Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Simjui ila kwakuwa kataka maoni yetu then najaribu kutengeneza picha fln kichwani mwake, kama anadhan mwanamke ni kwaajili ya ngono tu then sikumoja ngono haitakuwa ya muhimu akigundua kuna vitu vimemiss kwenye maisha yake, otherwise awe abnormal
Ndugu yangu, nashkuru sana kwa kutumia muda wako kunishauri. Ila sijui wewe ulipata wapi hiyo 'call' ya kutaka watoto kwa sababu mimi binafsi sihisi hiyo 'call'. Ila nahisi nahitaji mke tu.
 
Kwani wapi kasema mwanamke ni kwa ajili ya ngono tu?

Yani umeshindwa kumsoma mtu kwa ufahamu tu, utaweza vipi kutengeneza picha ya kichwani kwake vizuri?

Wewe una mawazo yako unayompandikizia mtoa mada.

Na kwa sababu hiyo, hujamtendea haki.
Asante kaka. Mwanamke ana nafasi ya kwa mwanaume ni si ngono tu.
 
Habari zenu wana-MMU.

Nataka maoni yenu katika hili swala. Swala hili linaonekana la ajabu kutokana na mila na tamaduni zetu za ki-Afrika ila SIO DHAMBI kabisa.

Mimi siitaji kuja kuwa na mtoto katika maisha yangu yote ila nataka kuoa niwe na mke TU. Hii ni kawaida sana kwa nchi za ulaya na marekani unakuta kuna familia/ndoa za namna hii nyingi sana lakini sio hapa Afrika. Hapa nyumbani(Tanzania) formula ni Ndoa = Watoto.

Ili ndoa ionekane imefanikiwa basi iwe na watoto japo mimi binafsi siamini hivyo.

Katika maamuzi hayo yawezekana ntakumbana na changamoto nyingi, lakini Kubwa ni Kupata mwanamke ambae atakubali kuwa ndani ya ndoa bila mtoto.

Wana MMU nipeni maoni yenu kuhusu hili swala kwa sababu sijiskii KABISA kuwa nina deni la kuwa na mtoto, sina tatizo lolote kiafya la kunizuia kuwa na mtoto ila SITAKI TU.

1. Mna maoni gani ?

2. Je, kuna msichana ambae anataka kuolewa lakini hana mpango wa kuzaa ?(kama baadhi ya wanawake wa ulaya/marekani)

Asanteni, mchana mwema.
Unaposema SIO DHAMBI KABISA unamaanisha nini? Kwa nini basi usifuate maandiko ya imani yako kwa vile umeshasema sio dhambi?
 
Tafuta wa kufanana nae wapo wanawake watakaokubali japo kibongobongo wachache....Kila la heri
 
Hakuna mwanamke atakayekubali kuolewa na wewe aise, na ukiona amekubali ujue hiyo ni kwa mda kwa sababu ana interest na wewe ya kitu fulani akishapata atakutupa, pia utakuja kukumbuka umuhimu wa watoto pindi ukizeeka, unaweza ufe kwa msongo wa mawazo hasa kipindi unapata matatizo uzeeni
 
Back
Top Bottom