama nikidhani ni Polisi wako doria!!
Nakuja kushtuka nimezungukwa na watu wana mapanga, nondo halafu wamevaa vikaptula vifupi,vifua wazi wamejipaka oil mwili mzima,kumbe ni Vibaka.
Kilichonisaidia sikuogopa, nilijikuta ninasema ninaenda kazini nimewaacha masela wangu bado wamelala, wakadhani ninafanya kazi kama zao. Maana waliniuliza upo kundi gani,nikataja majina ya marafiki zangu,lakini wakawa wanashangaa, wanaangaliana tu.
Bahati nyingine nilikuwa nimevaa kawaida sana wakanithaminisha wakaona sina cha kupoteza. Wakaniacha.
Kwahiyo rafiki yako anaweza kuwa hahusiki ila hofu ya kuitwa Polisi ndio ilimfanya aogope kuitikia wito,kumbe njia aliyoitumia haikuwa sahihi.
Mungu amsaidie alimalize salama.
Kutunza nyaraka zenye taarifa zetu ni muhimu sana dunia imeshaharibika,mtu anaweza kuchukua tiketi, vocha iliyotumika, kitambulisho akakitupa sehemu lilipotendeka tukio la uhalifu ilimradi tu uitwe kusaidia upepelezi, mpaka ijulikane hukutenda kosa tayari umeshapoteza muda wako ambao ungeutumia kufanya jambo la msingi.