Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

pole sana na hongera kwa uthubutu
 
Kama kuna mwenye clip ya ndugu Pascal Mayalla akiwa anajinadi tunaomba atume humu, kwani alitukwaza wengi baada ya kuachana na uhalisia wake wa kwanza na kuanza kujipendekeza kwa CCM
 
pole sana ulitegemea miujiza na hukwenda kuombewa kanisani ,,,,,, never give up .....mkuu ulifikiri siasa ni kama mchezo wa mpira unavua suruali unavaa bukta unaanza kupiga mpira
 
Usijali. CV zimefika serikalini. Anza kuandaa suti. Utapewa nafasi nyingine kubwa! (WOTE TUSEME EIMEEEEN)
 
Aiseee zile mbwembwe za kwenda kumtoa mdeeee kawe nazo hoi illa napenda ujasir wako na uthubutu wako toka ulipouliza maswali mazur pale ikulu nakmbka ilkua 2016

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu pole mkiambiwa tz ni muhimu kujenga upinzani madhubuti mnakataa ,upinzani ni fulsa nyingine za kuwapatia uongozi kwa wale wenye uwezo na utashi wa kuwaongoza wananchi nje ya chama kilicho madarakani
 
Poleni sana mzee mwenzangu mimi nilienda kupima upepo pale vunjo kwa kuweka kambi zaidi ya mwezi mzima nimeamua kurudi mjini kuangalia fursa nyingine kwanza.

Ningekushauri ungeanza na Udiwani naona huko kungekufaa zaidi ili hizo milioni 10 zianze na kata yako.
Asante
 
Binafsi nakupa pole nikiamini kuwa unastahili kupata pole kwa kuwa ulidhamiria kuwa mbunge.

Kwann , umeshindwa kuongoza na hatimaye kuwa mgombea ubunge kupitia CCM?

Upinzani umedhoofika, upinzani ndiyo afya ya wagombea vijana kupata nafasi kupitia vyama vingine vya kisiasa.

Ni ngumu sana, kushinda kwa kupitia CCM ukiwa bado kijana mdogo tena ambaye hujalelewa ndani ya CCM.

Malezi ya vijana kuandaliwa kuwa viongozi bora Taifa limesahau ndo maana vijana wanaonekana Wana Tamaa za kiuongozi.


Kaka pole !! Jifunze kuchungulia KAWE ni ngumu ngumu sana.
 
hiyo ajenda ya kugawa hela ndio iliyomuangusha chini pwaaaa chini chali
 
Ni makosa makubwa watu woote kutaka kuwa CCM. Checks and balances Ni muhimu sana kwenye kila jambo
 
Watu wengi mliingia huko kwanza hamu kuwa na plan
Mmekurupuka, tamaa tu ya kutaka nafasi, wengi wenu mlipoamka tu haooo mnaokwenda kutangaza nia, Mwishowe mmepewa za chembe Pascal Mayalla

Ova
 
Pole. Kumbe, mkuu ulitanguliza ahadi ya rushwa. Hebu tupe uzoefu wako kwenye masuala ya rushwa kwenye huo mchakato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…