Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Habari zenu wana-MMU.

Nataka maoni yenu katika hili swala.
Swala hili linaonekana la ajabu kutokana na mila na tamaduni zetu za ki-Afrika ila SIO DHAMBI kabisa.

Mimi siitaji kuja kuwa na mtoto katika maisha yangu yote ila nataka kuoa niwe na mke TU. Hii ni kawaida sana kwa nchi za ulaya na marekani unakuta kuna familia/ndoa za namna hii nyingi sana lakini sio hapa Afrika.
Hapa nyumbani(Tanzania) formula ni Ndoa = Watoto.

Ili ndoa ionekane imefanikiwa basi iwe na watoto japo mimi binafsi siamini hivyo.

Katika maamuzi hayo yawezekana ntakumbana na changamoto nyingi, lakini Kubwa ni Kupata mwanamke ambae atakubali kuwa ndani ya ndoa bila mtoto.

Wana MMU nipeni maoni yenu kuhusu hili swala kwa sababu sijiskii KABISA kuwa nina deni la kuwa na mtoto, sina tatizo lolote kiafya la kunizuia kuwa na mtoto ila SITAKI TU.

1. Mna maoni gani ?

2. Je kuna msichana ambae anataka kuolewa lakini hana mpango wa kuzaa ?(kama baadhi ya wanawake wa ulaya/marekani)

Asanteni, mchana mwema.
Kaoe marekani ikishindikana unioe mm, miezi ya kwanza ntakwambia mtoto staki, ila gafla bin vuuuu kijacho.
 
Ndoa isiyo na watoto, ni mwendo wa kutwa mara tatu, kama panadol. Raha.

Ila ndoa za hivyo uwe na hela. Yaani sehemu za kudinyanya ziwe zinabadilika badilika. Sio kila siku bedi hilo hilo. Mji huo huo. Nchi hio hio. Bara hilo hilo

I love my wife with my 3 children.
 
Kama hauna tatizo lolote kiafya ikitokea huyo mkeo akapata mimba utafanyaje?
Na je familia na ukoo wako utakuchukuliaje?
Fanya kile moyo wako Unapenda ila jiulize hayo maswali.
 
Ukizeeka ndio utajua umuhim wa watoto na wajukuu utakapokua unajikojolea kitandan na kupata bedsores utakosa hata wa kujuanika juan
 
Kwani hata mwanamke ntakaemuoa si ntawajibika kumtunza pia ? Chakula, mavazi, gharama za urembo.

Kwanza watoto sio gharama kama watu wanavyosema hasa kwa mtu ninaefanya kazi. Hawali saaana na nguo huwanunulii kila na ada ya masomo inalipwa mara moja tu kwa mwaka. Kwahiyo huo wajibu wa kuwatunza wala sio hoja kwa kweli.

Ukweli ni kwamba mimi SIONI haja/umuhimu wa kuwa na watoto. Sijawahi kuhisi nahitaji mtoto, labda hilo ndo swala la kunishutumu kama unataka kunishitumu.
Niliwahi kusikia mmarekani mmoja aliyekuwa mwanamitindo alifariki na kumwachia nyau/paka wake mabilioni ya pesa kwa kuwa hakuwa na mtoto, ndivyo unataka? Nendeni mkaijaze dunia mwanzo 1:28.....!,
 
Mie mwenyewe nataka mke wa kula nae raha tu ila watoto daaah!. Hebu nipe mbinu ulimpataje huyo mwanamke aliekubali kutozaa kaka ?
Kaka sijapata kwa hapa bongo sahau hilo
Chakufanya wee ni kuendelea kuwa mgegedaji tuu.

Kibongo bongo mpaka azae ndio ajione mwanamke au mwanaume.

Mie masuala ya ada sijui kulea sitaki kabisaaa....kwanza mie napenda papuchi hivyo maisha yangu sio marefu nikileta mtoto atateseka tuu.
 
Niliwahi kusikia mmarekani mmoja aliyekuwa mwanamitindo alifariki na kumwachia nyau/paka wake mabilioni ya pesa kwa kuwa hakuwa na mtoto, ndivyo unataka? Nendeni mkaijaze dunia mwanzo 1:28.....!,
Kumbuka hilo agizo lilitolewa wakati dunia ilikuwa paradiso sii dunia iliyojaa majanga na kuongozwa na shetani.

Tusichukulie poa jamani kuwa mzazi ni daraka kubwa sana. Kama huwezi bora utulizane tuu. Watu wanaleta watoto wanateseka tuu hapa duniani. Yaani ata mtoto mwenyewe analaani kizaliwa becoz maisha yake yote yanakuwa ni mateso filled with pockets of happiness
 
biblia ni ya wakati wote, ukisasa/uzungu usikuchanganye.... Uchoyo utakupeleka huko lengo la ndoa ni nini, Nani ataendeleza kizazi/uzao je unajua muhimu ya nguvu yako ya badae IPO kwa watoto, watoto ni zao la ndoa
 
Kuna watu wanajikuta wao ndo wanayajua sana maisha ya wenzao wewe fanya unaloona linakufurahisha

Hawa binadamu ukiwasikiliza sana watakuja kukuua siku si zako maisha ni mafupi san
Sio lazima kuwa na mtoto na pia sio lazima kuoa ni maamuz yako binafs
 
Kweli tunatofautiana maana mimi nnatamani katoto kakike hata leo navipenda sana vitoto vya ndugu zangu yaan
 
Anataka aendelee kufanya matusi
Aaaawwwwww

Umenikumbusha ujanani sikuwa najua kutongoza, kuna binti nilikuwa namtamani hatari, siku moja nikamfata nikamwambia fulani twende tukafanye matusi wooooiiiiiii alinitukana balaa
 
Aaaawwwwww

Umenikumbusha ujanani sikuwa najua kutongoza, kuna binti nilikuwa namtamani hatari, siku moja nikamfata nikamwambia fulani twende tukafanye matusi wooooiiiiiii alinitukana balaa

Ha haaaa ulitakiwa uanze na maneno matamu kwanza
 
Back
Top Bottom