Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?

Moja ya hasara ya kitaifa, ni hawa wabunge 19 kulipwa posho/ mshahara kinyume na sheria.

Wote tunajua kwamba chama kilishawavua uwanachama.
Kama Dola haitaki wale COVID 19 wavuliwe ubunge wao, automatically hawewezi vuliwa ubunge huo,may be chadema wanajua ukweli ila wameamu kuwa safe side ili wasionekane wasaliti,Kwa nchi hii politics is our way to the destination of woe...
 
Ukisoma comments za wadau utaona kwamba zaidi ya asilimia 90 wanapinga ulichokiandika. Maana yake ni kwamba hoja zako hazina relevance yoyote, hivyo unatakiwa kubadilika. Watu si wajinga tena wa kulishwa propaganda zako.
Mkuu malantu , hao asilimia 90 wanaonipinga hawaijui katiba kikamilifu katiba ya Chadema!, bahati nzuri sana imetokea tuu mimi pia ni mwanasheria na somo nililopindua utadhani mtihani natunga mimi ni LW. 100, Katiba!.

Hii sii mara ya kwanza mimi kutofautiana na public opinion humu, hata kwenye issue hii Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma! tulitofautiana na wengi na nikasema Hivyo mimi sifuati formula ya wengi wape hata kama ni vilaza!. Nitasimama na ukweli na mwisho wa siku ukweli ndio husimama mpaka mwisho!.
P
 
Achana na hilo zee njaa akili zipo tumboni.
Mpka umri huo bado anawaza kupata kazi za kuteuliwa kwa kulamba watu makalio.
Ni aibu sana kwa taifa na shule walizo soma kuwa na watu wa namna hii.
 
Achana na hilo zee njaa akili zipo tumboni.
Mpka umri huo bado anawaza kupata kazi za kuteuliwa kwa kulamba watu makalio.
Ni aibu sana kwa taifa na shule walizo soma kuwa na watu wa namna hii.
Hapana hiyo lugha unayotumia siyo ya staha. Hata mimi ni mzee na hata wewe utakuwa mzee. Tunajadiliana na tunaweza kutofautiana na tukitofautiana tusianze kutoleana maneno ya kuudhi. Au wewe hukuwahi kushiriki mijadala/debate shule ya msingi au sekondari - kununua baiskeli ni bora kuliko kununua radio? Kwani watoa mada kwenye hii mijadala wakitofautiana (kama ulikuwa ukishiriki) walikuwa wakitoleana maneno ya kuudhi? Hapana! Mwisho wa debate walikuwa wakishikana mikono. Ndivyo inavyotakiwa kwa watu wanaojadiliana. Tumia lugha nzuri na utaeleweka tu. By the way, hata mimi ni mzee na bado natafuta ajira ili familia ile maana sitaki niwe ombaomba. Kama una mihela ya kusaidia wazee wasitafute ajira nikupe namba yangu unirushie ili nipunguze idadi ya wazee wanaotafuta ajira wanaokukera.
 
Covid 19 ilikuwa ni janja janja ya mbowe na Magu.
Aliyekudanganya walikuwa na uadui kakuongopea.
 
PASCAL, PASCHAL, PASKALI ni jina la Kikristo. Sikuwahi kuona andiko katika vitabu vitakatifu linalosema watu wote watakwenda mbinguni bila masharti maana Mungu alishawasmehe Kwa kifo cha Yesu Msalabani.
Kwa hiyo wewe unapoleta andiko la kuwataka CHADEMA kuitisha kikao Peke yao, kuwasamehe Covid 19 bila wao kukiri kosa wlilotenda sijui unalitoa katika andiko gani au unàlitoa katika desturi gani? Wapi huko uliwahi kuona msamaha unatangazwa kabla ya mkosaji kukiri na kuomba kusamehewa?
Mt 18:15-17
15-Nduguyo akikukosea muonye mkiwa wawili Peke yenu, akikubali (AKIKIRI) umempata nduguyo.
16-Asipokubali chukua pamoja na mashahidi wawili au watatu......
17-Asipowasikiliza lijukishe Kanisa na asipowasikia na wao na awe kwako kama MTU WA MATAIFA na MTOZA USHURU.

1.Wameambiwa Peke yao hawakusikia.
2.Wakaitwa mashahidi wachache (Kamati Kuu) hawakushuka wala kukiri kosa.
3.Likaambiwa Kanisa(Wanachama wote) wakakaidi na kwenda mahakamani.

Sasa wamefanywa kama watu Baki, unawalàumu CHADEMA Kwa nini wasiwasamehe?
 
Figure of speech in quotation marks. Some kind of reward au mere gratification of the soul.
Thanks ila kwa ruhusa yako naomba kuitumia post yako hii kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Nimesoma mada zako nyingi kuhusu CHADEMA na sijashawishika kuwa zinaandikwa na mtu mwenye nia njema kuhusu hicho chama na upinzani kwa ujumla. Ni kama mtu anaye-celebrate ubabe wa chama dola kwa wapinzani na wananchi kwa ujumla.
Mkuu Drifter, honestly nimefarijika sana na comments zako, kwasababu kiukweli kabisa humu JF ni wachache sana wanaonisoma na kunielewa most of times naishia kutukanwa, kubezwa na kusimangwa, wenzangu wengi wa calibre yangu wenye ngozi laini, ama wameachana na JF, ama wapo wapo tuu kama hawapo, mimi naendelea kuwepo kwasababu naandika from my heart and I love it, 2024 nitakuwa naandikia magazeti 6!, na kipindi changu hiki,
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=BsKLwZgJL2nHPPqFkinarushwa kwenye vituo 5 vya TV, najihesabu very honest, truthfully, bonafide na genuine, kujua na wewe unanisoma, ni furaha yangu.
Ushauri wangu kwa Chadema ni very truthful na wenye nia njema ya kweli!. Mimi ni mmoja wa wana CCM ambao hata CCM ikiboronga, tunaibalasa, rais akiboronga tunambananisha.
Angalia mabandiko yangu haya kwa viongozi wa CCM - Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!
Na hata sasa Mama nae anakula spana za kutosha tuu, ila kwa vile ni Mwanamke, respect na humility is applied as well wakati spana za JPM zilikuwa ni spana za makavu live!. Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?

P
 
Andiko nzuri my Adv.Mayala, ila HAKUNA mgogoro ndani ya CHADEMA, huo mgogoro unaouna wewe kama mwandishi,
Mkuu Nkanini, kuna kitu kinachoitwa reality vs visibility, yaani muonekano, in reality Chadema ina mgogoro na hao 19, ila ni kweli kwa myopic visibility ya Chadema kwa ndani, wao ni hakuna mgogoro wowote, kwasababu kwao baada ya CC kuwatimua kwao hiyo issue imekwisha its final and conclusive. Hili jambo ukiliangalia from point of view of uchama Chadema, then you are right, hakuna mgogoro hili jambo limekwisha!, lakini ukiliangalia kwa jicho la haki bin haki, jee CC ya Chadema imewatendea haki?, jee wamefukuzwa kwa haki?, jee taratibu za kufukuza kwa mujibu wa katiba ya Chadema, zilifuatwa?. Halima Mdee ni Mwenyekiti wa Bawacha, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kusikiliza shauri lake na kumtimua?. Hoja yangu hapa kwenye hii issue, hakuna mkamilifu, Chadema sio wakamilifu kwasababu hawakuwaatimua kwa haki kwa mujibu wa katiba ya Chadema, hivyo the best option kwa muda uliobakia ni kuwasamehe, vinginevyo Chadema waitishe tena Baraza Kuu, wamalizane nao, na wakimalizana, wanarudi mahakamani, kufumba kufumbua ni 2025 hiyo!.
P.
 
issue hii CHADEMA walishatoa uamuzi wake na uamuzi ule ulikua kuwafukuza uanachama wale watuhumiwa,
Mkuu Nkanini, naamini katiba ya Chadema unaijua na umeisoma, imeweka utaratibu gani wa kuwafuta uanachama wanachama wake!, kwanini utaratibu huo haufuatwi?.
kwa shinikizo la chama dola wakaenda mahakamani
Nashauri kwenye hili lets deals with facts on hand, haki ya kutafuta haki mahakamani ni takwa la katiba ya JMT, hivyo hao 19 wanayo haki hiyo bila shinikizo kutoka popote au kwa yeyote, unless kama una ushahidi na uthibitisho wa hilo shinikizo!.
P
 
na hukumu imetoka, case hii imefungwa,
It's true hukumu imetoka case closed. Jee hukumu hii ni ya haki?. Imewatendea haki hawa 19?.

Jee wajua haki ya mtu huwa haipotei?.
Hoja kuu ya bandiko hili sio kuwaombea watu msamaha bali kuwafungua macho watu wenye macho lakini hawaoni!, na wana masikio, wanaambiwa lakini hawasikii!.

Chadema did the same kwa Juliana Shonza, Zitto Kabwe, Prof. Kitila Mkumbo, angalia mahali walipo sasa and compared kama wangekuwa Chadema?.

Pia kuna yule mlinzi wa Dr. Wilbroad Slaa, aitwae Khalid Kagenzi, kuna kitu alifanyiwa Chadema, kuna Mwigamba, kuna kitu alifanyiwa Arusha!.

Chadema fungueni macho muangalie nini kilikuja kuwatokea viongozi wa Chadema walioongoza operations hizo?. Can't you connect the dots kuwa it might be karna?.

Kama wale ni wachache tuu, hawakutendewa haki, karma zake ndio hizo, can you imagine what about hawa 19?.

Kama hawa 19 ni wakosaji, kwa kufoji na kujiteua, kwanini Chadema isithibitishe kwanza kosa, kisha ikawatimua kwa haki?.

Kama katiba ya Chadema imeweka utaratibu wake wa kuyashughulikia masuala ya nidhamu ndani ya chama, kuna ugumu gani kwa Chadema, kuufuata?.

A Best Way Forward
Kwa vile mahakama imeamuru kikao cha Baraza Kuu kifanyike upya kusikiliza rufaa zao,
  1. Chadema ianze moja, itoa tangazo la kufuta maamuzi batili ya CC kuwatimua, na badala yake itoe taarifa polisi ya kufanyika jinai ya forgery ndani ya Chadema katika barua za uteuzi
  2. Jeshi la polisi litawataka Chadema kuwasilisha bona-fide genuine headed paper zake stamped na kufanya uchaguzi wa forensic wa barua za uteuzi zilizowasilishwa NEC.
  3. Mamlaka ya kufanya uchaguzi wa kijinai Tanzania ni PT only. Hivyo Polisi wakijiridhisha kweli barua za uteuzi ni forgery, Chadema wanapewa uthibitisho wa evidence ya forgery.
  4. Wanaiandikia NEC kuripoti forgery hiyo na evidence ya polisi. NEC wanatoa barua za utenguzi wa ubunge wao na kuzipeleka Bungeni.
  5. Bunge linawatengua ubunge wao.
  6. Chadema inawaandalia hati 19 za mashitaka ya kufoji.
  7. Inaitisha kikao cha CC kuwasikikiza kwa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa katiba ya Chadema na kisha kuwatimua hao 18 isipokuwa Mdee kwasababu Mamlaka yake ya nidhamu sio CC ya Chadema.
  8. Wakikata rufaa, ndipo Chadema Inaitisha kikao cha Baraza Kuu na agenda mbili. Agenda ya kwanza ni kikao cha Baraza Kuu kama mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee, hiki kinakaa full kikiongozwa na mwenyekiti.
  9. Agenda ya pili ni kikao cha Baraza Kuu Chadema kama mamlaka ya rufaa ya wale Wabunge 18 kama watakata rufaa, hapa sasa ndio takwa la mahakama linafuatwa wajumbe wa CC ya Chadema waliowatimua hao 18, wanatoka nje.
  10. Jambo hili linakuwa limemalizika kwa haki na amani na Chadema inabaki salama.
P
 
na tuelewe kuwa kujiunga na chama cha kisiasa ni hiari ila ni muhimu katiba ya chama hicho kuiheshimu.
Mkuu Nkanini, hapa nakuunga mkono asilimia 100% chini ya 100%.
Tanzania yangu inahitaji kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Pia hapa Mkuu Nkanini, hapa nakuunga mkono asilimia 100% chini ya 100% ndio maana mimi mwenyewe nineisha pandisha mabandiko yanafika hata zaidi ya 100 kuzungumzia hitaji la uchaguzi wa huru na haki, utakao simamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
P
 
Mbowe alikwisha wasamehe ndio maana huwa hazungumzii hao watu ila walio mzunguuka Mbowe ndio tatizo!
Sintashangaa kama Mbowe atakuwa kinara kutaka hao covid19 wasamehewe kwani yeye na hao wanawake ndio vibaraka wa ccm. As long as Mbowe ni Mwenyekiti wa hicho chama kitaendelea kuwa saccos yake and the opposition will forever be weak!
 
Sintashangaa kama Mbowe atakuwa kinara kutaka hao covid19 wasamehewe kwani yeye na hao wanawake ndio vibaraka wa ccm. As long as Mbowe ni Mwenyekiti wa hicho chama kitaendelea kuwa saccos yake and the opposition will forever be weak!
Wee Mkuu Bulesi , usiseme hivi, wenyewe hawapendi maukweli ya kihivi!, niliwahi kuandika kitu humu, Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
P
 
Sintashangaa kama Mbowe atakuwa kinara kutaka hao covid19 wasamehewe kwani yeye na hao wanawake ndio vibaraka wa ccm. As long as Mbowe ni Mwenyekiti wa hicho chama kitaendelea kuwa saccos yake and the opposition will forever be weak!
Wafuasi watiifu hawataki kusikia hiii!
 
Paskal hawataweza kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…