Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 14,938
- 25,405
Kabla ya kuwatukana wana Mbeya kama ambavyo umefanya hapa, hebu jiulize kwanza maswali haya.Wana Mbeya sasa hivi jiji lenu limeteremka hadhi kabisa kwa sababu wamegundua kuwa kuna WAJINGA wengi. Ukiwaambia maandamano wanakuja.
Jiulize kwa nini wasipeleke Moshi? Wanajuwa Moshi watu ni wajanja hawatakubali kuacha kazi zao na kwenda kuunga mkono upuuzi.
Hiyo serikali yako imefanya nini mkoa wa Mbeya?
Pamoja na mapato yote yanayopatikana je Mbeya inastahili hali iliyonayo sasa?
Ameingia madarakani mtu wao zaidi ya zile Marathon na mikopo yake kafanya nini?
Wakasema wanajenga barabara kutoka Nsalaga mpaka Songwe mkataba wakaingia toka mwaka jana mwezi wa 3 mpaka juzijuzi ndio wameanza kujishughulisha na hiyo barabara napo kwa mwendo wa kusua sua.
Mnyonge mnyongeni wapeni haki yao wana Mbeya. Pengine hao Chedema ndio wanawasikiliza zaidi kuliko hiyo serikali yako.
Mkielimika mjifunze na madhara ya uchawa