Wana sayansi waanza kukukbali uwepo wa Mungu

Wana sayansi waanza kukukbali uwepo wa Mungu

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Katika makala haya, tutaangalia jinsi wanasayansi wa kawaida, tena ambao walikuwa hawaamini kabisa kwamba kuna Mungu au shetani, katika utafiti wao ambao haukuwa na uhusiano wowote na masuala ya rohoni, walijikuta wanagundua mambo ambayo yaliwatia hofu hadi wengine kukimbia kazi. Waliweza kusikia waziwazi sauti za vilio vya mateso kutokea katikati ya dunia! Sauti hizo walizirekodi; na mwisho wa makala haya utaona anwani inayoweza kukupeleka kuzisikia sauti hizo za kutisha na kusikitisha mno, mno!

Ni nani ambaye hajasikia habari za kwamba wanga huenda baharini, wakatupa mayai viza kisha malango yanafunguka nao wanashuka hadi kuzimu? Bila shaka habari hizi si ngeni masikioni mwa wengi wetu? Ni mambo ambayo ni rahisi kuaminika katika ulimwengu wa kawaida lakini unapoyaongelea kwa mtazamo wa Biblia, hapo watu wanaanza kukosa imani na kudhani kuwa si za kweli. Makala haya yanatokana na habari ambayo iliandikwa katika gazeti la Ammennusatia la kule Finland katika toleo lake la Julai 1989.

Sehemu ya gazetiKikundi kimoja cha wanajiologia (wana elimu ya miamba) wa Kirusi walikuwa katika mradi wa kutoboa tundu katika eneo la Kola, karibu na Murmansk; maili takriban 150 kaskazini mwa Duara la Aktiki, nchini Siberia. Watafiti hao waliweza kutoboa tundu ardhini lenye urefu wa kilometa 14.4 kwenda chini.

Dr Azzacov, ambaye alikuwa ndiye meneja wa mradi alisema kuwa wakati wa kutoboa, ghafla drili ilianza kuzunguka bila utaratibu, hali iliyoonyesha kwamba drili imefika kwenye sehemu iliyo na uwazi. Taarifa tunazokusanya ni za kushangaa sana, kiasi kwamba kwa kweli tumeingiwa na hofu maana hatujui kile tunachoweza kukikuta huko chini, alisema Dr Azzacov.

Jambo la pili lililotushangaza lilikuwa ni kiwango cha joto tulichokigundua katikati ya dunia. Mahesabu yanaonyesha kuwa joto hilo lilikuwa takribani nyuzi 1,000 za Selsiasi, aliongeza kusema Dr Azzacov. Hii ni zaidi ya kile tulichotegemea. Inaonekana ni kama moto wa jehanamu unawaka kwa nguvu sana humo ndani, katikati ya dunia!

Ugunduzi wa mwisho ndio uliokuwa wa kushitua sana masikioni mwetu kiasi kwamba wanasayansi wana hofu kubwa ya kuendelea na mradi huu. Tulikuwa tukijaribu kusikiliza mjongeo wa dunia kila baada ya muda fulani kwa kutumia vinasasauti vya hali ya juu sana (supersensitive microphones), ambavyo tulikuwa tukivishusha hadi chini kupitia kwenye tundu tulilotoboa.Dr Azaccov anaendelea kueleza kwamba, Kile tulichosikia, wanasayansi hawa ambao wamezoea tu kuamini mambo yanayoleta mantiki akilini, kiliwafanya kutetemeka kwa hofu kubwa mno! Wakati mwingine hicho tulichokisikia kilisikika kwa sauti ya chini lakini kali ambayo mwanzoni tulidhani inatokana na vifaa vyetu.Lakini baada ya kuvirekebisha, tulibaini kwamba zilikuwa ni sauti zilizotoka katikati ya dunia kabisa.

Hatukuamini masikio yetu. Tulisikia sauti ya mwanadamu akipiga kelele kwa maumivu. Japokuwa sauti moja ilikuwa inasikika kwa uwazi zaidi, tuliweza kusikia kwa nyuma sauti za maelfu, na huenda mamilioni ya watu wakilia kwa mateso na maumivu. Baada ya ugunduzi huu wa kutisha, nusu ya wanasayansi waliachana na mradi huo kutokana na hofu. Ni matumaini yangu kuwa hicho kilichoko huko chini kitabia hukohuko, aliongezea Dr Azzacov. Na kilichowamaliza kabisa nguvu hawa wanasayansi wa Kisovieti, mbali na hizo sauti walizozisikia, ilikuwa ni kutokea usiku uleule kwa gesi inayongaa kutoka kwenye tundu lile walilokuwa wamelitoboa; na katikati yake alijitokeza kiumbe mwenye mabawa kama ya popo pamoja na maneno yaliyokuwa yameandikwa kwa Kirusi Nimeshinda.

Baada ya mkasa huo, Dr Azzacove alisema, Mimi kama mkomunisti, siamini juu ya mbingu au Biblia, lakini kama mwanasayansi, hivi sasa naamini juu ya kuwapo kwa kuzimu. Ni kweli tuliogopa sana kutokana na ugunduzi huo. Lakini tunajua fika kile tulichokiona na kukisikia. Tunaamini kabisa kuwa tulitoboa tundu kwenye lango la kuzimu yenyewe!
 
Hakuna mwanasayansi mwenye akili timamu hasa natural thinking ability ambae anaamini the great architecture of the universe hayupo. Hayo ni maneno ya the secret society yaani freemason. G.A.O.U ultimately ni Mungu. Wale wanasayansi waliokariri hadi ubongo ume stack ndo wanaoyumbishayumbisha kuhusu uwepo wa Mungu.
 
Hakuna mwanasayansi mwenye akili timamu hasa natural thinking ability ambae anaamini the great architecture of the universe hayupo. Hayo ni maneno ya the secret society yaani freemason. G.A.O.U ultimately ni Mungu. Wale wanasayansi waliokariri hadi ubongo ume stack ndo wanaoyumbishayumbisha kuhusu uwepo wa Mungu.

indeed. The laws of physics are perfectly balanced with precise constants, and the sub atomic particles just have the right mass n charges to make life possible. The DNA complexity is way beyond comprehension. Mambo yote haya hayawezi kutokea by coincidence tu, God doesn't play dice!!
 
Wanasayansi hawajaanza leo kuamini kuwepo kwa mungu, sayansi haijali imani, inajali ujuzi.

Tuambie wanachojua, si wanachoamini.

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote, ukisema unajua, that's another story.

Sayansi si kama dini useme huyu mtume gani anaamini hivi nimfuate, sayansi inatazama uchunguzi.

Kutokuwa na jibu la kitu, au kupata matokeo usiyotegemea, hakumaanishi kwamba kuna mungu.

Inabidi uthibitishe kwamba mungu yupo ili kusema mungu yupo.
 
Katika makala haya, tutaangalia jinsi wanasayansi wa kawaida, tena ambao walikuwa hawaamini kabisa kwamba kuna Mungu au shetani, katika utafiti wao ambao haukuwa na uhusiano wowote na masuala ya rohoni, walijikuta wanagundua mambo ambayo yaliwatia hofu hadi wengine kukimbia kazi. Waliweza kusikia waziwazi sauti za vilio vya mateso kutokea katikati ya dunia! Sauti hizo walizirekodi; na mwisho wa makala haya utaona anwani inayoweza kukupeleka kuzisikia sauti hizo za kutisha na kusikitisha mno, mno!!

Ni nani ambaye hajasikia habari za kwamba wanga huenda baharini, wakatupa mayai viza kisha malango yanafunguka nao wanashuka hadi kuzimu? Bila shaka habari hizi si ngeni masikioni mwa wengi wetu? Ni mambo ambayo ni rahisi kuaminika katika ulimwengu wa kawaida lakini unapoyaongelea kwa mtazamo wa Biblia, hapo watu wanaanza kukosa imani na kudhani kuwa si za kweli.

Makala haya yanatokana na habari ambayo iliandikwa katika gazeti la Ammennusatia la kule Finland katika toleo lake la Julai 1989.

Sehemu ya gazeti

Kikundi kimoja cha wanajiologia (wana elimu ya miamba) wa Kirusi walikuwa katika mradi wa kutoboa tundu katika eneo la Kola, karibu na Murmansk; maili takriban 150 kaskazini mwa Duara la Aktiki, nchini Siberia. Watafiti hao waliweza kutoboa tundu ardhini lenye urefu wa kilometa 14.4 kwenda chini.

Dr Azzacov, ambaye alikuwa ndiye meneja wa mradi alisema kuwa wakati wa kutoboa, ghafla drili ilianza kuzunguka bila utaratibu, hali iliyoonyesha kwamba drili imefika kwenye sehemu iliyo na uwazi.

"Taarifa tunazokusanya ni za kushangaa sana, kiasi kwamba kwa kweli tumeingiwa na hofu maana hatujui kile tunachoweza kukikuta huko chini," alisema Dr Azzacov.

"Jambo la pili lililotushangaza lilikuwa ni kiwango cha joto tulichokigundua katikati ya dunia. Mahesabu yanaonyesha kuwa joto hilo lilikuwa takribani nyuzi 1,000 za Selsiasi," aliongeza kusema Dr Azzacov. "Hii ni zaidi ya kile tulichotegemea. Inaonekana ni kama moto wa jehanamu unawaka kwa nguvu sana humo ndani, katikati ya dunia!"

"Ugunduzi wa mwisho ndio uliokuwa wa kushitua sana masikioni mwetu kiasi kwamba wanasayansi wana hofu kubwa ya kuendelea na mradi huu. Tulikuwa tukijaribu kusikiliza mjongeo wa dunia kila baada ya muda fulani kwa kutumia vinasasauti vya hali ya juu sana (supersensitive microphones), ambavyo tulikuwa tukivishusha hadi chini kupitia kwenye tundu tulilotoboa."

Dr Azaccov anaendelea kueleza kwamba, "Kile tulichosikia, wanasayansi hawa ambao wamezoea tu kuamini mambo yanayoleta mantiki akilini, kiliwafanya kutetemeka kwa hofu kubwa mno! Wakati mwingine hicho tulichokisikia kilisikika kwa sauti ya chini lakini kali ambayo mwanzoni tulidhani inatokana na vifaa vyetu."

"Lakini baada ya kuvirekebisha, tulibaini kwamba zilikuwa ni sauti zilizotoka katikati ya dunia kabisa. Hatukuamini masikio yetu. Tulisikia sauti ya mwanadamu akipiga kelele kwa maumivu. Japokuwa sauti moja ilikuwa inasikika kwa uwazi zaidi, tuliweza kusikia kwa nyuma sauti za maelfu, na huenda mamilioni ya watu wakilia kwa mateso na maumivu.

"Baada ya ugunduzi huu wa kutisha, nusu ya wanasayansi waliachana na mradi huo kutokana na hofu. Ni matumaini yangu kuwa hicho kilichoko huko chini kitabia hukohuko," aliongezea Dr Azzacov.

"Na kilichowamaliza kabisa nguvu hawa wanasayansi wa Kisovieti, mbali na hizo sauti walizozisikia, ilikuwa ni kutokea usiku uleule kwa gesi inayong'aa kutoka kwenye tundu lile walilokuwa wamelitoboa; na katikati yake alijitokeza kiumbe mwenye mabawa kama ya popo pamoja na maneno yaliyokuwa yameandikwa kwa Kirusi ‘Nimeshinda'."

Baada ya mkasa huo, Dr Azzacove alisema, "Mimi kama mkomunisti, siamini juu ya mbingu au Biblia, lakini kama mwanasayansi, hivi sasa naamini juu ya kuwapo kwa kuzimu. Ni kweli tuliogopa sana kutokana na ugunduzi huo. Lakini tunajua fika kile tulichokiona na kukisikia. Tunaamini kabisa kuwa tulitoboa tundu kwenye lango la kuzimu yenyewe!"

Nani aliwahi kukuambia kuwa WanaSayansi hawakubali uwepo wa Mungu? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa nchi yetu Tanzania haina dini, je unadhani alimaanisha kuwa WaTanzania hawana dini? Tofautisha kati ya Sayansi na WanaSayansi, Sayansi ndiyo haikubali uwepo wa Mungu lakini si WanaSayansi
 
Wanasayansi hawajaanza leo kuamini kuwepo kwa mungu, sayansi haijali imani, inajali ujuzi.

Kutokuwa na jibu la kitu, au kupata matokeo usiyotegemea, hakumaanishi kwamba kuna mungu.
Hiyo Bold rekebisha kidogo ndugu yangu isomeke kama nilivyojaribu kui-edit hap chini

Kutokuwa na jibu la kitu, au kupata matokeo usiyotegemea, hakumaanishi kwamba kuna mungu AU HAKUNA MUNGU
 
indeed. The laws of physics are perfectly balanced with precise constants, and the sub atomic particles just have the right mass n charges to make life possible. The DNA complexity is way beyond comprehension. Mambo yote haya hayawezi kutokea by coincidence tu, God doesn't play dice!!

teh teh . . . .God doesnt play dice! hii nimeipenda! Mungu hafanyi siasa!
 
Wanasayansi hawajaanza leo kuamini kuwepo kwa mungu, sayansi haijali imani, inajali ujuzi.

Tuambie wanachojua, si wanachoamini.

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote, ukisema unajua, that's another story.

Sayansi si kama dini useme huyu mtume gani anaamini hivi nimfuate, sayansi inatazama uchunguzi.

Kutokuwa na jibu la kitu, au kupata matokeo usiyotegemea, hakumaanishi kwamba kuna mungu.

Inabidi uthibitishe kwamba mungu yupo ili kusema mungu yupo.

Kwa kauli hii namwomba Mungu ajithibitishe yeye mwenyewe kwako na kwa wengine wasioamini uwepo wake. Afanye hivyo sio kwa utashi wangu mimi binadamu bali kwa utashi wake yeye mwenyewe kama Mungu. Amen.
 
Nani aliwahi kukuambia kuwa WanaSayansi hawakubali uwepo wa Mungu? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa nchi yetu Tanzania haina dini, je unadhani alimaanisha kuwa WaTanzania hawana dini? Tofautisha kati ya Sayansi na WanaSayansi, Sayansi ndiyo haikubali uwepo wa Mungu lakini si WanaSayansi

Je mwl Nyerere alikuwa ni mwana sayansi?
 
Hiyo Bold rekebisha kidogo ndugu yangu isomeke kama nilivyojaribu kui-edit hap chini

Kutokuwa na jibu la kitu, au kupata matokeo usiyotegemea, hakumaanishi kwamba kuna mungu AU HAKUNA MUNGU

Since you cannot prove a negative anyway, the part that says "au hakuna mungu" is redundant like the "ay" in "okay".
 
Back
Top Bottom